Hija ya Kitume ya Papa Francisko Malta:Imani inakua katika kujitoa zawadi
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Dominika tarehe 3 Aprili 2022 kabla ya sala ya Malaika wa Bwana, ameshukuru maneno Kardinali Charles Scicluna aliyomwelekea kwa niaba ya wote. Lakini Papa amesema ndiye anapaswa kutoa shukrani kwao. kwa maana hiyo Papa amependa kuonesha utambuzi na shukrani zake kwa Rais wa Jamhuri na Mamlaka, ndugu zake maaskofu, wapendwa mapadre, watawa kike na kiume, wazalendo na waamini wote wa Malta na Gozo kwa makaribisho yao na upendo alioupokea. Papa amebainisha kwamba jioni mara baada ya kukutana na ndugu kaka na dada wahamiaji, itakuwa ndiyo saa ya kurudi Roma, lakini ataondoka akipeleka rohoni mwake, vipindi vyote na maneno aliyosikia katika siku hizi. Hasa kwa kuhifadhi ndani ya moyo wake sura nyingi, na angavu ya Malta. Amewashukuru hata wale ambao wamefanya kazi kwa ajili ya kufanikisha ziara yake na kuwasalimia kwa upendo kaka na dada wa madhehebu mbali mbali ya kikristo na kidini ambao amekutana nao. Kwa wote Papa amewamoba wasali kwa ajili yake na yeye atafanya hivyo hivyo
Visiwa vya Malta na Gozo vinauishwa na maana ya Watu wa Mungu
Baba Mtakatifu Francisko amesema kwamba katika visiwa hivyo vinauishwa na maana ya Watu wa Mungu. Amewaomba waendelee mbele hivyo kwa kukumbuka kuwa imani inakua katika furaha na kuongezeka katika kujitoa zawadi. Amewaomba wandeleeze katika mnyororo wa utakatifu ambao ulipelekea watu wengi wa Malta kujitoa kwa shauku kwa Mungu na kwa wengine. Papa amefikiria Dun Ġorġ Preca, aliyetangazwa Mtakatifu miaka kumi na tano iliyopita.
Kwa vijana: Mungu kamwe hatawakatisha tamaa
Hatimaye Baba Mtakatifu Francisko amependa kuelekeza neno moja kwa vijana ambao amebainisha ndiyo mstakabali wao. Papa Francisko amesema anashirikishana na vijana jambo moja zuri sana katika maisha. Je wanafahamu ni nini? Ni furaha ya kuitumia katika upendo ambao unawafanya kuwa huru. Lakini furaha hiyo amesema inaitwa jina lake: “Yesu”. Baba Mtakatifu amewatakia matashi mema ya kuwa na uzuri wa kuweza kumpenda Yesu, ambaye ni Mungu wa huruma, kwa kuwakumbusha jinsi walivyosikia katika Injili, na ambaye anawaamini, anaota ndoto na wao, anapenda maisha yao na kamwe hawakatishi tamaa. Na ili kwenda mbele daima na Yesu hata na familia,na watu wa Mungu, wasisahau mizizi. Papa amewashauri wazungumza na bibi na babu pamoja na wazee!
Maombi kwa ajili ya amani nchini Ukraine
Kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu Francisko amesema, kwamba Bwana wasindikize na Mama awalinde. Kwa kuongezea Papa amerudi tena katika suala la hali halisi inayozunguka nchi ya Mashariki mwa Ulaya na hivyo ameomba kusali kwa ajili ya amani, akifikiria janga la kibinadamu la mateso ya Ukraine, ambayo bado iko chini ya mabomu, ya vita hivyo vya kinyama”. Papa ameomba wasichoke kusali na kusaidia anayeteseka. Amani iwe kwao.