Hija ya Kitume ya Papa Francisko Malta:Maswali na majibu kwa waandishi wa habari
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, akizungumza na waandishi wa habari kwenye ndege wakati wa kurudi kutoka Malta katika ziara yake ya kitume ya 36 ya kimataifa na kujibu maswali hasa baada ya kukumbuka kile alichoshangazwa na makaribisho, katika visiwa, amerudia kuzungumzai juu ya vita na kwama “bado hatujajifunza! Bwana atuhurumie, wote kwa pamoja, wote tuna makosa” Matatizo ya wahamiaji ni makubwa sana kwa sababu iwe Ugiriki, Cyprus, Italia, Hispania, na Nchi hizi ziko karibu na Afrika na Nchi za Mashariki ya Kati, ambao watafika, na watawendelea kufika, hivyo lazima wapokelewe daima”, Papa alsisiza. Akiendelea Papa alisema “Tatizo ni kwamba kila serikali lazima iseme ni watu wangapi iweza kuwa nao wa kuishi hapo. Kwa maana hiyo inahitajika makataba wa Nchi za Bara la Ulaya na wale wote ambao wako tyari kupokea wahamiaji”.
Kufuatia na maswali aliyoulizwa kuhusu kushangazwa na kwenda kwenye Kikanisa alichozikwa Mtakatifu George Preca, na sababu ya kufanya hivyo na kuhusu afya yake swali alililoulizwa na mwandishi wa (TVM), Papa alisema kuwa Afya yake kidogo ina matatizo kwa sababu tatizo la goti ni la muda mrefu, lakini anaendelea taratibu kuwa afadhali anaweza kwenda. Wiki mbili zilio pita hasingeweza kufanya lolote. Na kuhusu Malta, amefurahi kuhusu ziara hiyo ameona hali halisi na shauku ya watu nzuri iwe kwa upande wa Gozo, Malta, Valletta na sehemu nyingine. Shauku kubwa njiani, na amebaki ameshangazwa na watu hao kwa ukarimu. Ilikuwa ni ziara fupi.
Hata hivyp Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kwamba tatizo kubwa ambalo ameliona ni tatizo la uhamiaji. Tatizo la uhamiaji ni kubwa kwa sababu Ugiriki, Cyprus, Malya, Italia, Uhispania ni nchi ambazo zimepakana na Afrika na Nchi za Mashariki ya Kati na wanashukua wahamiaji wengi. Wahamiaji lazima wakaribishwe kila wakati! Shida ni kwamba kila serikali inapaswa kusema ni watu wangapi inaweza kupokea kwa kawaida ili waishi huko. “Kwa hili tunahitaji makubaliano na nchi za Ulaya, ambayo si wote wako tayari kupokea wahamiaji. Tunasahau kuwa Ulaya iliundwa na wahamiaji, sivyo? Lakini hivyo ndivyo ilivyo… Angalau bila kuacha mzigo wote kwa nchi hizi jirani ambazo ni wakarimu sana, na Malta ni mojawapo”, amsema Baba Mtakatifu.
Kwa kuongeza Baba Mtakatifu amesema “Leo nilikuwa katika kituo cha kukaribisha wahamiaji na mambo niliyoyasikia huko ni mabaya: mateso ya hawa kufika huko na baadaye katika kambi, ni kambi ambazo ziko pwani ya Libya, na wakati wanarudishwa. Hii inaonekana jinai. Na kwa hili naamini kuwa ni shida inayogusa moyo wa kila mtu. Na kama ilivyo Ulaya kwa sasa ambayo inaweka nafasi kwa ukarimu kwa Waukraine wanaobisha hodi mlangoni, vivyo hivyo na wengine wanaotoka Mediterania. Hii ni hatua ambayo wakati wa kuhitimisha ziara na ilinigusa sana, kwa sababu nilihisi shuhuda, mateso, ambayo ni zaidi au kidogo kama yale ambayo nadhani nilisema juu yake na yamo ndani ya kitabu kidogo kilichochapishwa, Hermanito, kwa Kihispania, “ndugu mdogo,” na njia zote za misalaba za watu hawa. Mmoja aliyezungumza leo alilazimika kulipa mara nne. Ninawaomba mfikirie juu ya hili”, Papa alisisitiza
Akijibu swali la pili kutoka kwa mwandishi wa Radio ya Kihispania ameuliza kuhusiana na suala la kwenda Kiev na wakati akiwa huko Malta ametoa mwaliko kuhusu ukaribu wa watu wa Ukraine, na zaidi baada ya kusikia taarifa kuhusu picha za Bucha, eneo karibu na Kiev, lililoachwa na wanajeshi wa Urussi wakatuta maiti nyingi sana zimetupwa barabani, nyingine zimefungwa, na hata kwenye maziko ya alaiki, je ziara hii kweli inawezekana?
Baba Mtakatifu Francisko amemshukuru kwa kumwambia habari hiyo ambayo hakujua. “Vita siku zote ni ukatili, jambo lisilo la kibinadamu na linakwenda kinyume na roho ya mwanadamu, sisemi Mkristo, mwanadamu. Ni roho ya Kaini. Niko tayari kufanya lolote linaloweza kufanywa; na Vatican hasa upande wa kidiplomasia, Kadinali Parolin, Monsinyo Gallagher, wanafanya kila kitu, huwezi kuchapisha kila kitu wanachofanya, kwa busara, kwa usiri, lakini tuko kwenye kikomo cha kazi. Miongoni mwa uwezekano ni kusafiri”.
Baba Mtakatifu aidha amebanisha kwamba:“Kuna safari mbili zinazowezekana: moja, Rais wa Poland ameniomba nimtume Kardinali Krajewski kutembelea Waukraine ambao wamepokelewa huko Poland. Tayari alikwenda mara mbili, alipeleka magari mawili ya wagonjwa akakaa nao, lakini atafanya tena safari hiyo, yuko tayari kufanya hivyo. Safari nyingine ambayo mtu mwingine kaniomba, ni zaidi ya moja: Nilisema kwa uaminifu kwamba nilikuwa na nia ya kwenda huko, nilisema kuwa kuna uwezekano daima, hakuna ukuu hapana, niko tayari”.
Baba Mtakatifu amesema “Unafikiria nini juu ya safari ... Swali lilikuwa hivi: Tulisikia kwamba unafikiria safari ya Ukraine, na nikasema: “Iko kwenye meza”, mradi, iko pale, kama moja ya mapendekezo yaliyofika, lakini sijui ikiwa inawezekana kufanywa, ikiwa ni rahisi kuifanya, ikiwa kuifanya itakuwa bora, ikiwa ni rahisi kuifanya na lazima niifanye, yote haya, inasubiri. Baadaye kwa muda, mkutano na Patriaki Kirill ulikuwa umefikiriwa: hili linafanyiwa kazi, tunafanya kazi na tunafikiria kufanya hivyo katika Mashariki ya Kati. Hivi ndivyo mambo yalivyo sasa”.
Baba Mtakatifu Francisko akijubu swali la Gerry O’Connell (America Magazine) wa (Gazeti la Marekani) kuhusiana na vita, na mwanzoni aliweza kuzungumza na Rais Putin lakini leo hii anaweza kueleza nini, Papa amejibu, “Mambo niliyoyasema kwa Mamlaka za kila sehemu ni hadharani. Hakuna hata moja ya mambo ambayo nilisema na ambayo yamehifadhiwa kwa ajili yangu. Nilipozungumza na Patriaki alitoa kauli nzuri ya kile tulichoambiana. Nilimsikia Rais wa Urusi mwishoni mwa mwaka aliponipigia simu kunipongeza, tukazungumza. Kisha, nilimsikia pia Rais wa Ukraine, mara mbili. Na nilifikiri, siku ya kwanza ya vita, kwamba nilipaswa kwenda Ubalozi wa Kirussi kuzungumza na Balozi, ambaye ni mwakilishi wa watu, na kuuliza maswali na kutoa maoni yangu juu ya kesi hiyo. Hayo ndiyo mawasiliano rasmi ambayo nimekuwa nayo. Nikiwa na Urussi nilifanya hivyo kupitia Ubalozi”.
Baba Mtakatifu akiendelea amesema “zaidi ya hayo, nilisikia kutoka kwa Askofu Mkuu wa Kiev, Shevchuk. Baadaye kila baada ya siku mbili au tatu, mara kwa mara, nilimsikia mmoja wenu, Elisabetta Piqué, ambaye sasa yuko Odessa, lakini nilimsikia alipokuwa Lviv. Ninamsikia na ananiambia jinsi mambo yalivyo. Pia nilizungumza na mkuu wa seminari pale, nikiwa na ujumbe kwa wanasemina na watu wa huko. Pia ninawasiliana na mwakilishi wako. Na nikizungumza haya ningependa kutoa pole kwa wenzako waliokufa. Haijapishi upande wowote ule. Lakini kazi yako ni kwa manufaa ya wote na wamefia katika huduma ya manufaa ya wote, ya habari. Tusiwasahau. Wamekuwa wajasiri na ninawaombea, kwamba Bwana awape tuzo kwa kazi yao. Hizi ndizo habari ambazo tumekuwa nazi kwa sasa”.
Baba Mtakatifu aidha amesema “Ujumbe nilioutoa kwa Mamlaka zote ndio ninafanya hadharani. Sifanyi mazungumzo mara mbili. Siku zote ni sawa. Ninaamini kuwa chini ya swali lako pia kuna shaka juu ya vita tu au vita visivyo vya haki. Kila vita huzaliwa na ukosefu wa haki, daima. Kwa sababu ni mpango wa vita, sio mpango wa amani. Kwa mfano, kufanya uwekezaji kununua silaha. Wananiambia: lakini tunahitaji kujitetea. Na huu ndio mpango wa vita. Vita vya Kidunia vya pili vilipoisha, kila mtu alipumua na kusema “pasiwepo vita tena: bali amani.” Na wimbi la kazi ya amani lilianza, hata kwa nia nzuri ya kutotengeneza silaha, zote, hata silaha za atomiki, wakati huo, baada ya Hiroshima na Nagasaki”.
Baba Mtakatifu amesema hii “Ilikuwa nia njema kubwa. Miaka sabini baadaye, miaka themanini baadaye tumesahau haya yote. Ni kama hii: mpango wa vita umewekwa. Matumaini makubwa kwa kazi ya Umoja wa Mataifa wakati huo. Lakini mtindo wa vita umejiweka kwa mara nyingine tena. Hatuwezi kuwa na uwezo wa kufikiria mpango mwingine, kufikiri na mpango wa amani. Kumekuwa na watu wakuu: Ghandi na wengine wengi, ambao nimewataja mwishoni mwa Waraka wa “Sote ndi Ndugu” ambao wamechezwa kamari juu ya mpango wa amani. Lakini sisi ni wakaidi! Sisi ni wakaidi kama wanadamu. Tunapenda vita, na roho ya Kaini. Si kwa bahati kwamba mwanzoni mwa Biblia kuna tatizo hili: roho ya “Kaini” ya kuua, badala ya roho ya amani. “Baba, huwezi! ...”.
Baba Mtakatifu aamependa kusema jambo lake binafsi kwamba: “ninawambia kitu cha kibinafsi: nilipokwenda Redipuglia mwaka wa 2014 na kuona majina, nililia. Kweli, nililia, kwa uchungu. Mwaka mmoja au miwili baadaye, kwa siku ya Marehemu wote nilikwenda kuadhimisha Misa huko Anzio, na huko pia niliwaona vijana waliokufa wakitua huko Anzio: kulikuwa na majina, na wote vijana. Na huko pia nililia. Ya kweli. Sikuelewa. Ni lazima tulie juu ya makaburi. Ninaheshimu, kwa sababu kuna tatizo la kisiasa, lakini ilipofanyika kumbukumbu ya kutua kwa Normandy, wakuu wa serikali walikusanyika kuadhimisha; lakini sikumbuki kama kulikuwa hata mmoja aliyewataja wale vijana elfu thelathini waliobaki kwenye fukwe za bahari. Boti zilifunguliwa, zikatoka nje na zilipigwa risasi na mashine huko, kwenye fukwe. Je, kwa vijana haijalishi? Hii inanifanya nifikirie na kuniumiza. Nimesikitishwa na yanayotokea leo hii. Hatujifunzi. Bwana atuhurumie sisi sote. Sisi sote tuna hatia!”,
Msemaji wa vyombo vya habari Dk. Bruni alimshukuru Baba Mtakatifu na muda ndiyo ulikuwa unawaacha na Papa akarudia kushuru sana kwa kazi yao, ya mawasiliano, na ni matarajio ya kuwaona tena wakati mwingine. Amewashukuru kwa uvumilivu wao na habari zao. Waendelee mbele na kutua kwema kwa ndege.