Tafuta

Papa amekutana na wahamiaji katika kituo cha Yohane XXIII wakati wa ziara yake ya kitume nchini Malta Papa amekutana na wahamiaji katika kituo cha Yohane XXIII wakati wa ziara yake ya kitume nchini Malta 

Hija ya Kitume ya Papa Francisko Malta:Ndoto ya Papa wahamiaji kuwa mashuhuda wa ukarimu

Papa Francisko akikutana na kundi la mwisho kabla ya kurudi Roma baada ya siku hizi mbili za ziara yake ya Kitume amefafanua ndoto yake kwamba wahamiaji wanaweza kugeuka kuwa watu mashuhuda na uuishaji wa ukarimu na udugu.Kuanzia hapo na pale ambapo Mungu atapenda na kuwaongoza katika njia.Amesema hayo akiwa katika kituo cha Wahamiaji cha Yohane XXIII huko Malta.

Na Angella Rwezaula- Vatican.

Papa Francisko Dominika tarehe 4 Aprili 2022 amekutana na wahamiaji huko Hal Far, katika Kituo cha Yohane XXIII, kiwa ndiyo kituo cha mwisho wa hija yake ya 36 ya kitume katika Kisiwa cha Malta na Gozo kabla ya kuanza safari ya kurudi Roma.  Mara baada ya salamu, hotuba za Padre Dionizio (OFM) na shuhuda mbili za wahamiaji, Papa Francisko ameanza hotuba yake na salamu za upendo akiwa na furaha ya kuhitimisha ziara yake huko Malta kwa kukutana nao. Ameshukuru Padre Dionizio kwa makaribisho yake hasa shukrani kwa Daniel na Siriman waliotoa ushuhuda, ambao amesema wamefungua moyo kwao  na maisha yao, na wakati huo huu wamekuwa wasemaji wakuu wa kaka na dada waliolazimika kuacha nchi zao ili kutafuta kimbilio salama.

Mkutano wa Papa Francisko na wahamiaji huko Malta
Mkutano wa Papa na wahamiaji na wakimbizi
Mkutano wa Papa na wahamiaji na wakimbizi

Papa Francisko amekumbusha maneno aliyosema hivi karibuni huko Lesvos kuwa yeye amekwenda hapokuwa karibu nao, kuwaona nyuso zao na  kuwatazama macho yao (Hotuba huko Mytilene, 5 Desemba 2021). Tangu siku alipokwend Lampedusa hakuweza kuwasahau kamwe. Daima anawakumbuka moyoni mwake na daima anawaombea. Katika mkutano na wahamiaji, Papa amebainisha kuwa  pale ndipo kilikuwa kiini cha Kauli mbiu ya Ziara yake ya kitume huko Malta. Hiyo ni nukuu kutoka katika Kitabu cha Matendo ya Mitume kisemacho: “Wenyeji wakatufanyia fadhili zisizokuwa za kawaida.”(Mdo 28: 2). Inahusu jinsi Watu wa Malta walivyomkarimu Mtume Paulo na wale wote aliokuwa nao katika kisiwa, Papa ameongeza kusema kwamba walikirimiwa na ubinadamu adimu”. Hilo la ajali ya meli ni tukio ambalo maelfu ya wanaume, wanawake na watoto wamekuwa nalo katika miaka ya hivi karibuni katika Mediterania. Na kwa bahati mbaya kwa wengi wao ilikuwa ya kusikitisha. Papa Francisko ameongeza kusema: “Hapo jana habari ziliibuka za uokoaji uliofanyika katika pwani ya Libya, wa wahamiaji wanne pekee yao  tu kutoka kwenye boti iliyokuwa na takriban  watu tisini. Tuwaombee hawa ndugu zetu waliofariki katika bahari yetu ya Mediterania. Na pia tunaomba kuokolewa kutoka humo lakini kuna ajali nyingine ya meli ambayo inafanyika wakati matukio haya yanatokea: ni ajali ya ustaarabu, ambayo inatishia sio tu wakimbizi, lakini sisi sote.

Mkutano wa Papa na wahamiaji na wakimbizi
Mkutano wa Papa na wahamiaji na wakimbizi

Je, tunawezaje kujiokoa na ajali hii inayotishia kuzamisha meli ya ustaarabu wetu? Baba Mtakatifu ametoa jibu kwamba ni kwa kuwa na tabia ya ubinadamu. Kwa kutazama watu si kama adui lakini jinsi walivyo, kama alivyosema Siriman, yaani nyuso za historia, kwa urahisi wanawake na wanaume na kaka na dada. Kwa kufikiria kwamba nafasi ya mtu yule nimwonaye kwenye mtumbwi au meli ai katika bahari kwenye televisheni au katika picha, nafasi yake ingekuwa mimi, au mwanangu wa kike na kiume… Labda hata wakati huo huo wakiwa kwenye mkutano huo, wengine wako wanakatisha bahari kutoka kusini kwenda Kaskazini… Papa ameomba kusali kwa ajili ya Kaka na dada ambao wanaatarisha maisha baharini wakitafuta tumaini. Hata waliotoa ushuhuda waliishi janga hilo kabla ya kufika mahali walipo. Historia yao inafanya kufikiria wale maelfu na maelfu ya watu ambao kwa siku hizi wamefurika wakilazimika kukimbia kutoka Ukraine kwa sababu ya vita. Lakini watu wengi hao wanawake na wanaume katika kutafuta mahali salama walilazimika kuacha nyumba zao na ardhi zao kutoka Asia, Afrika na katika Bara la Amerika. Kwa wote hao, baba mtakatifu anawafikiria na kuomba kwa ajili yao.

Mkutano wa Papa na wahamiaji na wakimbizi
Mkutano wa Papa na wahamiaji na wakimbizi

Ppa ameongeza kusema: “Wakati fulani uliopita nilipokea ushuhuda mwingine kutoka Kituo chenu: hisotria ya kijana ambaye alisimulia wakati uchungu ambao alilazimika kumwacha mama yake na familia yake ya asili. Hili lilikuwa limenisukuma na kunifanya nifikirie. Lakini wewe pia Daniel, wewe Siriman, na kila mmoja wenu ameishi uzoefu huu wa kuanza kwa kujitenga na mizizi yenu. Ni machozi. Chozi linaloacha alama yake. Sio tu maumivu ya kitambo, ya kihisia. Inaacha jeraha la kina katika njia ya ukuaji wa mtoto mdogo, wa mwanamke mdogo. Inachukua muda kuponya jeraha hili; inachukua muda na juu ya yote inachukua uzoefu tajiri katika ubinadamu: kukutana na watu wa kukaribisha ambao wanajua jinsi ya kusikiliza, kuelewa, kusindikiza; na pia kuwa pamoja na wasafiri wengine, kushiriki, kubeba uzito pamoja… Hii inasaidia kuponya majeraha”, Papa amewashauri. Papa amefikiria vituo vingi vya makaribisho na jinsi  ilivyo muhimu kuwa sehemu za kibidamua. Ni ngumu, kuna miktadha mingi sana inayokuza mivutano na ugumu. Lakini pamoja na hayo Baba Mtakatifu ameshauri kuwa kila bara, kuna watu na jumuiya ambazo zinakubaliana na changamoto kwa utambuzi kuwa uhamiaji ni ishara ya nyakati, mahali ambapo panahitajika uthubutu wa ustaarabu. Kwa wakristo ni mchezo wa imani katika Injili ya Yesu ambayo alisema: “Nilikuwa mgeni na mkanikaribisha (Mt 25, 35). Lakini hiyo haijengwi kwa siku moja. Inahitaji muda, na uvumulivu mwingi na zaidi inahitaji upendo unaofanywa kwa ukaribu, kwa huruma, kama upendo ule wa Mungu kwetu sisi. Ni matumaini makubwa kwa Papa kwamba wanaweza kweli kufanya mambo makubwa na ameshukuru awali ya yote kukubali changamoto hiyo huko  ambayo imetoa maisha ya Kituo hicho, amewaomba wapigiwe makofi....

Mkutano wa Papa na wahamiaji na wakimbizi
Mkutano wa Papa na wahamiaji na wakimbizi

Papa Francisko hata hivyo amefafanua juu ya ndoto yake, kwamba wahamiaji siku moja wanaweza kugeuka kuwa watu mashuhuda na uuishaji wa ukarimu na udugu. Kuanzia hapo na pale ambapo Mungu atapenda na kuwaongoza katika njia. Na ndiyo ndoto yake ambayo amependa kushirikishana na kuikabidhi mikononi mwa Mungu. Kwa saababu kile ambacho hakiwezekani kwa binadamu kwa Mungu inawezakana. Anafikiria kwamba hiyo ni muhimu katika  ulimwengu leo hii katika uhamiaji ambao wanaweza kuwa mashuhuda wa thamani za binadamu, msingi kwa maisha ya hadhi na udugu. Hizo ni thamani ambazo wanazo ndani mwao, na zinatokana na mzizi yao. Mara tu wanapoondolewa majeraha, wao wataweza kweli kuwa na utajiri wali nao ndani mwao,  urithi wa ubinadamu msingi ambao utawekwa kwa pamoja katika jumuiya ambazo zitawakaribisha na mazingira ambayo watakuwapo. Hiyo ni njia ya udugu na urafiki kijamii. Hapo kunwa wakati ujao wa familia ya binadamu iliyo na utandawazi. Papa amefurahi kuweza kushirikishana na ndiyo  ushuhuda na  kuwaomba washirikishane ndoto zake. Kwa upande wa mtoa ushuhuda Siriman, amekumbusha alivyo acha nchi yake na sehemu ya ndoto moyoni. Ndoto ya uhuru na demokrasia. Hiyo ni ndoto kweli ambayo inakutana na ugumu, mara nyingi hatari na isiyosemekana, isiyo ya kibinadamu. Kwa maana hiyo yeye ametoa sauti na wito kwa ajili ya mamilioni ya wale waliosongwa ambapo haki msingi zimekiukwa na kwa bahati mbaya kuungwa mkono na baadhi ya mamlaka husika. Papa amesema  juu ya wito wa kuweka umakini katika msingi wa hadhi ya mtu. Amesema hayo kwa maneno yake kwamba “ninyi sio idadi bali ni watu wenye mwili na mifupa, nyuso na wakati mwingine zenye mateso”.

Mkutano wa Papa na wahamiaji na wakimbizi
Mkutano wa Papa na wahamiaji na wakimbizi

Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu amesema inawezekana kuanzia hapo, kwa hadhi yao. Papa ameomba wasiache wadanganywe na yule anayesema: “Hakuna la kufanya, ni matatizo makubwa zaidi yetu”, “mimi ninafanya kazi yangu na wengine watajijua”. Hapana! Papa amerudia kusema kuwa wasiangukie katika mtego huo. Wajibu kwa changamoto ya wahamiaji na wakimbizi kwa mtindo wa ubinadamu, wawashe moto wa udugu, wakizingatia kiini cha mtu ambaye anaweza kupata joto kuamka na kuwasha tumaini. Papa ameomba waongeza nguvu katika tambaa la urafiki wa kijamii  wa kukutana, kwa kuanzia  katika maeneo kama hayo ambayo kwa hakika hayatakuwa kamilifu lakini “ni maabara ya amani”. Kwa kuwa kituo hicho kinaitwa jina la Papa Yohane XXIII, Papa amependa kukumbuka maneno yake aliyoandikwa katika Waraka wake usiosaahulika kuhusu amani: “Mungu aondolee mbali katika moyo wa watu kile ambacho kinaweza kuleta  hatari ya amani; na kuwabadili kuwa mashuhuda wa ukweli, wa haki  na wa upendo kidugu. Awaangazie wahusika wakuu wa watu ili karibu nao kuwepo na mwamko kwa ajili ya  haki za ustawi wa wazalendo wao kwa kuhakikisha na kulinda zawadi kubwa ya amani; awashe utashi kwa wote wa kushinda vizingiti ambavyo vinatengenisha  na kukuza ufungamano wa upendo zaidi, wa uelewa wa wengine, wa msamaha kwa wale ambao wametenda mabaya, katika muktadha wa matendo yao, wawe na  udugu wa kindugu wote wa nchi na kuchanua kwao na daima kuchanua kwa  amani inayotamaniwa" ( Pacem in terris,91).

Mkutano wa Papa na wahamiaji na wakimbizi
Mkutano wa Papa na wahamiaji na wakimbizi

Baba Mtakatifu amebainisha juu ya wale ambao walikuwa wawashe mishumaa mbele ya picha ya Bikira Maria. Ishara moja rahisi lakini yenye maana kubwa. Katika utamaduni wa kikristo. Moto mdogo ni ishara ya imani kwa Mungu. Pia ni ishara ya tumaini, ambalo kwake Maria, Mama Yetu alitoa maana ya safari hiyo na anawasaidia kwenda mbele. Mama awasaidie wasipoteze matumaini hayo. Na kwake Papa amewakabidhi kila mmoja wao, familia zao na kuwakumbuka katika sala zake. Amewaomba nao wasisahau kusali kwa ajili yake.

HOTUBA YA PAPA KWA WAHAMIAJI HUKO MALTA 3 APRILI 2022
03 April 2022, 18:41