Tafuta

2022.04.03 Papa akiwa katika ziara yake ya kitume huko Malta alikutana na Jumuiya ya Wajesuit. 2022.04.03 Papa akiwa katika ziara yake ya kitume huko Malta alikutana na Jumuiya ya Wajesuit. 

Hija ya Kitume ya Papa Francisko Malta:Padre Spadaro,shauku ya Papa ni Kanisa wazi

Mkurugenzi wa Gazeti Civiltà Cattolica amezungumzia kwa ufupi juu ya mazungumzo yaliyofanyika kati ya wanajumuiya za Shirika la Yesu(Wajesuit)ambapo kutoka kikundi kidogo cha Malta kimekuwa mwamsho wa Uinjilishaji.Papa anashuku ya kuona Kanisa linalojifungua wazo katika changamoto kubwa.

Na Angella Rwezaula - Vatican

Mazungumzo ya moyo ulio  wazi ni yale ambayo Papa Fransisko alikuwa nayo asubuhi ya Dominika tarehe 3 Aprili 2022  alipokutana na  Wajesuti wa Malta, kwa mujibu wa mapokeo yaliyojikita katika Upapa wake, yale ya kuweza kufanya mkutano wa wanashirika wenzake kila mara anapokuwa katika safari zake za  kitume na yaliyomo ndani ya mkutano huo kwa kawaida  ujulikana baadaye kupitia Gazeti la shirika la "La Civiltà Cattolica".  Lakini kwa kwa ufupi yaliyojiri, ni katika mahojiano na mkurugenzi wa gazeti hilo Padre Antonio Spadaro katika siku ya pili ya ziara ya  Papa  Francisko huko Malta, ambaye alikuwa naye katika ziara hiyo  kipapa.

Mkutano wa Papa na Wajesuit huko Malta
Mkutano wa Papa na Wajesuit huko Malta

Kwa mujibu wa Padre Spadaro amebainisha kwamba katika safari zake zote, inapowezekana, Papa Francisko hukutana na jumuiya ya Wajesuit waliopo mahali anaposafiri. Kama kawaida, wao ni wema sana,  kwa watu na  ukaribu sana wa kawaida mahali wanapokuwa.  Na katika mkutano kwa kawaidi ni wa haliya utulivu, ya mazungumzo ya wazi juu ya mada nyingi. Labda jambo zuri zaidi ni kumwona Papa, akiwa katikati ya safari, akitoa maoni yake, kuelewa kidogo halijoto ya makaribisho aliyopokelewa,  ba  mambo ambayo Papa anataka kusema kwa wanajumuiya wake. Hivyo mazungumzo hayo, kwa mujibu wa Padre Spadaro amesema kuwa yalikuwa ya  faragha na ambayo yatachapishwa katika Gazeti la Civiltà Cattolica, Papa atakapotaka na akitaka.

Kimisingi yaliyomo ni yale yanayohusu maisha yenyewe ya Jumuiya ya Yesu na kwa hiyo maana ya uinjilishaji leo hii. Papa alirudia tena juu ya furaha hii ya uinjilishaji, ambayo aliizungumzia sana katika hotuba yake huko Malta na mtazamo aliyonao mtu, na nia aliyonayo Papa ni ile ya Kanisa ambalo liko wazi kwa ajili ya changamoto kubwa. Kisiwa hicho kwa namna fulani kina changamoto kubwa ndani yake, kwa sababu ni njia panda katikati mwa Bahari ya Mediterania kwa hiyo ni msukumo wa uinjilishaji.

Mkutano wa Papa na Wajesuit huko Malta
Mkutano wa Papa na Wajesuit huko Malta

Akijibu swali kuhusu muda mfupi tu kabla ya mipango yake iliyofuata na wahamiaji  ni matunda gani ambayo wengi wanaweza kuvuna katika ziara hiyo ya  Papa? Padre Spadaro alijibu kuwa "Zaidi ni mada ya wahamiaji ambayo Papa aligusia katika mkutano wake na Wajesut na ambayo iko karibu sana na moyo wake. Maana ya kina ya ziara hiyo, kutembelea kitovu cha Mediterania, njia panda ya miingiliano, inapatikana katika ujumbe ambao Papa anautoa kwa ulimwengu kuanzia pembezoni ambayo ni kitovu cha mabadilishano ya kitamaduni na kiroho, kwa hivyo kukutana huku Malta si hapo tu lakini pia  kiukweli inahusu ulimwengu mzima", alisisitiza Padre Sapadaro..

Papa aliweka msisitizo maalum mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana alipozungumzia vita vya Ukraine ambavyo kwa mara ya tatu Papa Francis alivitaja kuwa vya kufuru, na hivyo Padre Spadaro alisema: “Hasa. Hii ni mada ambayo kwa hakika inaendesha safari hiyo, wakati wa Misa tuliona bendera nyingi za Ukraine na haiwezi kushindwa kufanya hivyo. Tayari katika mkutano na mamlaka, Papa alikuwa wazi sana, pia akionesha majukumu kuhusu maandalizi ya masharti ya kupigana vita, sio ya sasa lakini  ni vita vilivyopangwa kwa  muda, kwa njia ya silaha, hivyo ujumbe ulikuwa wenye nguvu sana.

04 April 2022, 17:36