Hija ya Kitume ya Papa Francisko Malta: sala katika groto ya Mt. Paulo
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Dominika tarehe 3 Aprili 2022, ikiwa ni siku ya pili ya Ziara ya 36 ya Kitume ya Papa Francisko kisiwani Malta na Gozo, kwa kuongozwa na kauli mbiu ya maneno ya Mtakatifu Paulo isemayo: “Wenyeji wakatufanyia fadhili zisizokuwa za kawaida.” (Mdo 28: 2), ametembelea Groto ya Mtakatifu Paulo mtume wa watu huko Rabat na mara baada ya kufika ametia saini kwenye kitabu cha Heshima. Katika kitabu hicho Papa ameandika : “Katika mahali hapa patakatifu, ambayo yanakumbusha Mtakatifu Paulo, Mtume wa Watu na Baba wa imani ya watu hawa. Ninashukuru Bwana na ninamwomba ili aweze kuwajalia daima watu wa Malta Roho ya faraja na shauku ya tangazo”.
Baadaye Baba Mtakatifu Francisko amesali sala katika Groto: “Mungu wa huruma, katika majaliwa yako ya ajabu ulitaka Mtume Paulo atangaze upendo wako kwa wakazi wa Malta, ambao hawakujua bado. Alitangaza neno lako kwao na kuponya udhaifu wao. Wakiwa wameokolewa kutoka katika ajali ya meli, Mtakatifu Paulo na wasafiri wenzake walipata hapa makaribisho kutoka kwa watu wapagani wenye moyo mzuri, ambao waliwatendea kwa ubinadamu adimu, kwa kutambua kwamba walihitaji makazi, usalama na usaidizi. Hakuna mtu aliyejua majina yao, asili au hali yao ya kijamii; walijua jambo moja tu: kwamba walihitaji msaada. Hapakuwa na wakati wa mazungumzo, kwa hukumu, uchambuzi na mahesabu: ilikuwa wakati wa kusaidia; waliacha kazi zao na ndivyo walivyofanya. Waliwasha moto mkubwa na kuwafanya wakaushe nguo zao na joto. Wakawakaribisha kwa moyo mkunjufu na pamoja na Publio. Kiongozi wa kwanza katika serikali na katika huruma walipata malazi kwa ajili yao. Baba mwema utujalie neema ya moyo mwema anayepigania upendo wa ndugu zake. Tusaidie kutambua mahitaji kutoka mbali ya wale wanaopambana katika mawimbi ya bahari, kutupwa kwenye miamba ya ufuo usiojulikana. Utujalie huruma zetu zisiishie katika maneno ya bure, lakini washa moto wa kukaribisha, ambao unafanya kusahau hali mbaya ya hewa, uwasha mioyo na kuwaunganisha: moto wa nyumba iliyojengwa juu ya mwamba, wa familia pekee ya watoto wako, dada na kaka wote. Wewe unawapenda bila ubaguzi na unataka wawe kitu kimoja pamoja na Mwanao Yesu Kristo, Bwana wetu, kwa nguvu ya moto uliotumwa kutoka mbinguni, Roho wako Mtakatifu, hiyo inachoma uadui wote, na usiku huangaza njia kuelekea ufalme wako wa upendo na amani. Amina.
Sala ya mwisho katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo na salamu kwa watu
Papa amewasalimia watu mbali mbali wenye ulemavu, wazee, watoto na familia mbali mbali, kabla ya kuacha Kanisa kuu la Mtakatifu Paulo. Hawa ni wagonjwa wa Parokia mbali mbali na baadhi ya watu ambao wanatunzwa kwenye nyumba ya "Papa Francisko" ya Mtakatifu Venera na karibu watu kama therathini wanaotafuta kuondokana na madawa ya kulevya. Watu hawa wanasaidiwa na Caritas Malta ambayo inashirikishana na mashirika 26 ya utunzaji katika Kanisa la Kisiwa hicho. Kwa kuhimisha Papa amewabariki na kusali: "Ee Mungu, huruma zako hazina kikomo na hazina ya wema wako haina kikomo. wazidishie imani watu waliowekwa wakfu Kwako ili wote wapate kufahamu kwa hekima ni upendo gani uliowaumba, ni damu gani iliyowakomboa, na ni Roho gani imewafanya upya. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina".