Hija ya Kitume ya Papa Francisko Malta:Tusinyoshee vidole bali tusikilize
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtamatifu ameanza mahubiri katika Misa na wawakilishi wa makanisa ya Kikristo na madhehebu mengine ya kidini huko Floriana kisiwani Malta kwa kuongozwa na Injili ya Dominika tarehe 3 Aprili 2022, Baba Mtakatifu amesema kuwamapema asubuhi Yesu alikwenda hekaluni kusali na watu wote waliokuwa wanakwenda kwakwe ( Yn 8,2). Na ndivyo linaanza tukio la mwanamke mzinzi. Historia hii inajiwakilisha katika hali ya tulivu, asubuhi katika mahali patakatifu katika moyo wa Yerusalemu. Wahusika wakuu ni Watu wa Mungu katika uwanja wa hekalu ya wanamtafuta Yesu, Mwalimu. Wanatafua kumsiliza, kwa sababu Yeye anaangaza na kutia joto. Mafundisho yake yanagusa maisha na kutoa uhuru, hubadilisha na kupyaisha. Ndiyo maana sababu kuu ya watu wa Mungu ambao hawaridhishwi na hekalu lililojengwa kwa mawe bali wanazungukia mtu Yesu. Katika sura hizi wanaonekana watu waamini wa kila wakati, watu watakatifu , ambao kwa upande wa Malta ni wengi, wapo waaminfu wanaotafuta Bwana, waliofungwanishwa kwa dhati na kuishi. Papa amewashukuru na kusema kwamba mbele ya watu wanaomkimbilia Yesu, hana haraka.
Baba Mtakatifu Francisko amesema kwamba Yesu alikaa na kuwafundisha wao, kama isemavyo Injili. Lakini katika shule ya Yesu, kuna nafasi tupu, maana wanakusekana wengine kama mwanamke na wale wanamuhukumu. Hawakwenda kama wengine kwa Mwalimu na sababu zao ambazo ni tofauti, waandishi na mafarisayo wanafikiri kujua tayari kila kitu na hawana haja ya mafundisho ya Yesu. Mwanamke lakini ni mtu anayehangaika, ametoka nje ya njia akaingia njia mbaya. Ukosefu huo kwa maana hiyo umetokana na sababu tofauti kama ilivyo hata matukio yao. Awali ya yote wanaomshitaki mwanamke. Katika wao inaonekana sura ya wale wanaojidai kuwa wenye haki, wachambuzi wa sheria ya Mungu, watu ambao wanafikiria wako salama na vema. Hawajali mabaya yao lakini wako makini kwa kutazama ya wengine. Na hivyo walikwenda kwa Yesu si kwa moyo uliowazi ili kumsikiliza bali kumweka katika majaribu ili wapate sababu ya kumhukumu. Hawa wana lengo la ndani la watu walioelimika na wa kidini ambao wanajua maandiko , wanakwenda katika hekalu, lakini wanaweka mbali kila kitu kwa ajili ya maslahi yao na hawapambani dhidi ya mawazo mabaya iliwaondokane nayo. Kwa kufanya hivyo wanamweka mwanamke mbele ya umma na kumhukumu kuwa ni mzinzi. Wanataka kuwa mwanake huyo aweze kupigwa mawe. Wanafanya hayo yote chini ya vazi la kuwa watu wa dini.
Baba Mtakatifu amesema watu hawa wanafafanua hata katika maisha yetu ya dini inawezekana kutoka nje, kuwa na tabia mbaya ya kunyoshea kidole. Kila nyakati na katika kila jumuiya. Daima kuna hatari ya kumtaja Yesu katika midomo lakini ni kinyume na matendo. Na inawezakana kufanya hivyo hata kwa kubeba msalaba. Je ni jinsi gani ya kuhakikisha hilo iwapo sisi ni wafuasi wa Shule ya Yesu? Kutokana na mtazamo wetu na jinsi ambavyo tunawatazama jirani zetu na jinsi tunavyo jitazama sisi wenyewe. Kwa jinsi tunavyo tazama jirani, ikiwa tunafanya kama Yesu, anavyofanya leo hii kwa mtazamo wa huruma au kwa namna ya kuhukumu ambayo hata kufikia kudharau na kushutumu kama Injili inavyooesha. Waohawakutambua kuwa wanakanyaga Ndugu. Kiukweli anayeamin analinda imani kwa kunyoshea mwingine kidole, anaweza kuwa wa dini lakini siyo wa Roho ya Injili kwa sababu anasahamu huduma ambayo ni moyo wa Mungu.
Baba Mtakatifu Francisko amesema ili kuelewa hilo ya kuwa wanafunzi wa kweli wa mwalimu ni lazima kuhakikisha mtazamo wetu. Washutumu wa mwanamke walijiamini, kwa sababu walifikiri wanaelewa. Kwa maana ya kiju juu wanajiona wakamilifu lakini inakosekana ukweli wa moyo. Hii ni picha ya waamini wa kila wakati ambao hufanya imani kuwa kitu cha kijujuu tu, mahali ambapo wanajionesha nje wanakosa umaskini wa ndani ambao ni tunu msingu wa binadamu. Baba Mtakatifu amesema, kile ambacho Yesu anataka ni ufunguzi wa kwa yule anayehitaji msaada wa wokovu na wa sio anayefikiri kafika. Itakuwa vizriu kwa maana hiyo wanapokuwa katika sala, hata katika ushiriki wa aina yoyote ya sala za kidini kuomba kwa BWANA. Moja kwa moja: “Nipo hapa na wewe lakini wewe unataka nini kwangu?. Unataka nibadilishe nini katika maisha yangu? Unataka nitazame wengine namna gani? Papa ameongeza kusema kwamba " Itakuwa vizuri kusali namna hiyo".
Baba Mtakatifu Francisko amesema walimwona mwanamke mzinzi. Hali yake ilikuwa namna hiyo lakini macho yake yalikuwa yamefunguliwa katika upeo mpya usiofikiriwa. Akiwa amefunikwa na matukano, alikuwa tayari kupokea maneno mabaya na kwa ukali wa kutengwa. Maisha ya mwanamek huyo yalibadilika shukrani kwa msamaha. Inawezakana kufikiria kwamba mara baada ya kupoata msamaha wa Yesu alijifunxa kwa mara nyingine kusamehe. Labda kwa watesi wake, ambao walikuwa wagumu na wabaya, lakini walio mfanya akutne na Yesu. Bwana Yesu anatamani kukutana na kila mfuasi, kama sisi sote, kama Kanisa ambalo tunahitaji kusamehewa na Yeye, tunageuka kuwa mashuhuda wasiochoka wa upatanisho; wa Mungu ambaye hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu ambaye daima anasamehe, anaaendelea kuamini sisi na kila mara anatoa fursa ya kuanza. Hakuna dhambi au kushindwa kwetu kwa sababu inakuwa fursa ya kuanza maisha mapya, tofauti katika isahara ya huruma .
Leo hii ni mwanamke huyo, ambaye alijua huruma katika taabu yake na ambaye anaenda ulimwenguni akiwa ameponywa kwa msamaha wa Yesu, ambaye anatushauri sisi kama Kanisa kujiweka tena katika shule ya Injili, shule ya Mungu wa matumaini ambaye daima hushangaza, amesisitiza Papa Francisko. "Tukimwiga, hatutakuwa na mwelekeo wa kukazia fikira kushutumu, dhambi, bali kuanza kwa upendo kutafuta watenda dhambi. Hatutahesabu waliopo, lakini tutaenda kutafuta wasiokuwepo. Hatutarudi kunyoosha vidole, lakini tutaanza kusikiliza. Huyo ndiyo Bwana Yesu. Anamfahamu kiukweli yule anayefanya uzoefu wa msamaha. Ni nani kama mwanamke wa Injili, anayegundua kuwa Mungu alitutembelea kwa nia ya majeraha yetu ya ndani. Ni pale tu Bwana amependa kuwapo, kwa sababu alikuja si kwa ajili ya wenye afya bali wagonjwa (Mt 9, 12). Kwa kufanya hivyo hatutanyosha kamwe kidole kwa mwingine, hatutawatupa waliodharauliwa, lakini tutawaangalia kwanza wale wanaohesabiwa kuwa wa mwisho.Hivi ndivyo Yesu anatufundisha leo kwa mfano.Tushangazwe naye.Tunaukaribisha upya wake kwa furaha".