Tafuta

2022.04.02 Hija ya Papa Francisko huko Malta 2022.04.02 Hija ya Papa Francisko huko Malta  

Hija ya Kitume ya Papa Francisko Malta:Papa ameanza safari!

Papa Francisko ameondoka na ndege kutoka Uwanja wa Ndege Kimataifa wa Fumicino, Roma baada ya saa 2.30 hivi.Safari ya kwenda Malta ni karibu kwa muda wa saa 1 na nusu hivi mahali ambapo anasubiriwa kwa shangwe kuu huko.

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi asubuhi tarehe 2 Aprili 2022 ameondoka baada ya saa 2.30 hivi kutoka uwanja wa Kimataifa wa Fiumicino Roma, kuelekea Kisiwa cha Kimediteranea, Malta katika ziara yake ya Kitume ya 36 kimataifa ambapo anatarajia kufika huko baada ya saa moja na nusu hivi. Katika  hija ya kitume nchini Malta inaongozwa na kauli mbiu “Wenyeji wakatufanyia fadhili zisizokuwa za kawaida.” Mdo 28: 2”.

Hija ya Kitume ya Papa Francisko huko Malta na Gozo
Hija ya Kitume ya Papa Francisko huko Malta na Gozo

Akifika huko atapokelewa uwanja wa ndege kwa afla za Makaribisho. Baadaye atakwenda Jumba la La Valletta na  kumtembelea Rais wa Jamhuri kwa faragha Bwana George William Vella. Baadaye atakuwa na mkutano na Waziri Mkuu Robert Abela ikifuata mkutano na viongozi wakuu wa nchi, raia, kidini na wanadiplomasia. Baba Mtakatifu atatahutibia.

Ziara ya Kitume ya 36 Kimataifa ya Baba Mtakatifu huko Malta na Gozo 2-3 Aprili

Hata hivyo kabla ya kuondoka katika Nyumba ya Mtakatifu Malta mjini Vatican, amewasalimia baadhi ya familia za wakimbizi kutoka Ukraine na kuelekea Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa  "Leonardo Da Vinci" wa  Roma Fiumicino.

Papa amekutana na baadhi ya familia kutoka Ukraine kabla ya kuanza safari kuelekea Malta
Papa amekutana na baadhi ya familia kutoka Ukraine kabla ya kuanza safari kuelekea Malta

Telegramu kwa Rais  Mattarella

Kabla ya kuacha eneo la Italia, Papa Francisko ametuma talegramu kama utamaduni wa kila ziara ya kwenda nje ya nchi kwa Rais wa Jamhuri ya Italia Bwana  Sergio Mattarella, ambapo amebainisha "furaha ya kukutana na ndugu wa imani katika Nchi angavu yenye uzuri sana katikati ya Bahari ya Mediteranea, vilevie Bandari salama kwa milenia ya wasafiri wa kufika na kuondoka". Baba Mtakatifu kwa maana hiyo amemtumia "kiongozi wa nchi na watu wote wa Italia matashi mema, utulivu na amani".

Papa akwenda kusali katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu  kukabidhi kwa mama zira yake ya kitume
Papa akwenda kusali katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu kukabidhi kwa mama zira yake ya kitume

Baba Mtakatifu kama kawaida yake  kabla ya kuanza safari yoyote ile ya kimataifa, ameikabidhi kwa Mama Maria Afya ya Warumi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu Roma.

Siku ya Dominika 3 Aprili: Misa na kukutana na wahamiaji

Katika siku ya pili ya Ziara yake ya kitume huko Malta na Gozo, Dominika tarehe 3 Aprili 2022, siku ya Papa itafunguliwa na mkutano wa faragha na wajumbe wa Shirika la Yesu yaani Wajesuit, katika Ubalozi wa Rabat majira ya saa 1.45. Wakati huo huo  Saa2.30 Baba Mtakatifu atakwenda kutembelea Groto ya Mtakatifu Paulo katika Kanisa Kuu linalobeba jina hilo. Sehemu hiyo inakumbusha manusura ya Mtume wa Watu kwenye miaka ya 60 baada ya Kristo. Baba Mtakatifu anatarajia kuwa na kipindi cha sala. Mida ya saa 4.15 hivi  Baba Mtakatifu ataadhimisha misa katika Uwanja Granai huko Floriana na baadaye kufuata sala ya Malaika wa Bwana.

Mchana Papa anatarajia kukutana na kundi la wahamiaji, mida ya saa 10.45 jioni  hivi katika kituo cha wahamiaji cha  Yohane XXIII  huko Hal Far na atatoa hotuba yake. Itakuwa ndiyo mwisho wa ziara yake ya kitume kimataifa, ambapo baadaye ataelekea uwanja wa Kimataifa wa Malta kwa afla za kuagwa. Saa 11.50 hivi ataanza safari ya kurudi Roma na anatarajia kufika mida ya saa 1.40 hivi za usiku katika uwanja wa Ndege kimataifa Fiumicino, Roma.

02 April 2022, 09:08