Hija ya Kitume ya Papa Francisko Malta:Ukarimu na ushuhuda wa Injili
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 2 Aprili 2022 majira ya saa 11 jioni amekuwa na katika Madhababu ya Taifa ya Ta’ Pinu ya Bikira Maria katika kisiwa cha Gozo, amesali ndani ya Madhabahu ya Kitaifa kwa kimya mara baada ya kufika hapo. Ni katika Ziara yake ya kitume cha 36 katika Kisiwa cha Kimediteranea, Malta. Hija hiyo inaongozwa na kauli mbiu: “Wenyeji wakatufanyia fadhili zisizokuwa za kawaida.” (Mdo 28: 2”), Maneno yanayotukumbusha ushuhuda ya Mtakatifu Paulo Mtume wa watu wakati wa ajali na kunusurika na wenzake katika bahari ya Mediteranea na kufika katika bandari ya Malta. Katika mahubiri yake Papa Francisko amesema., "Mbele ya Msalaba wa Yesu kuna Maria na Yohane. Mama aliyemzaa Mtoto wa Mungu ana uchungu kwa ajili ya kifo cha mwanae wakati giza linazungukia ulimwengu". Mwanafunzi mpendwa aliyekuwa ameacha kila kitu kumfuata sasa amesimama chini ya Mwalimu aliyesulibiwa. Utafikiri yote yamekwisha milele. Na wakati anachukua majeraha ya ubinadamu Yesu anasali: “Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeaniacha (Mt 27, 46; Mk 15,34). Papa amesema "Hii pia ni sala yetu wakati maisha yanapokumbana na mateso; ni sala hata ya kila siku ambayo inapaa kwa Mungu kutoka katika mioyo yenu Sand ina Domeniko, akiwageukia waliotoa ushuhuda wao wa maisha. "Asante kwa uvumilivu wa Mioyo yenu na kwa ajili ya ushuhuda wenu wa imani".
Baba Mtakatifu akiendelea amesema Saa ya Yesu ambayo inatajwa katika Injili ya Yohane ambayo ni Saa ya kifo juu ya msalaba, haiwakilishi hitimisho la historia, lakini kwa kukita juu ya mwanzo wa maisha mapya. Akiwa Msalabani, kiukweli tunatafakari upendo wa huruma wa Kristo ambaye anafungua wazi mikono yake na kwa kupitia kifo chake anatufungulia furaha ya maisha ya milele. Kutokana na saa ya mwisho inafungua maisha ambayo yanaanza, kutoka saa ya kifo na kuanza saa nyingine ya maisha. Ni kipindi cha Kanisa ambalo linazaliwa. Kutoka katika asili Bwana anaunganisha watu,na ambaye ataendelea kupitianjia zisizotarajiwa katika historia kwa kupeleka moyo wa faraja ya Roho, ambaye anakausha machozi ya ubinadamu. Baba Mtakatifu Francisko amesema katika Madhabahu ya Ta’ Panu, wanaweza kutafakari pamoja kuhusu mwanzo wa Saa ya Yesu. Hata katika mahali hapo kabla ya jengo zuri ambalo linaonekana leo hii kulikuwa na kikanisa kidogo sana kilichopigwa na bomu. Kikanisa kilikuwa limeondolewa na utafikiri ulikuwa ndiyo mwisho. Lakini kutokana na safu za matukio yakabadili mambo, kama vile Bwana alikuwa anataka kuzungumza na watu hao kwamba: “Hutaitwa tena Aliyeachwa, wala nchi yako haitaitwa tena, Ukiwa; bali utaitwa Hefsiba; na nchi yako Beula;kwa kuwa Bwana anakufurahia ,na nchi yako itaolewa (Is 62,4).
Baba Mtakatifu amebainisha kuwa kikanisa hicho kimegeuka kuwa Madhabahu ya Taifa, eneo la mahujaji na kisima cha maisha mapya. Papa amekumbusha hayo kwa Jeniffer aliyetoa ushuhuda kuwa watu wengi wanakwenda kwa Bikira Maria na kukabidhi mateso yao na furaha zao na wote wanahisi kukaribishwa. Papa amekumbushaalivyo kwenda hapo kama mhujaji mtangulizi wake Mtakatifu Paulo II ambaye tarehe 2 Aprili, ilikuwa ni siku ya kumbu kumbu ya kifo chake. Sehemu moja ambayo utafikiri ilikuwa imepotea na sasa inatoa imani na matumaini katika Watu wa Mungu. Katika mwanga huo Papa ameomba kufuata mwaliko wa saa hiyo ya Yesu, saa ile ya wokovu. Papa amesema ili kuweza kupyaisha imani na utume wa jumuiya wote wanaalikwa kurudi katika mwanzo wa Kanisa ambalo linaonesha Msalaba akiwapo Maria na Yohane. Lakini je ina maana agani kurudi mwanzoni? Nini maana ya kurudi katika asili. Awali ya yote Papa amesema ni kugundua yaliyo msingi wa imani. Kurudi katika Kanisa la asili, haina maana ya kutazama nyuma na mtindo wa Kanisa la Jumuiya ya kwanza ya Kikristo. Haiwezekani kuruka Historia, kama vile Bwana hakuweza kuzungumza na kutenda mambo makuu hata katika maisha ya Kanisa kwa karne zilizofuata. Hii haina maana pia ya wenye mawazo ya kufikiria jumuiya ambayo hakuna matatizo; kinyume chake, Papa amesema inasomeka kuwa Mitume wa kwanza walijadili hata kufikia kugombana kati yao na daima hawakuweza kuelewa mafundisho ya Bwana. Kwa maana hiyo kurudi katika asili maana yake ni kurudisha roho ya Jumuiya ya kwanza ya Kikristo yaani kurudi katika moyo na kugundua kiini cha imani, ambacho ni uhusiano na Yesu na tangazo la Injili yake katika ulimwengu mzima. Hiyo ndiyo msingi.
Baba Mtakatifu Francisko amesema, baada ya saa ya kifo cha Yesu, mitume wa kwanza kama Maria Magdalena na Yohane kwakuwa waliona kaburi wazi bila kupoteza wakati, kwa moyo wa shangwe, walikimbia kwenda kutangaza Habari Njema ya Ufufuko. Machozi ya uchungu katika msalaba yaligeuka kuwa furaha ya tangazo. Papa amefikiria hata mitume wengine ambapo imeandikwa: “Na kila siku, ndani ya hekalu na nyumbani mwao, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema za Yesu kwamba ni Kristo.”(Mdo 5, 42.) Wasiwasi mkuu wa wafuasi wa Yesu haukuwa ni kutafuta sifa ya jumuiya na huduma yake, wingi wa jamii na ibada yao. Wasiwasi wao ulikuwa ni ule wa kutangaza na kushuhudia Injili ya Kristo. Papa Francisko amesema Kanisa la Malta linajivunia historia msingi ambayo inaweza kuchotwa utajiri mwingi wa kiroho na kichungaji. Pamoja na hayo wakumbuke kuwa maisha ya Kanisa daima hawapo peke yao na historia ya wakati uliopita inapaswa kukumbukwa lakini kwa matazamio ya wakati ujao wa kujenga, na upole wa mipango ya Mungu. Haiwezekani kutosheka na imani inayotumika kama utamaduni uliorithishwa, sherehe, fursa nzuri za watu, na vipindi muhimu vya nguvu, kwa sababu kuna haja ya imani ambayo inakita mzizi na kupyaisha na kukutana binafsi na Kristo katika kusikiliza kila siku Neno lake katika ushiriki hai wa maisha ya Kanisa, na kutoka katika roho za watu.
Baba Mtakatifu Francisko amebainisha juu ya kushuka kwa imani ya waamini hasa baada ya janga la uviko, sintofahamu za vijana, kulinda na uwepo wa Mungu kwamba sio masuala ya kudharau, kwa kufikiria kwamba roho ya kidini bado ipo. Wakati mwingine mpasuko huo unaweza kuwa wa kidini lakini nyuma yake kuna anguko la imani iliyochakaa. Umaridadi wa kutazama nguo nyingine za kidini daima haziendani na imani hai inayouishwa na mwendelezo wa unjilishaji. Inahitaji kikesha kwa sababu mazoezi ya kidini yasipunguzwe na marudio ya wakati uliopita badala yake kueleza imani hai, iliyo wazi na ambayo inaeneza furaha ya Injili. Baba Mtakatifu Francisko amekumbusha walivyoanza Mchakato wa Sinodi ambao ni kujipyaisha anawashukuru kwa safari hiyo. Sasa ni saa ambayo ya kurudi mwanzoni, chini ya msalaba kwa kutazama jumuiya za kwanza za Kikristo. Ili kuweza kuwa Kanisa ambalo kiini cha moyo wa urafiki na Yesu ina maana ya kutangaza Iniili yake na sio kuacha nafasi na vishawishi.
Baba Mtakatifu amebainisha kwamba kuwa Kanisa moja ambalo linaweka kiini cha ushuhuda na sio tabia za za kidini, kuwa Kanisa linalotamani kwenda kukutana na wote likiwa na taa zinawaka za Injili na sio zilizofungwa. Papa ameomba wasiogope kuchukua njia hiyo ambayo tayari walianza michakato ya njia mpya ambayo labda ni hatari ya unjilishaji na tangazo linalogusa maisha. Akitazama asili ya Maria na Yohane wakiwa chini ya Msalaba Papa amesema katika chemi chemi ya Kanisa wapo wao pamoja na ishara ya kujikabidhi. Bwana kwa hakika alimkabidhi kila mmoja kumtunza mwingine. Yohane kutunza Maria na Maria kutunza Yohane na ndiyo tangu wakati huo, akamchukua mama huyo (Yh 19,27). Kurudi mwanzoni maana yake pia ni kuendeleza sanaa ya kukaribisha. Kati ya maneno ya mwisho ya Yesu, Juu ya msalaba ni yale aliyomweleza Mama yakee na Yohane ambayo yanashauri kufanya makaribisho kama mtindo mkuu wa utume. Haikuwa ishara rahisi tu ambayo Yesu alimkabidhi Mama yake kwa Yohane kwa sababu hasibaki peke yake baada ya kifo, lakini kwa kuelekeza kwa dhati jinsi ya kuishi amri kuu, ile ya upendo. Ibada ya Mungu inapitia kwa ukaribu wa ndugu.
Jinsi gani ilivyo muhimu katika Kanisa upendo kati ya ndugu, na ukarimu wa jirani. Bwana anakumbusha katika saa ile msalabani na katika ukaribishwaji wa pamoja kati ya Maria na Yohane, wakishauri jumuiya ya kikristo ya kila wakati na sio kumazlia kipumbele hiki. “Tazama mwanao, na tazama mama yako(Yh 26.27). Hii ni kama kusema mmekombolewa kwa damu sawa, ninyi ni familia moja, hivyo basi mkaribishane, mpendane, mfariji wengine. Bila shuku, migawanyiko na masengenyo. Kwa sababu Mungu yupo palipo na upendo. Baba Mtakatifu Francisko kwa maana hiyo ameshauri wakaribishane, na wasiogope lakini kwa jina la Kristo na ndiyo changamoto ya kudumu. Hiyo ipo hasa katika mahusiano ya kikanisa, kwa sababu utume wake unaanza kuzaa matunda ikiwa wanafanya kazi katika urafiki na katika umoja kidugu. Ni jumuiya mbili za Malta na Gozo, Papa ameongeza kusema kuwa hajui iliyo muhimu na wala ya kwanza… ambazo kama ilivyokuwa Maria na Yohane. Maneno ya Yesu juu ya msalaba kwa njia hiyo yawe ndiyo nyota kuu ili kukaribishana, kuunda familia, kufanya kazi kwa umoja na kwa pamoja daima. Daima wakende mbele kwa unjilishahi kwa sababu furaha ya kanisa ni Uinjilishaji.
Baba Mtakatifu anasema kuwa lakini ukarimu pia ndiyo ramani ya kurudisha mwanga wa kuhakikisha kile ambacho Kanisa linashauiriwa na Roho ya Injili. Maria na Yohane walikaribishana si katika nyumba ya karamu kuu, lakini katika msalaba katika eneo ambalo lilikuwa limemhukumu na kumsulibisha kama jambazi. Hata kwa upendo wao kama wakrisro awawezi kukaribishwa kati yao katika kivuli ha mambo mazuri ya Makanisa yao wakati nje kaka na dada zao wanateseka na wamesulibiwa na uchungu, majanga, umaskini na vurugu. Papa amebainisha jinsi ambavyo kisiwa chao kipo katika sehemu ili katika Mediteranea kwenye ncha ya kivutio na bandari salama kwa watu wengi ambao wameyumbishwa na dhoruba ya maisha kwa sababu tofauti, wanapofika katika maneo yao. Katika sura zao za maskini ni Kristo mwenyewe anayewakilisha ndani yao. Na ndiyo ulikuwa uzoefu wa Mtume Paulo ambaye mara baada ya kunusurika aliweza kupata makaribisha mazuri kutoka kwa mababu zao. Katika kitabu cha Matendo ya mitume, kinathibitisha kuwa: “Wenyeji wakatufanyia fadhili zisizokuwa za kawaida. Kwa maana waliwasha moto, wakatukaribisha sote, kwa sababu ya mvua iliyonyesha na kwa sababu ya baridi”
Baba Mtakatifu Francisko amesema kwamba Injili inatoa mwaliko wa kuishi wa ukaribu, kuwa wazi wa ubinadamu, kuwasha moto wa huruma inapofiria maisha ya wale ambao wanateska. Na hiyo ni katika muktadha wa uzoefu wa janga na jambo muhimu kwa sababu Paulo alitangaza na kueneza Injili na baadaye watangazaji wengi, wahubiri, mapadre na wamisionari walifuata nyazo zake. Baba Mtakatifu Francisko ametoa shukrani maalum kwao yaani idadi kubwa ya wamisionari wa Malta ambao waliendeleza Furaha ya Injili ulimwenguni, mapadre wengi, watawa wa kike na kiume na waamini wote. Kama alivyo sema Askofu Teuma kuwa wao ni kisiwa kidogo lakini cha moyo mkuu. Wao ni tunu katika Kanisa na kwa ajili ya Kanisa. “Ili kulinda lazima kurudia katika mambo muhimu ya Kikristo ambayo ni upendo kwa Mungu, Injili ya furaha yetu, ambaye anatupafanya kutoka nje na kukimbia kwenda kwenye njia za ulimwengu, na kwa namna hiyo ya kwenda katika njia za ulimwengu kwa sababu Kanisa ni kuinjilisha na kukaribisha jirani ambaye ni ushuhuda rahisi sana wa uzuri katika ulimwengu. Bwana awasindikize katika njia hiyo, Bikira Maria awaongoze. Yeye aliyeomba kusali Salamu Maria Tatu ili kutukumbusha moyo wake wa kimama, awashe ndani ya watoto wake moto wa utume na shauku ya kuanza kutunza wengine Mama awalenda na kuwasindikiza katika Uinjilishaji, amehitimisha Papa.