Tafuta

2022.04.06 Papa Francisko anaonesha Bendera ya Ukraine iliyofika kutoka Bucha mji ambao umeoneshwa maiti zimetapaa kwenye mitaa.Inasikitisha 2022.04.06 Papa Francisko anaonesha Bendera ya Ukraine iliyofika kutoka Bucha mji ambao umeoneshwa maiti zimetapaa kwenye mitaa.Inasikitisha 

Katekesi ya Papa:Kilio cha mauaji huko Bucha,Ukraine kinapaa mbinguni

Mara baada ya katekesi Papa ameonesha kusikitishwa na ukatili wa mauji huko Bucha,mji wa Ukraine,kilomita chache kutoka Kiev,ambako picha na habari juu ya maiti za raia mitaani zimesambazwa.Papa amesisitiza wito wa kuzuia kelele za silaha.Baadaye ameonesha bendera ambayo imewasili kutoka Bucha na kuwakaribisha watoto waliofika kutoka Ukraine wapande jukwaa la Ukumbi wa Paulo VI.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko amesema kwa nguvu zote akiwa katika Ukumbi wa Paul VI, akiwa katika salamu kwa watu mbali mbali waliofika katika ukumbi huo kwamba “Mauaji ambayo mbele yake ni kilio kinapaa mbinguni: Acha vita hivi, nyamazisha silaha, acha kupanda kifo na uharibifu”. Mbele ya macho yake ana picha za maiti nyingi za raia zilizotawanyika barabarani, huku mikono yao ikiwa imefungwa nyuma ya migongo yao, huko Bucha, mji wa Ukraine ulio kilomita chache kutoka Kiev, ambao picha zao zilitolewa na mamlaka za serikali pamoja na ripoti hiyo na makaburi ya halaiki. Kwa hakika miundo ya kutisha ambayo imeukasirisha ulimwengu mzima na ambayo wengi wanaombwa kuanza uchunguzi wa uhalifu wa kivita kwa haraka. “Hatujufunzi kwa sababu tumependelea vita na roho ya Kaini. Habari za hivi karibunu juu ya vita vya Ukraine, badala ya kuleta ahueni na matumaini, ni kushuhudia ukatili mpya, kama vile mauaji ya Bucha”, amesema Papa. Kwa kuongeza “ukatili wa kutisha unaoongezeka, unaofanywa pia dhidi ya raia, wanawake wasio na silaha na watoto. Wao ni waathirika ambao damu yao isiyo na hatia inalia Mbinguni na kusihi: “Komesha vita hivi! Nyamazisha silaha! Acha kupanda kifo na uharibifu!”

Papa Francisko ametoa wito tena kunyamazisha vita:amewalimia watoto kutoka Ukraine
Papa Francisko ametoa wito tena kunyamazisha vita:amewalimia watoto kutoka Ukraine

Papa amewaomba waamini wote kuomba kwa ajili ya hili na, akiwa ameinamisha kichwa chake, kwa muda mfupi kwa ukimya amesali. Baadaye amesimama na kuonesha bendera yenye vivuli viwili vya kijani, ikiwa na msalaba uliochorwa juu yake na kuandikwa kwa Kiukreni kuizunguka. Papa amesema:  “Jana tu kutoka Bucha waliniletea bendera hii. Bendera hii inatoka katika vita, kutoka kwa jiji lililopigwa, la Bucha”. Hata hiyo kwenye jukwaa baadhi ya watoto wa Kiukreni waliungana naye, wakifuatana na wazazi wao. Mdogo zaidi yuko mikononi mwa mama yake, mkubwa zaidi amebeba mchoro wenye mikono nyeupe juu ya rangi za bendera ya Ukraine na moyo karibu na bendera ya Italia iliyowakaribisha.

Papa Francisko akionesha Bendera ya Ukraine kutoka
Papa Francisko akionesha Bendera ya Ukraine kutoka

Papa Francisko kwa maana hiyo amesema: “Tuwasalimie na tusali pamoja nao”… “Watoto hawa walilazimika kukimbia na kufika katika nchi ya kigeni: hii ni mojawapo ya matunda ya vita. Wacha tusiwasahau, na tusiwasahau watu wa Kiukreni”. Papa Francisko baadaye  amekunja bendera, mara baada ya kuibusu na kuibariki. Baadaye alichukua mayai ya Pasaka ya Choklate na kuwapatia watoto. Mabembelezo, mikono juu ya kichwa, kwenye shavu la mdogo: ishara za huruma kwa wale ambao bado wanapata mshtuko wa sauti ya mabomu na kutoroka kutoka kwa nyumba zao.

Watoto wa Ukraine waliopokelewa katika jukwaa la ukumbi wa Paulo VI
Watoto wa Ukraine waliopokelewa katika jukwaa la ukumbi wa Paulo VI
Watoto wa Ukraine waliopokelewa katika jukwaa la ukumbi wa Paulo VI
Watoto wa Ukraine waliopokelewa katika jukwaa la ukumbi wa Paulo VI

Tayari katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ndege ya kurudi kutoka Malta, Papa Francisko alikuwa ametoa maoni yake juu ya mauaji ya Bucha, habari ambayo mwandishi wa habari alikuwa amemjulisha. “Vita siku zote ni ukatili, jambo lisilo la kibinadamu, ambalo linakwenda kinyume na roho ya mwanadamu, sisemi Mkristo, mwanadamu, alisema Papa. Ni roho ya Kaini, roho ya 'Kaini.

Watoto wa Ukraine waliopokelewa katika jukwaa la ukumbi wa Paulo VI
Watoto wa Ukraine waliopokelewa katika jukwaa la ukumbi wa Paulo VI
Watoto wa Ukraine waliopokelewa katika jukwaa la ukumbi wa Paulo VI
Watoto wa Ukraine waliopokelewa katika jukwaa la ukumbi wa Paulo VI

Shukrani kwa Wapoland

Huku mtazamo wake ukiwa kwa upande wa Ukraine. Papa Francisko hata hivyo   aliwashukuru waumini wa Poland waliokuwepo katika Ukumbi wa Paulo VI na wale waliounganishwa kupitia vyombo vya habari kwa moyo wa ukaribishaji uliooneshwa kwa wakimbizi wa Ukraine. Karibu milioni tatu, kulingana na makadirio ya hivi karibuni. “Mmeonesha ukarimu wa ajabu na wa kupigiwa mfano kwa ndugu zetu wa Ukraine, ambao mmewafungulia mioyo na milango ya nyumba zenu” amesema Papa. “Asante, asante sana kwa kile ambacho umewafanyia Waukreni!” anaongeza. Hatimaye baraka: “Bwana aibariki nchi yenu kwa mshikamano wenu huu na awaoneshe Uso wake”.

Walikuwapo watu wa Ukraine pia katika ukumbi wa Paulo VI katika katekesi ya Papa
Walikuwapo watu wa Ukraine pia katika ukumbi wa Paulo VI katika katekesi ya Papa
WITO WA PAPA KWA AJILI YA KUACHA VITA NCHINI UKRAINE
06 April 2022, 16:24