Tafuta

Katekesi ya Papa kuhusu ziara ya kitume nchini Malta

Katika katekesi ya Papa,amezungumzia juu ya 'ukarimu adimu' wa watu wa Malta lakini pia upepo wa kidunia wa utandawazi.Amerudia kutazama vita Ukraine kuwa mantiki kuu ni ile ya mikakati ya serikali zenye nguvu zaidi kuthibitisha maslahi yao wenyewe.Ameshauri kuiga mfano wa nchi ya Malta inayowakilisha haki na nguvu ya mataifa madogo yanapaswa kuendeleza mantiki ya heshima na uhuru,kinyume na ukoloni wa wenye nguvu.

Na Angella Rwezaula- Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika katekesi yake Jumatano tarehe 6 Aprili 2022, kwa waamini na mahujaji katika ukumbi wa Paulo VI ametoa mhatasari wa ziara yake kisiwani Malta ambayo amehitimisha hivi karibuni,ambapo  akiwa huko  aliweza  kuhutubia kwa  viongozi wakuu wa  serikali, kirai na  wanadiplomasia  huko La Valletta; tafakari Mkutano wa sala katika Madhabahu ya Kitaifa  ya Bikira Maria ya Ta’ Pinu (Gozo); sala katika Groto ya Mtakatifu Paulo na baadaye katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo huko Rabat; Papa Francisko vile vile aliongoza misa na sala ya Malaika wa Bwana huko Floariana, Dominika tarehe 3 Aprili 2022 kwa ushiriki na wawakilishi wa Makanisa ya Kikristo na dini nyingine na sala kwa ulimwengu wote wakati wa mkutano na wahamiaji katika Kituo cha Yohana XXIII, kiitachwa Peace Lab yaani mabara ya amani, na ndiyo ilikuwa mkutano wa mwisho kabla ya kurudi Roma, Dominika  jioni. Papa Francisko kwa maana hiyo akianza katekesi yake amesema: “Jumamosi na Dominika iliyopita nilikwenda Malta: safari ya kitume ambaye ilikuwa imeandaliwa kwa muda: na iliharishwa miaka miwili iliyopita kutokana na uviko, kwa mambo hayo. Sio wengi wanatambua kuwa Malta pamoja na kuwa kisiwa katikati ya Mediterane, ilipokea mapema sana Injili. Je ni kwa nini? Kwa sababu Mtume Paulo alipata ajali karibu na fukwe kwa miujiza akaokolewa na wenzake aliokuwa nao kwenye meli, zaidi ya watu 260. Kitabu cha Matendo ya Mitume kinasimulia kuwa Watu wa Malta waliwapokea wote na kusema neno hili “kwa ubinadamu adimu (Mdo 28,2). Hili ni jambo muhimu sana, msimsahau “kwa ubinadamu adimu”.

KATEKESI YA PAPA KUHUSU ZIARA YAKE YA KITUME NCHINI MALTA
KATEKESI YA PAPA KUHUSU ZIARA YAKE YA KITUME NCHINI MALTA

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea kuelezea, juu ya ziara yake ya kitume aliyofanya kwa siku mbili 2 na 3 Aprili 2022 katika kisiwa cha Malta na Gozo amesema alichugua kwa hakika maneno hayo ya “ na ubinadamu adimu” kama kauli mbiu ya safari yake, ili kuelezea safari ya kufuata na si tu kwa ajili ya kukabiliana matukio ya uhamiaji, lakini zaidi kwa ujumla kwa sababu, ulimwengu uweze kuwa wa kidugu, unaoishi zaidi na kuweza kuokolewa na ajali ambazo zinatishia wote na ambazo Papa amesema  kama tulivyo jifunza sisi sote kuwa ndani ya mtumbwi sawa. Malta kwa upeo huo ni penye ufunguo. Awali ya yote ni mahali kijiografia, katika nafasi yake katikati ya Bahari ambayo ipo kati ya Ulaya na Afrika, lakini inalowesha hata bara la Asia. Kwa maana hiyo Malta ni kama vile “waridi la upepo” mahali ambapo wanakatisha watu na tamaduni; ni sehemu muafaka kwa mtazamo wa nyuzi 360 za eneo la mediteranea. Baba Mtakatifu Francisko amesema kwamba leo hii wanazungumzia juu ya siasa za kijigrafia lakini kwa bahati mbaya mantiki kuu ni ile ya mikakati ya serikali  zenye nguvu zaidi kuthibitisha maslahi yao binafsi kwa kutaka kupanua maeneo yenye wingi wa uchumi, au wingi wa itikadi, au wingi wa wanajeshi.

KATEKESI YA PAPA KUHUSU ZIARA YAKE YA KITUME NCHINI MALTA
KATEKESI YA PAPA KUHUSU ZIARA YAKE YA KITUME NCHINI MALTA

 

Papa ameongeza kusema: “tuko tunatazama hayo katika vita.” Malta inawakilisha picha hiyo, haki na nguvu za Mataifa madogo lakini tajiri ya historia na ustaarabu, ambao unapaswa kupeleka mbele mantiki nyingine ile ya heshima ya uhuru; hata ya mantiki ya uhuru wa kuishi pamoja na tofauti, kinyume na ukoloni wa wenye nguvu zaidi. Kwa njia hiyo ameongeza kwamba: “tupo tunatazama sasa. Na sio kwa upande mwingine: hata sehemu. Baada ya vita ya Pili ya dunia walijaribu kuweka chini historia ya amani, lakini kwa bahati mbaya hatujajifunza, iliendelea mbele historia ya kizamani ya wenye nguvu na washindani. Na katika vita vya sasa vya Ukraine, tunashuhudia Mashirika ya Umoja wa Mataifa kutokuwa na uwezo”. Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa katika sehemu Malta ni kama ufunguo kwa kile kinachotazama matukio ya uhamiaji. Katika kituo cha Wahamiaji cha Yohane XXIII alikutana na idadi kubwa ya wahamiaji, ambao wamefika katika Kisiwa hicho mara baada ya safari ngumu. Papa meomba “wasichoke kusikiliza shuhuda zao, kwa sababu ndiyo tu inawezekana kundoka katika maono potofu ambayo mara nyingi yanazunguka katika vyombo vya habari na kuweza kujua sura, historia, majeraha, ndoto na matumaini ya wahamiaji hawa. Kila mhujaji ni wa kipekee sio idadi, ni mtu, ni wa kipekee kama kila mmoja wao. Kila mhamiaji ni mtu mwenye hadhi yake, asili yake na utamaduni wake. Kila mmoja wao ni mchukuzi wa utajiri mkubwa sana usio na kikomo cha matatizo yatokanayo nayo” na hivyo amesisitiza kuwa wasisahahu kwamba Ulaya imetengenezwa na wahamiaji.

KATEKESI YA PAPA KUHUSU ZIARA YAKE YA KITUME NCHINI MALTA
KATEKESI YA PAPA KUHUSU ZIARA YAKE YA KITUME NCHINI MALTA

Kwa hakika makaribisho yanahitaji utaratibu, na kweli hiyo lazima iwe na usimamizi na kabla zadi inahitaji kupanga kwa pamoja kwa ngazi ya kimataifa. Kwa sababu matukio ya uhamiaji hayawezi kupunguzwa kwa kile cha dharura, ni ishara ya nyakati zetu. Na ndiyo inatakiwa kutafsiriwa hivyo. Inawezekana kugeuka ishara ya mgogoro, lakini pamoja na hayo ni ishara ya amani. Inategemea na sisi jinsi gani tunavyoichukulia. Aliyeanzisha kituo huko Malta cha Yohane wa XXIII, alifanya chaguo la kikristo kwa maana hiyo alikiita “Peace Lab”: yaani maabara ya amani”. Papa Francisko ameongeza kusema “Lakini mimi ninapendelea kusema kuwa Malta kwa ujumla wake ni Maabara ya amani! Taifa zima kwa tabia yake, kwa hakika ni mahabara ya amani”. Na inawezekana kutumiza utume wake huo ikiwa katika mizizi yake, inachota kiini cha udugu, cha uhuruma na cha mshikamano. Watu wa Malta walipokea thamani hizi pamoja na Injili na shukrani kwa Injili wataweze kuzitunza kwa uhai.

KATEKESI YA PAPA KUHUSU ZIARA YAKE YA KITUME NCHINI MALTA
KATEKESI YA PAPA KUHUSU ZIARA YAKE YA KITUME NCHINI MALTA

Papa Francisko akiendelea na tafakari hiyo amesema kama Askofu wa Roma, alikwenda huko kuwathibitisha watu katika imani na katika umoja. Kwa maana hiyo ndiyo mantiki ya tatu. Malta ni ufunguo hata kwa mtazamo wa uinjilishaji. Kutoka Malta na Gozo, ni majimbo mawili ya Nchi ambapo wameweza kutoka mapadre wengi na watawa lakini hata waamini walei ambao walipeleka ulimwengu wote ushuhuda wa kikristo. Hii ni kama vile safari ya Mtakatifu Paulo iliweza kuacha utume katika Kinasaba cha Wa Malta. Kwa maana hiyo ziara ya Papa ilikuwa awali ya yote tendo la utambuzi na shukurani kwa Mungu na watu watakatifu waamini ambao ni wa Malta na Gozo. Pamoja na hayo yote, hata Malta pia upepo wa kidunia unapuliza,  mabadiliko ya utamaduni wa  utandawazi unaoegemea juu ya utumiaji hovyo,  ubepari mamboleo unaovuma huko pia uwiano.

KATEKESI YA PAPA KUHUSU ZIARA YAKE YA KITUME NCHINI MALTA
KATEKESI YA PAPA KUHUSU ZIARA YAKE YA KITUME NCHINI MALTA

Kwa njia hiyo hata Malta ni kipindi cha Unjilishaji mpya. Ziara yake kama ilivyo kuwa hata kwa watanguliza wake, aliweza kwenda katika Groto ya Mtakatifu Paulo, na ambaye ilikuwa kama kuchota katika kisima, kwa sababu Injili iweze kububujika kutoka Malta kwa uhai  wake wa asili na kutoa ari ya urithi wake mkubwa wa kidini kwa watu. Hiyo ina alama yake kutoka katika Madhabahu ya kitaifa ya Maria ya Ta’ Pinu, Katika kisiwa cha Gozo mahalia ambapo waliadhimisha mkutano wa sala ya kina. papa aliweza kuwasikia watu mapigo yao ya moyo ambao wana imani kubwa katika Mama yao Mtakatifu. Baba Mtakatifu Francisko ameongeza: “Maria anatupeleka katika yaliyo muhimu, kwa Kristo Msulibiwa na mfufuka na hiyo kwa ajili yetu, kwa upendo wake wa huruma. Maria anatusaidia kuwasha moto wa imani kwa kuchota kutoka katika moto wa Roho Mtakatifu, ambaye anauuisha kizazi hadi kizazi furaha ya kutangaza Injili kwa sababu furaha ya Kanisa ni kuinjilisha! Papa amesisitiza wasisahahu sentensi ya Mtakatifu Paulo anayesema: “wito wa Kanisa ni kuinjilisha; furaha ya Kanisa ni kuinjilisha. Wasisahau kamwe hilo kwa sababu ndiyo maana iliyo nzuri kabisa ya Kanisa”.

KATEKESI YA PAPA KUHUSU ZIARA YAKE YA KITUME NCHINI MALTA
KATEKESI YA PAPA KUHUSU ZIARA YAKE YA KITUME NCHINI MALTA

Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu ametumia furaha hiyo kupyaisha tena shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Malta kwa heshima na kama kaka. Amewashukuru Yeye na familia yake: Waziri Mkuu na Viongozi wa serikali na raia ambao walimkarisha shangwe na kwa ukarimu; kama ilivyo pia maaskofu na wajumbe wa jumuiya za kikanisa, watu wa kujitolea na wale wote ambao walimsindikiza ziara hiyo kwa sala. Papa pia hakuweza kuacha kutotaja Kituo cha makaribisho cha Wahamiaji cha Yohane XXIII, kwani hapo, yupo Ndugu mdogo Mfransiskani Padre Dionisio Mintoff mwenye umri wa miaka 91 anaendelea kufanya kazi na wahudumu wa jimbo. Ni mfano wa ari ya kitume na upendo kwa wahamiaji, ambao leo hii unahitajika sana. Katika ziara hiyo Papa Francisko amesema, wamepanda mbegu lakini ni Bwana anayefanya kukua. Kwa wema wake usio na kikomno awape matunda mengi ya amani na kila wema watu wapendwa wa Malta. Amewashukuru sana watu wa Malta kwa ukarimu huo wa kibinadamu, namna hiyo kikristo.

KATEKESI YA PAPA KUHUSU ZIARA YA MALTA
06 April 2022, 16:03