Papa Francisko kwa vijana:muwe na ujasiri kama wa mtume Petro

Baba Mtakatifu Francisko, jioni Jumatatu ya Pasaka amekutana na vijana kutoka pande zote za Italia waliosindikizwa na maaskofu,mapadre,watawa,makatekista na wahudumu wa kichungaji,kuishi uzoefu wa kukutana na kusali mara baada ya miaka miwili ya janga la uviko.Wameongozwa na kauli mbiu "Nifuate",ambapo Papa ameshauri kuendeleza shauku na kumwiga Petro.Na wawe na furaha na amani.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameanza hotuba yake kwa makumi elfu ya vijana waliunganika katika uwanja wa Mtakatifu Petro  Vatican, kutoka Italia nzima ambao wamesindikizwa na maaksofu, mapadre, watawa na  wahudumu mbali mbali wa kichungaji katika maparokia, jioni ya Jumatatu ya Pasaka tarehe 18 Aprili 2022. Akianza tafakari yake mara baada ya hotuba ya Kardinali Guartiero Bassetti, Rais wa Baraza la Maaskofu Italia, (CEI) sala, nyimbo, Injili, na ushuhuda wa vijana kuhusu maisha yao na ndoto zao,  Baba Mtakatifu amesema: “Ninawashukuru jioni hii kuwa hapa katika uwanja huu ambao ulikuwa ukiwasubiri kwa muda mrefu ili kuujaza kwa uwepo wenu, kwa nyuso zenu na shauku zenu. Miaka miwili iliyopita mnamo tarehe 27 Machi nilikuwa hapa peke yangu ili kuwakilisha kwa Bwana maombi kwa ajili ya ulimwengu ambao ulikuwa umepata pigo la janga. Labda usiku ule mlikuwa hata ninyi katika nyumba zenu mbele ya televisheni mkisali pamoja na familia zenu. Leo mko hapa pamoja mmekuja kutoka pande  zote za Italia, katika mkumbatia huu wa uwanja na katika furaha ya Pasaka ambayo tumemaliza kuadhimisha.

Mkutano wa vijana na Papa Francisko Jijini Vatican 18.04.2022

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea amesema, “Yesu  ameshinda giza la kifo. Kwa bahati mbaya bado kuna shaka zito ambazo zinaweka giza la wakati wetu. Zaidi ya Janga, Ulaya iko inaishi vita vya kutisha, wakati vinaendelea na katika kanda nyingi za Nchi visivyo na haki na vurugu ambazo zinaharibu mtu na sayari. Mara nyingi wanaolipa gharama kubwa zaidi ni vijana kama ninyi, si katika maisha yenu ambayo ni ya wasiwasi na kutokuwa na uhakika lakini hata ndoto za wakati wenu ujao zimekanyagwa. Ndugu wengi na dada wengi wanasubiri bado mwanga wa Pasaka”. Baba Mtakatifu Francisko amesema simulizi ya Injili ambayo imesikika inaanzia katika giza la usiku. Petro na wengine wanachukua mtumbwi na wanakwenda kuvua samaki lakini usiku ule hawakuweza kupata chochote kile. Ni jinsi gani ya kukatisha tamaa! Amesema Papa. Tunaweka nguvu nyingi ili kutumiza ndoto zetu, tunapowekeza kama mitume bila  kupata lolote. Lakini ilitokea jambo la kushangaza, wakati ilikuwa inaanza siku mpya alifika katika fukwe mtu, ambaye alikuwa ni Yesu na  alikuwa akiwasubiri na kuwambia  watupe mahali pengine penye samaki. Na hapo ikatokea muujiza wa samaki wengi na nyavu zikavunjika. Jinsi gani tunaweza kufakari vipindi hivyo vya maisha, Papa amesisitiza.

Mkutano wa papa na vijana jijini Vatican 18.04.2022
Mkutano wa papa na vijana jijini Vatican 18.04.2022

Hayo yanatuweka katika majaribu magumu,  na kutufanya kugusa kwa mkono udhaifu wetu na kutufanya tusikie kuwa watupu wasio na mlinzi na upweke. Papa ameuliza kwamba ni mara ngapi vijana hao wamehisi kuwa peke yao na kuwa mbali na marafiki. Ni mara ngapi walihisi hofu. Hakuna haja ya kuwa na aibu ya kusema ninaogopa, kwani giza kwa kawaida linafanya kuwa na hofu. “Na wote tuna hofu za giza.  Hata hivyo hofu lazima isemwe, hofu lazima ioneshwe ili kuzifukuza”. “Kumbuka hilo: hofu lazima zielezwe. Kwa nani? Kwa baba, mama, rafiki, mtu anayeweza kukusaidia. Ni lazima ziangaziwe. Na hofu, zilizo gizani, zinapoingia kwenye nuru, ukweli hupasuka. Msikate tamaa: ikiwa mnaogopa, wekeni kwenye nuru na itawafanyia mema!”, Papa amewashauri.  "Giza linatuweka kwenye mgogoro kweli; japokuwa katika shida ni jinsi gani mimi ninavyosimamia shida hiyo: ikiwa ninajiona peke yangu, kwa moyo wangu na sizungumzi na mtu yeyote ...na kumbe  hapana, migogoro lazima izungumzwe, na hivyo zungumza na rafiki anayeweza kukusaidia, baba, mama, babu, bibi, mtu anayeweza kusaidia. Kwa kuongezea amesema “ Sijui, lakini… migogoro lazima iangaziwa ili kushinda”.

Mkutano wa papa na vijana jijini Vatican 18.04.2022
Mkutano wa papa na vijana jijini Vatican 18.04.2022

Baba Mtakatifu Francisko amewambia vijana hao wa kike na kiume kwamba, hawana uzoefu kama wa watu wazima, lakini wana kitu ambacho watu wazima wamepoteza wakati mwingine. Kwa mfano: kwa kadiri ya mika inavyozidi kwenda, watu wazima wanahitaji miwani kwa sababu wanapoteza uwezo wa kuona, au wakati mwingine wanakuwa viziwi kidogo, wanapoteza kusikia ...Au mara nyingi, katika tabia ya maisha wanapoteza kunuia na vijana wanaweza kunuia na wasipoteze tabia hiyo. Wao wanaweza kunuia kiukweli na hii ni jambo kubwa. Suala la kunuia alikuwa nako Yohana, maana  mara tu alipomwona yule bwana, yule jamaa aliyesema: “Tupeni kulia nyavu, alinuia kwa haraka na kusema “Ni Bwana!” Huyo alikuwa mdogo kati ya mitume.

Mkutano wa papa na vijana jijini Vatican 18.04.2022
Mkutano wa papa na vijana jijini Vatican 18.04.2022

Baba Mtakatifu Francisko kwa maana hiyo amesema  “Ninyi mnanuia na  Msipoteze! Kwa kunuia kusema “Hii ni kweli na  hii sio kweli,  hii sio nzuri, kunuia kumtafuta Bwana. Kunuia Ukweli. Baba Mtakatifu amewatakia waweze kunuia kama Yohane, lakini pia kuwa na ujasiri wa Petro, kwa sababu Petro alikuwa maalum: alimkana Yesu mara tatu lakini mara tu yule mdogo zaidi, aliposema: “Ni Bwana!”, Alijitupa majini ili kumtafuta Yesu. Baba Mtakatifu amewashauri vijana wasiwe na aibu kwa shauku yao ya ukarimu: Kwa kunuia kuwaongoze katika ukarimu. “Jitupeni maishani, amewashauri. “Lakini  Baba, mimi sijui kuogelea, ninaogopa maisha!  Siyo hivyo Mna mtu ambaye anawasindikiza, tafuteni wa kuwasindikiza. Lakini msiogope maisha, tafadhali! Ogopa kifo, kifo cha roho, kifo cha siku zijazo, kufungwa kwa moyo hiyo ndiyo ya kuogopa. Lakini ya maisha, hapana: maisha ni mazuri, maisha ni kuishi na kuyatoa kwa  wengine, maisha ni kushiriki na wengine, si kuyafunga ndani binafsi”, Papa amesisitiza bila kusoma, hotuba aliyokuwa ameiandaa.

Mkutano wa vijana na Papa Francisko Jijini Vatican 18.04.2022

Na hatimaye Baba Mtakatifu amesema kwamba  hakutaka kuongeza mengi zaidi ila alipenda kusema kwamba ni muhimu kwenda mbele. Na hofu? ziangaziwe na zisemwe. Na kukatishwa tamaa? Shinda kwa ujasiri, na mtu anayekuunga mkono, na mtu anayekwenda mbele. Na kunuia kwa uzima, msipoteze: hili ni jambo zuri. Na katika wakati wa shida, watoto huwaita  mama zao, hivyo hata sisi pia tunamwita mama yetu, Maria. Kuweni waangalifu  Yeye alikuwa karibu  na umri kama wenu  alipokubali wito wake wa ajabu wa kuwa mama wa Yesu. Katika umri wenu, zaidi au kidogo ... Yeye anaweza kuwasaidia kujibu “Tazama Mimi hapa, Bwana: nifanye nini? Niko hapa kufanya mema, kukua vizuri, kusaidia wengine na kunuia”.  Mama Yetu, mama ambaye alikuwa karibu na rika lenu alipopokea tangazo la Malaika na kupata mimba, awafundishe kusema: “ Tazama Mimi hapa!”, Wala msiogope. Muwe na ujasiri, na kuendelea! Papa amewahimiza. Na mara baada ya baraka, Papa amesema: “Yesu Mfufuka awe nguvu ya maisha yenu: enendeni kwa amani na furaha, ninyi nyote: kwa amani na furaha!

HOTUBA YA PAPA KWA VIJANA WA ITALIA 18.04.2022
18 April 2022, 18:56