Tafuta

Papa Francisko:Nchi maskini hazina uwezo wa kutibu wagonjwa,sera za kisiasa zahitajika!

Papa Francisko katika nia za sala kwa Mwezi Aprili 2022 kwa njia ya video,amejikita kuwatazama wahudumu wa kiafya ulimwenguni.Katika ujumbe kwa njia ya video Papa anashutumu matumizi mabaya ya rasilimali katika afya na anaomba serikali na jumuiya mahalia kuunga mkono kujitolea kwa madaktari,wafanyakazi wa kujitolea,watawa katika kusaidia wagonjwa na wazee.

Na Angella Rwezaula – Vatican

Sauti ya king'ora cha gari la wagonjwa, linalosikika kichini chini katika historia ya mara kwa mara katika miezi ambayo janga la Uviko lilifikia kilele chake, inafungua ujumbe wa kwa njia ya video na nia ya sala ya Papa Francisko kwa mwezi wa Aprili 2022. Sauti ya Papa Francisko inaingizwa kama kunong'ona: “Tuombe mwezi huu kwa ajili ya wahudumu wa afya" anazungumza kwa lugha ya Kihispania, huku picha za madaktari na wauguzi zikipita, kundi linalolazimika kutoa huduma zao ndani ya mfumo dhaifu wa afya kwa sababu Papa Francisko anasisitiza, kuwa hilo "ni tunda na matokeo ya usimamizi mbaya wa rasilimali na ukosefu wa jitihada kubwa ya kisiasa". Katika video iliyotolewa na Mtandao wa Sala ya Papa Kimataifa, Papa anarejea dharura ya kiafya ambayo imeonesha wazi juu ya kazi ya kujitolea na kujinyima ambayo imekuwa ikifanywa na watu wa kujitolea, wafanyakazi wa afya, mapadre na wa watawa hivyo Papa anasema: “Janga hilo limetuonesha kujitolea na ukarimu wa wafanyakazi wa afya.”

Wito wakati wa sala ya Malaika wa Bwana huko Gemelli

Hata hivyo kiukweli janga hili daima limeleta mapungufu ya mifumo ya afya na ukosefu wa usawa katika kupata huduma ya kutosha. Kwa maana hiyo Papa anasema: “Sio kila mtu anaweza kufikia mfumo mzuri wa afya ya umma”. Na hil tatizo kubwa ambalo tayari limeshutumiwa katika matukio mengine, ambayo  si haba hata katika sala ya Malaika wa Bwana ambayo haitasahaulika ya mwezi Julai 2021,  kutoka kwenye balcony ya Hospitali ya Gemelli mara baada ya kupata Opesheni ya Utumbo mpana. “Katika siku hizi za kulazwa hospitalini, nimeona kwa mara nyingine jinsi huduma bora ya afya ilivyo muhimu, inayofikiwa na wote ... Huduma ya afya ya bure ambayo inahakikisha huduma nzuri inayopatikana kwa wote. Hatupaswi kupoteza mali hii ya thamani”, alisema Papa Francisko. Kwa maana hiyo katika ujumbe wake kwa njia ya vedeo  Papa Francisko anasema “Wazee, wanyonge na walio hatarini zaidi sio kila wakati wanahakikishiwa kupatahuduma, na sio kila wakati kwa njia ya usawa. Hii inategemea uchaguzi wa kisiasa, jinsi rasilimali zinavyosimamiwa na kujitolea kwa wale wanaoshikilia nafasi za uwajibikaji. Kuwekeza rasilimali katika matunzo na usaidizi wa wagonjwa ni kipaumbele kinachohusishwa na kanuni kwamba afya ni manufaa ya msingi kwa wote”

Serikali na jumuiya mahalia zisaidie wafanyakazi wa afya

Maneno ambayo yanarudiwa katika ujumbe wa video wa mwezi Aprili 2022, uliotafsiriwa katika lugha 23, na matangazo ya vyombo vya habari katika nchi 114, Papa Francsiko anasema: “Tusali ili wafanyakazi wa afya katika kusaidia wagonjwa na wazee, hasa katika nchi masikini zaidi, waungwe mkono na serikali na serikali mahalia za jumuiya”.  Askofu wa Roma anaongeza: “Ninataka kuziomba serikali za nchi zote za dunia kutosahau kuwa huduma bora ya afya inayofikiwa na watu wote ni kipaumbele”. Wakati huo huo, katika filamu unaweza kuona fremu, zinazopendekeza jinsi gani zinavyo staajabisha, za vibanda vinavyotumika kama kliniki barani Afrika au picha za Dk. Erik Jennings Simões ambaye amekuwa akiwasaidia watu wa kiasili wa msitu wa Amazonia wa Brazili kwa miaka ishirini.

Papa alianzisha Mfuko wa hospitali za Kikatoliki

Mbele ya picha hizo, Papa Francisko ambaye alianzisha hata Mfuko wa hospitali za Kikatoliki amerudia tena kueleza malalamiko yake kwa nguvu: “Nchi maskini zaidi, nchi zilizo hatarini zaidi, haziwezi kupata matibabu muhimu ili kukabiliana na magonjwa mengi yanayoendelea kuwasumbua. Mara nyingi hii ni kwa sababu ya usimamizi duni wa rasilimali na ukosefu wa jitihada thabiti ya kisiasa”.

Kampeni katika mabara matano

Kwa mujibu wa ripoti ya (OECD)2021, inabainisha hali mbaya ya mfumo wa afya kuwa imeathiri utunzaji unaopokelewa na wagonjwa. Uhaba wa wahudumu wa afya umekuwa na athari kubwa kuliko ule wa vitanda vya hospitali au vifaa vya kiufundi. Katika mazingira magumu kama haya, ambayo yamezidisha tofauti zilizopo, jukumu la kuamua lilichezwa na kujitolea kwa wafanyakazi wa afya katika mipango mbali mbali katika mabara matano, iliyosimuliwa na picha za video ya Papa: Kuanza kampeni ya “Chanjo kwa ajili yetu, ya  “Kwanza mama na watoto” ya Cuamm, ya  Madaktari na Afrika, hadi mpango wa  AVSI nchini Uganda ya kuwapeleka wajawazito hospitalini kwa kutumia teksi ya pikipiki, na kuanzia na kazi ya agizo la hospitali ya Mtakatifu Yohane wa Mungu katika nchi mbalimbali hadi kufikia ile ya Watawa Wakamillian nchini Thailand na Brazili, na wengine wengi.

Kutoa  maisha  kwa ajili ya wagonjwa

Kwa hakika, Papa Francisko anakumbusha kwamba huduma ya afya sio shirika tu, bali inajumuisha wanaume na wanawake wanaojitolea maisha yao ili kutunza afya ya kila mmoja wao, na ambao wakati wa janga hili la uviko walitoa maisha yao kusaidia wagonjwa wengi. Kwa maana hiyo anasema: “Hata hivyo, kazi ya ziada ya wafanyakazi wa afya katika miaka hii miwili haiwezi kuwa suluhisho la kuhakikisha usaidizi wa kutosha kwa wote. Mwaliko basi ni ule wa kuwa na dhamira thabiti na ya kudumu ya kuhakikisha huduma bora ya afya inayotolewa kwa wote”.

Padre Fornos (Js): hatari ya magonjwa mengine

Kwa maoni yake Padre Frédéric Fornos, mkurugenzi wa kimataifa wa Mtandao wa Sala ya Papa Kimataifa amesema, katika nia hizi sa sala ya Papa amsema “Papa Francisko daima yuko makini sana kwa watu, wagonjwa, wazee, na walio hatarini zaidi”.  Wafanyakazi wa afya wanaowasaidia wamepitia hali ya shida na mara nyingi bila usaidizi wa kutosha, hasa katika nchi zilizo na rasilimali chache, kwa maana hiyo: “Papa anaomba waungwe mkono kwa rasilimali zaidi, vinginevyo tutajikuta tunakabiliwa na mangonjwa mengine ya mlipuko”.

NIA ZA SALA YA PAPA KWA MWEZI APRILI 2022
05 April 2022, 16:55