Papa Francisko:Ulimwengu ni maskini wa ubinadamu!
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kuwakaribisha Jumuiya ya Kichungaji ya Madhabahu ya “Mama wa Machozi” kutoka Treviglio nchini Italia, waliofika kwa wingi sana karibia elfu tatu kufanya hija jijini Roma wakiadhimisha miaka 500 ya kutokewa na Mama Maria wa machozi Jumamosi tarehe 23 Aprili 2022. Papa Francisko amesema:“Ninamshukuru Paroko kwa maneno yake na ninamsalimu pia kwa moyo Askofu wenu. Asante kwa kuja wengi namna hiyo! Labda nyumbani amebaki Mama peke yake! Ametania Papa. Amefafanua kuhusiana na mama wa Machozi na kwamba sio madhabahu pekee yake yenye kuitwa jina hilo. Amekumbuka kwa haraka madhabahu ya Siracusa huko kisiwani Sicilia, lakini ya kwao ni ya kizamani sana, ambayo inaadhimisha miaka miatano. Na vile vile inasifika sana kuhusu machozi ya Bikira Maria aliyetokea huko La Salette.
Papa amesema machozi ya Mama Maria ni kioo ca machozi ya Yesu, Yesu alilia, kama Injili inavyoeleza matukio mawili juu moja juu ya kaburi la rafiki yake Lazaro (Yh 11,35) na mbele ya Yerusalemu, (Rej. Lk 19, 41). Matukio yote mawili yalikuwa ni machozi ya uchungu. Lakini tunaweza kufikiria kuwa Yesu alilia hata kwa furaha kwa mfano alipokuwa akiona walio wadogo, wanyenyekevu wa watu wakipokea kwa shauku Injili. Maria, Mama ni mfuasi wa kwanza. Mama ni zaidi ya mwanafunzi. Alimfuata Mwanae kwa kila kitu hata katika utakatifu wa hisia, wa mhemko, hata katika vicheko na katika machozi. Kwa uhakika kutoka katika macho yake yalitiririka machozi ya furaha alipomzaa Yesu katika pango la Bethlehemu na aliwaona wachungaji na Mamajusi wa kiinama kusujudu mbele yake. Na mwishowe alilia machozi ya uchungu alipokuwa akimfuata kwenda njia ndefu ya mateso na alipokuwa amekaa chini ya msalaba. Mama ambaye analia.
Machozi ya Maria yalibadilishwa kwa neema ya Kristo, kama ilivyo maisha yake yote, kila kitu kwa Maria kilibadilishwa katika ukamilifu wa muungano na Mwana, kwa fumbo lake la wokovu. Kwa maana hiyo Maria anapolia, machozi yake ni ishara ya huruma wa Mungu. Mungu ni mwenye huruma kwetu sisi daima; Yeye anapenda kutusamehe. Papa amewakumbusha jambo moja kwamba Mungu anasamehe daima, Ni sisi ambao hatupaswi kuchoka kuomba msamaha. Na maana hiyo machozi ya Mama ni ishara tosha ya huruma ya Mungu ambaye kwa huruma hiyo anatusamehe daima; ni ishara ya uchungu wa Kristo kwa sababu ya dhambi zetu, kwa ajili mabaya ambayo yanatesa ubinadamu, hasa walio wadogo, wasio na hatia ambao ni wale wanaoteseka.
Baba Mtakatifu amemtaja Padre Nobert kwa maneno yake aliyosema, kuwa machozi ya Maria ni sawa na machozi ya Mungu kwa ajili ya waathirika wa vita ambavyo vinaendelea kuharibu, na si tu nchini Ukraine. “Tuna ujasiri na tuseme ukweli: vita viko vinaharibu watu wote ambao wamehusishwa katika vita. Ni wote kwa sababu vita haviharibu watu walioshindwa tu. Lakini vinaharibu hata washindi; Vinaharibu hata wale ambao wanatazama habari za kijujuu ili kuona ni nani mshindi na ni nani ameshindwa. Vita vinaharibu wote”. Baba Mtakatifu ameomba kuwa waangalifu katika hilo.. Kwa moyo wake safi wa Bikiria Maria Papa ameongeza kusema kwamba walimkadhi sala na kuwa na uhakika kwamba alisikiliza na anaendelea kuomba kwa ajili ya amani kwa sababu yeye ni Malkia wa Amani. Ni Mama kweli wa Amani na Jumapili ni Dominika ya Huruma. Na yeye ni Mama wa Huruma. Anajua nini maana ya huruma kwa sababu alipewa kutoka kwa Mungu.
Kwa karne tano za ardhi yao iliyo lowanishwa na machozi ya Maria; kizazi hadi kizazi cha watu wao wanasindikizwa na upole wa kimama. Yeye, Mama anawafundisha wasiwe na aibu ya machozi. Hawapaswi kuwa na aibu ya kulia, na zaidi, watakatifu wanafundisha kuwa machozi ni zawadi na wakati mwingine ni neema, kuitumia, na kujihisi uhuru wa moyo. Kulia kuna maana ya kujifungua, kuvunja ugumu wa umimi ulifuungwa ndani binafsi na kujifungulia upendo ambao unatukumbatia na ambao daima unatusubiri kutusamehe amesisitiza Papa. “Na ndivyo ilivyo moyo wa Mungu. Mungu anasubiri: je anasubiri nini? Anasubiri Msamaha yaani kutusamehe. Yeye hana utulivu, hawezi kurekebishwa: anataka kusamehe, Yeye anaomba tu kwamba tunamwombe msamaha. Na hivyo anataka tujifungulie kwa Baba mwema na hata kujifungulia kwa ndugu”. Papa amewashauri wajiachie katika upole wa kimama, waache aguse majeraha ambayo wanakutana nayo katika safari ndefu ya maisha; ili kujua kushirikishana, kukaribishana na kujua kufurahi na yule anayefurahi na kulia na anayelia.
Papa Francisko amesema kwamba katika nyakati zetu, kwa kuzungumza tumepoteza tabia kulia. Labda tunalia inapotokea jambo fulani linalogusa au tunapokata vitunguu. Lakini machozi yatokayo moyoni, yaliyo ya kweli ni kama yale ya Petro aliyetubu na kama yale ya Mama Maria. Ustaarabu wetu, katika nyakati zetu, umepoteza maana hiyo ya machozi. Sisi tunapaswa kuomba neema ya kulia mbele ya mambo ambayo tunaona mbele ya matumizi ambayo anafanya ubinadamu si tu vita, Papa amekumbusha kwa mara nyingine tena kwamba pia ubaguzi, wazee waliobaguliwa , watoto waliobaguliwa hata kabla ya kuzaliwa… Majanga mengi sana ya kutupa; aliye masikini huko na hana riziki anatupwa. Viwanja, mitaa iliyojaa watu wasio na makazi, wafukara wa wakati wetu wanapaswa kutufanya kulia na tunahitaji kulia. Kuna Misa katika Liturujia Katoliki ya kuomba zawadi ya machozi. Lakini wao ambao wana Mama wa Machozi amewawaomba waombe zawadi hiyo. Na sala ya Misa ya kuomba machozi inasema hivi: “Ee Bwana, wewe uliyetoa maji kutoka mwambani, ufanye machozi yatoke kwenye mwamba wa moyo wangu. Moyo wa mwamba ambao umesahau kulia. Tafadhali ninaomba neema ya kulia”.
“Na kwa hilo, machozi ya Maria yanatusaidia. Ni muhimu kwamba ubinafsi wetu husifungwe, uwe wazi kwa wengine, hasa kwa Baba anayesamehe na kwa ndugu. Ni lazima tujiruhusu kuguswa, na majeraha ya wale tunaokutana nao njiani, tujue jinsi ya kushiriki, tujue kukaribisha, tujue kufurahi pamoja na wale wanaofurahi na kulia pamoja na wale wanaolia. Jumuiya yao inachukua jina hilo: ‘Mama wa Machozi’. Ni vizuri hili! Papa ameongeza, “Katika jina ili kuna uchungaji wote. Uchungaji wa upole, wa huruma na ukaribu. Na huo ndio mtindo wa Mungu ambaye alijifanya kuwa karibu, uhuruma na upole. Kuna mtindo wa kichungaji ambao unatazama wote: mapdre, mashemasi, waamini walei, na watawa…. Wote wanakuwa karibu kwa huruma na kwa upole sana. Na rika zote, hatua zote za maisha”. Papa Francisko ameendelea kukazia kwamba “Wote lazima na daima kujifunza kutoka kwa Maria kufuata Yesu, kuacha roho mtakatifu aongoze hisia zetu, shauku zetu, mipango yetu na matendp yetu kwa mujibu wa moyo wa Mungu”. Na hiyo ni kwa sababu kama sala nzuri ya kiliturujia inavyosema: “Nafsi zetu zisiwe na nguvu ndani yetu, bali utendaji wa Roho wake Mtakatifu”. Kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu amewashukuru tena kwa ziara yao! Baba Mtakatifu Francisko mewashukuru kwa sababu ya kumsaidia kutoa tafakari juu ya machozi ya Mama yetu na mama yao. “Hiyo ni kwa sababu wote tunahitaji na tuna haja ya kula sana”. Amewabariki kwa moyo wote na familia zao pamoja na jumuya yao.