Papa Fransisko:upendo hufanya kazi kwa watu unaowasaidia
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amekutana Ijumaa tarehe 8 Aprili 2022 na wajumbe wa Chama cha “Marcello Candia” na kuwashukuru kukutana nao na kumshukuru Mungu kwa miaka 40 tangu kuanza shughuli ya Chama hicho. Candia alikianzisha mnamo 1982 na mwakauliofuata akafariki. Kwa sasa wanamheshimu kama mtumishi wa Mungu na kuomba maombezi yake, hasa kwa ajili ya magonjwa, maskini zaidi na walioachwa pembezoni mwa Kaskazini Mashariki mwa Brazili mahali yeye alipofanya kazi kwa miaka mingi. Papa Francisko amewashukuru kwa jitihada na kuanzisha shughuli nyingine. Hasa kwa njia na mitindo ambayo wanapeleka mbele aliyoianzisha Marcello Candia na ambayo aliipokea kutoka kwa Mtakatifu Paulo VI. Baba Mtakatifu kwa maana hiyo amependa kutazama kwa upya pamoja maelekezo na ili waweze kufanya vizuri zaidi.
Awali ya yote amesema Paulo VI alimwambia Candia kuwa: “Ikiwa inawezekana kujenga Hospitali Brazili, uwe kama mbrazili..” Kwa maana ya kujikita ndani ya hali halisi mahalia, kujihusisha na watu wa eneo hilo… Hata kama kabla labda kidogo angeweza kuweka mtindo wa Milano…. Papa ameongeza kusema. Utamadunisho ni kuchukua utamaduni wa eneo hilo mahali na kuishia mbapo tunakwenda kufanya kazi. Paulo VI aliendelea kusema kuwa “Kuwa mwangalifu na epuka aina yoyote ya ubaba, usilazimishe maoni yako kwa wengine, hata kwa nia njema". Kwa maana hiyo Candia alikuwa ni mjasiriamali, alikuwa amezoea kuamua binafasi, kwa sasa alikuwa ajifunze kuongoza mambo ya mwingine kwa mtindo mwingine. Papa amerudia kusema " Utengeneze shule, si kwa ajili ya Wabrazii, lakini na Wabrazili”, “Si tu kwa ajili ya… lakini na…” Hii ni muhimu, ni kanuni kuu ya upendo: wa kufanya kazi na watu mahalia katika huduma”. Papa Paulo VI aliongeza: “pendekeza kama lengo la mwisho la kuwa wewe sio wa lazima tena”.
Kwa maana hiyo Papa ameongeza: “Hii ni busara! mara nyingi hapa, hata sisi katika Kanisa, tunapata watu wa thamani, mapadre, maaskofu, lakini wanaamini kwamba historia ya wokovu inapita kutoka kwao, kwamba ni muhimu. Hakuna mtu, anayehitajika kabisa. Ni muhimu kufanya kile unachopaswa kufanya, na baadaye, historia hiyo, Mungu, itasema ikiwa itaendelea na ikiwa mwingine atakuja ... Hii ni nzuri: "Na ifanyike kwa lengo la mwisho ambalo wewe sio wa lazima tena". 'Ni Mwenye hekima.' Ikiwa utagundua kuwa Hospitali inajiendesha, ndipo utakapotambua kuwa ni kazi ya kweli ya mshikamano wa kibinadamu. Hii pia ni sheria ya busara sana: usiwafunge watu na ujifanyie kazi, usijifanye kuwa wa lazima, lakini kinyume chake wafunze washirika wenzako na uhakikishe utulivu na mwendelezo.
Baba Mtakatifu Francisko amewapongeza kwa sababu ya jitihada za nguvu wanazoweka katika kufuata njia hiyo. Kwa hakika mfuko huo haujiendeshi na kazi zake binafasi, bali unasaidia na jumuiya mahalia na wamisionari katika shughuli na wagonjwa, wakoma, na watu mbali mbali katika hali halisi ya mahitaji. Na sifa nyingine waliyo nayo ni kwamba gharama za matengenezo ya Mfuko huo wa chama ni ndogo, karibu kila kitu huenda kwenye kazi nchini Brazil. “Na hii ni muhimu sana, kwa sababu kuna mashirika na vyama vya kazi vinavyofanya mema, japokuwa wana muundo wa watu, wa mambo ambayo labda hataki kuweka chumvi kwani nusu au 60% inakwenda kulipa mishahara. Hii sio nzuri", Papa amesisitiza. "Kiwango cha chini, kwa sababu kiwango kikubwa cha pesa lazima kiende kwa watu. Hili ni muhimu, liendelee”. Baba Mtakatifu amewashukuru kwa ujio wao na kuwatia moyo wa kwenda mbele katika roho na mtindo wa Mtumishi wa Mungu Marcell Candia. Na Mama Maria aawasindikiza. Baraka yake aliyowapatia , ameomba iwe kwa wahuduma wote walioko Italia na Brazili. Na pia, tafadhali, wasisahau kumwombea kwa sababu kazi hii sio rahisi hata kidogo. Amewabariki, pia shukrani zake kwa kile wanachofanya kwa njia hiyo, kila siku na kwa siri: hii ni nzuri sana!