Papa:kama kaka na dada tuchangie kusimamisha uharibifu wa dunia
Na Angella Rwezaula - Vatican
Tarehe 22 Aprili ya kila mwaka ni Siku ya kimataifa ya Mama Dunia ambapo ni fursa muhimu ya kutambua sayari hii inayotutunza na ambayo tunazidi kuiharibu kila kuchapo, kuinyonya rasimali zake na kuiweka katika hatari za sa na siku zijazo. “Sisi sote tunapaswa kuchangia kusimamisha uharibifu wa nyumba yetu ya pamoja na kurudisha nafasi za asili. Serikali, mashirika, makampuni, raia lazima kutenda kwa dhati kama kaka na dada ambao wanashirikishana ardhi, nyumba ya pamoja ambayo Mungu alitukabidhi” Huu ndiyo ujumbe mfupi wa Papa katika Tweet yakae katika Siku ya Earth Day, yaani siku ya kimafaita ya Mama dunia. Ni Nchi 193 ambazo tarehe 22 zinasheherekea Siku ya 52 ya Kimataifa ya Mama Dunia kwa ajili ya kuhamasisha utunzaji bora wa sayari.
Mtandao wa Kimataifa wa Earth Day ulioko Washington unahamasisha kwa hakika na na kwa upande wa Italia pia kuna makao yao ya Earth Day Italia, ambao wanawahusisha watu wengi, vyama na hali halisi ya kila aina ambayo ilizaliwa kwa upya kwa kuwa na dhamiri za mazingira na wanatenda matendo ya dhati kwa ajili ya utetezi wa Mama yetu Dunia. Kwa miaka mitatu sasa kila tarehe 22 Aprili wanaandaa Marathoni ya vyombo vya habari iitwayo #OnePeopleOnePlanet yaani ‘watu wamoja na sayari moja’, inayojikita kuhusisha shule na vijana, wakitoa ushuhuda na kupendekeza kupitisha kijiti cha sauti kwa ulimwengu mzima. Tukio hili lilifikiria kwanza kutoa ujumbe wa matumaini na ambalo linajumuisha vyombo vya habari vya Vatican vya Baraza la Kipapa la Mawasiliano, RAI, Ansa, Radio Italia na Washirika wengi zaidi.
Papa Franciko mara kadhaa amezungumzia kuhusiana na Siku hii ya Mama Dunia. Mnamo tarehe 22 Aprili 2015, baada ya Katekesi yake, alishauri wote kutazama dunia kwa macho ya Mungu Muumba na kuwa dunia na mazingira yake ya kulindwa na bustani zake kupaliliwa. Na zaidi alionya kwamba: “Uhusiano wa wanadamu na maumbile haupaswi kuongozwa na uchoyo, uendeshaji na unyonyaji, lakini lazima uhifadhi maelewano ya kimungu kati ya viumbe na viumbe katika mantiki ya heshima na huduma, ili kuiweka katika huduma ya ndugu, hata vizazi vya baadaye. Mwaka uliofuata mnamo tarehe 24 Aprili Papa Francisko alikwenda kwa kushangazwa na Village for the Earth, yaani kijiji kwa ajili ya Dunia kilichanzishwa huko Roma, kwenye mtaa wa Villa Borghese, kiliandaliwa na Mtandao wa Earth Day Italia, na Harakati ya Wafokolari. Katika hotuba yake aliwasifu wale wanaojitolea kubadilisha majangwa kuwa misitu, kuleta matumaini pale ambapo hakuna matumaini. Papa alisema: “Jangwa ni baya, lililo moyoni mwetu sote, na lililo ndani ya jiji, katika vitongoji, huku, akibainisha kwamba mtu asiogope kwenda jangwani ili kuibadilisha kuwa msitu; kuna maisha ya furaha, na unaweza kwenda kukausha machozi mengi ili kila mtu atabasamu.” Baadaye Papa Francisko alisisitiza umuhimu wa msamaha na kusema majuto, chuki na kwamba mambo haya hututenganisha. Lazima tujenge kila wakati, kwa ufahamu kwamba sote tuna kitu cha kusamehewa, lazima sote tufanye kazi pamoja, tuheshimiane, na kwa hivyo tutaona muujiza huu: wa jangwa ambalo linakuwa msitu.
Mnamo tarehe 22 Aprili 2020, katikati ya janga, kutoka Maktaba ya Jumba la Kitume, Papa alitoa katekesi nzima kwa ujumla katika Siku ya 50 ya Dunia Mama na akasisitiza kwamba ni muhimu kukua katika ufahamu wa utunzaji wa nyumba ya pamoja ambayo imenajisiwa na kuporwa. Papa Francisko pia alibainisha kuwa kwa pamoja na kuwatunza walio dhaifu, tu tunaweza kushinda changamoto za kimataifa, na pia akasema kwamba uongofu wa kiikolojia nampango wa pamoja inahitajika ili kuzuia kuzorota kwa Dunia, kutunza kila kitu, kiumbe na kulea upendo na huruma kwa wengine. Dunia sio ghala la rasilimali Papa aliongeza, lakini kwa sisi waamini ulimwengu wa asili ni Injili ya Uumbaji, huku akibainisha tena kwamba sisi ni familia moja ya kibinadamu inayotegemeana, iliyofanywa kwa vitu vya dunia, na pumzi muhimu inayotoka kwa Mungu, na kwa hivyo katika sura ya Mungu , lakini hiyo kwa sababu ya ubinafsi, tumeshindwa katika jukumu hili la kuwa walinzi wa dunia, tukiweka maisha yetu hatarini. Hakuna wakati ujao kwetu ikiwa tutaharibu mazingira yanayotuunga mkono, Papa Francisko aliendelea, akihimiza kujitolea, kuandaa uingiliaji wa pamoja katika ngazi ya kitaifa na ya kikanda pia kutoa uhai kwa harakati za watu katika nchi.
Na maneno yake yaliyoandika kwa Siku ya Dunia Mama moja kwa moja 2021 #Rejesha Dunia Yetu. Papa Francis pia alielezea kwamba kutokana na janga hili kuna kujifunza kutegemeana, kushiriki huku kwa sayari, wakati huo unatusukumana kwamba ni wakati wa kuchukua hatua kwa sababu tuko kwenye kikomo. Pia alinukuu msemo wa zamani wa Kihispania: Mungu husamehe kila wakati, sisi wanadamu tunasamehe mara kwa mara, asili lakini haisamehe tena. Na alibainisha kuwa uharibifu huu wa asili unapotokea, ni vigumu sana kuuzuia. Lakini bado tuna wakati. Pia alihimiza ubunifu, uvumbuzi, kutafuta njia mpya na kwa kuangalia janga hilo alibaini: Kutoka kwa shida hautoki sawa, tunatoka bora au mbaya zaidi. Hii ndio changamoto, na ikiwa hatutatoka bora tunapita kwenye njia ya kujiangamiza”. Na kulikuwa na wito kwa viongozi wote wa ulimwengu kufanya kazi kwa ujasiri, kufanya kazi kwa haki na kuwaambia watu ukweli kila wakati, ili watu wajue jinsi ya kujilinda kutokana na uharibifu wa sayari, jinsi ya kulinda sayari kutokana na uharibifu. uharibifu ambao mara nyingi tunasababisha.