Papa Francisko amekutana na Wawakilishi wa Watu Asilia kutoka Manitoba nchini Canada, Papa Francisko amekutana na Wawakilishi wa Watu Asilia kutoka Manitoba nchini Canada, 

Papa amekutana na Wamétis wa Manitoba:"Ametugusa moyo"

Wajumbe karibu hamsini wa shirikisho la Wametis wa Manitoba,ambalo limekuwa sasa serikali ya kijitegemea mara baada ya makubaliano na Serikali mnamo 2021,wamefika Roma kutoka Canada ili kuendeleza na mchakato wa upatanisho na Kanisa mara baada ya nyanyaso katika shule za bweni.Mwenyekiti wa Chartrand amesema ujumbe wao si wa upatanisho tu lakini pia wa matumaini.Papa Francisko anatazama mbali kwa ajili ya wakati ujao.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Machozi, kumbu kumbu, historia, shukrani kwa sababu ya kuomba msamaha na kuomba ziara ya kutembelea ardhi yao, ni mambo ambayo yamesikika katika mkutano wa kina na wa hisia kali ambapo Papa Francisko amekutana na Watu wa Asilia 55 wajulikanao 'Métis Manitoba Federation',  yaani Shirikisho  la Watu Asilia kutoka nchini Canda ambao wamepokelewa asubuhi na Baba Mtakatifu tarehe 21 Aprili 2022 katika ukumbi wa Clementina jijini Vatican.  Hii ni serikali ya kweli ya Canada ambayo ilitia saini mkataba wa kujitegemea na Serikali mnamo tarehe 6 Julai 2021.  Wajumbe wajulikanao kama “Red River Métis” yaani 'Watu wa Asilia wa Mto Mwekundu' wanaishi hasa katika Mkoa wa Manitoba, uliopo Kaskazini Magharibi mwa Canada. Na kwa sababu hiyo shirikisho hilo halikushiriki katika mikutano iliyofanyika mwishoni mwa mwezi Machi na Papa Francisko na watu wa Asilia wa Canada (Métis, Inuit enaFirst Nation), ambao walikutana baada ya maandalizi na kwa hawamu jijini Vatican.

Papa alikutana na Wajumbe wa Shirikisho la Wametis nchini Canada
Papa alikutana na Wajumbe wa Shirikisho la Wametis nchini Canada

Ujumbe wa matumaini na upyaisho

Pamoja na watu wengine wa Asilia lakini hata wengi  kutoka Métis ya Manitoba walipata nyanyaso za ndani kwa kile kiitwacho “shule za bweni”, zilizokuwa zimeanzishwa na Serikali na kukabidhiwa kwa Makanisa ya Kikristo, miongoni hata za kikatoliki. Tendo ambalo Papa Francisko katika mkutano wa tarehe Mosi Aprili, kwa uwepo hata wa maaskofu wa Canada, alielezea uchngu na aibu na kuomba msamaha. Ulikuwa ni ujumbe wa nguvu ambao kwa watu hawa walikuwa wakisubiri kwa miaka mingi. Watu wa Asili wa Métis ya Manitoba wamebaki wameshangazwa kwa nguvu sana kutokana na ishara na maneno ya Papa Francisko , kama alivyoeleza mwenyekiti David Chartrand katika ujumbe uliondikwa kuhusiana na mkutano huo mjini Vatican na kwamba ameomba maandalizi ya miaka mitatu.

Papa alikutana na Wajumbe wa Shirikisho la Wametis nchini Canada
Papa alikutana na Wajumbe wa Shirikisho la Wametis nchini Canada

Katika ujumbe wake ameandika: "Kama ilivyo watu wote  wa asili wa Canada, kwa namna ya pekee kama sisi ambao tulipata madhara kwa mikono ya watu ambao walificha ubaya wao nyuma ya Kanisa Katoliki, amenipa faraja kusikia Papa Francisko anawakilisha msamaha wa pamoja. Ninajua kuwa Wamétis wa Mto Mwekundu walikuwa wanasubiri kuombwa msamaha kwa miaka mingi. Ni matumaini kuwa itasaidia kuanza mchakato wa uponeshaji na wanaungana nasi katika safari hii ya upatanisho, uuisho na upyaisho”. Maneno hayo ya Chartrand hata hivyo ameyarudia katika uwanja wa Mtakatifu Petro mbele ya kikundi cha waandishi wa habari waliokutana nao mara tu baada ya mkutano katika ukumbi wa Clementina. Kwa mujibu wake ameeleza kuwa: “Ujumbe wetu ulikuwa kidogo ni tofauti. Tulikuwa kwa hakika kumpongeza na kukubali samahani ya Papa na tulizungumza pia juu ya upatanisho lakini tulikuwa na ujumbe mkubwa zaidi wa matumaini na upyaisho".

Machozi na huruma

“Machozi yaliyotiririka ndani humo, historia ambazo zimeshirikishwa, Baba Mtakatifu amezipokea kwa neema kubwa na tulishangazwa namna hiyo alipoomba msamaha”, alisema kiongozi wa watu Asilia. Muhanga mmoja kwa jina Andrew, “aliyelipata gharama nzita kiwa mtoto” amepata uwezekano wa kusimulia suala lake binafsi kwa Papa na ambaye ameonesha kuwa na uvumilivu, umakini na hisia kali, kwa maana hiyo “Ametugusa kwa moyo hasa kwa kuona huruma yake”. Wawakilishi hawa wameomwonesha Baba Mtakatifu mkatabata uliotiwa saini huko Canada. Papa Francisko ametia saini, katika  kopi ambayo itawekwa katika makumbusha na itawekwa hivi karibuni. Watu wa Asilia baadaye walimkabidhi Papa zawadi zao, kimsingi ni shughuli zao za kiufundi zilizoandaliwa na shanga hata zile  za miaka 300 iliyopita,ambayo ni ishara hai ya urithishwaji wa watu hawa. Kwa maelezo yake kiongozi huyo amesema: “ kazi yetu na shanga ni historia ya jinsi sisi tulivyo na kwa wakati ule tulijulikana kama watu wa Magharibi na shanga za maua” kwa sababu hawakujua waituiteje. Walikuwa wakituita damu nusu, au watu wa kijijini. Na hivyo kazi zetu zote zina maua ya uwanda wetu ambayo  inayosimulia historia yetu”.

Papa alikutana na Wajumbe wa Shirikisho la Wametis nchini Canada
Papa alikutana na Wajumbe wa Shirikisho la Wametis nchini Canada

Watu Asilia wametoa zawadi kwa Papa hata aina ya kandambili na misalaba ya miaka 1800. “Yeye ameshukuru kwa ukarimu wa watu wetu”. Papa akiwa bado katika simulizi za wageni wake, aliwasalimia kwa kuwa mikono wote waliokuwapo. Aliamka kutoka katika kiti chake na alikuwa anataka kwenda kwao. Walipomwona anavyochechemea walimwomba, akae na ili wao waende kwake. "Ilikuwa nzuri sana kumwona Papa na nguvu sana hivyo, shauku na hamu. Ametugusa mioyo yetu na wengi wetu hawatasahau tendo hili hadi wanaishi. Na ni heshima kubwa sana kwa wao kuona Papa kuwa na matazamio makubwa wa wakati ujao. Ni Papa kwanza wa Mungu na baadaye wa Vatican”, amesema kiongozi huyo wa Asilia.

Maombi ya kutembelea kaburi la  Louis Riel

Kwa upande wa Papa, kwa kila mmoja amemzawadia medali ya kipapa.  Walio wengi wamelia. Mkutano huo ulikuwa  pia ni fursa kwa ajili ya Wametis kumwalika Papa Francisko (ambaye amewakikishia utashi wa kwenda Canada na labda mwezi Julai) kutembelea eneo la Mkoa wa Winnipeg ili kubariki kaburi la Louis Riel, aliyekuwa ni kiongozi wa Wamétis, na aanayehemiwa na wao kama Baba wa Manitoba,  ambaye mnamo 1800 aliongoza harakati za wazalendo wa Red River  (Mto Mwekundu)  akitafuta kufuata haki na utamaduni wa watu  Asilia wakati ardhi yao ilipokuwa nakuchuliwa kuwa  chini ya  Canada. Waziri wa kwanza wa wakati ule alikuwa ni John A. MacDonald aliweka fadhila ya dola 5,000 juu ya kichwa chake na Riel aliuawa. Watu wa Asilia kwa maana hiyo walimwomba Papa kwamba, katika safari yake ya kwenda Canada, anaweza kupitia kwenye kaburi la mtu ambaye alitoa kila kitu, sio tu kwa ajili ya watu wa Wamétis, lakini kwa ajili ya Kanisa.

Papa alikutana na Wajumbe wa Shirikisho la Wametis nchini Canada
Papa alikutana na Wajumbe wa Shirikisho la Wametis nchini Canada
22 April 2022, 10:25