Tafuta

2022.05.24 Papa Francisko - Ufumaji wa dunia 2022.05.24 Papa Francisko - Ufumaji wa dunia 

Francisko:huruma hubadilisha maisha ya watu binafsi na jamii

Tunachapisha maneno ya baadaye ya Papa katika kitabu:“Ufumaji wa dunia”,mazungumzo yenye sauti kadhaa kuhusu simulizi kama njia ya wokovu, kilichochapishwa na Lev na Salani.Kimehaririwa na Andrea Monda,kuanzia 25 Mei kipo katika maduka ya vitabu ambacho kinakusanya sauti za wahusika wakuu wa utamaduni.Maandishi ya Papa yamechapishwa kwa ukamilifu na magazeti ya Avvenire,pamoja na vyombo vya habari Vatican.

PAPA FRANCESCO

“Historia tunazosimulia na kusimulia tena na  ambazo tunarithishwa  mmoja na mwingine ni  kama mahema ya kukusanyika ndani mwake, mabango ya kufuata katika vita, kamba zisizoweza kuharibika za kuunganisha walio hai na wafu na kuingiliana kwa njama hizi kubwa kupitia enzi na tamaduni zinazotufungamanisha sisi kwa sisi na kwa historia, zikituongoza kwa vizazi”. Ndivyo anaandika Donna Tartt baada ya kusoma kitabu hiki ambacho kinakusanya tafakari za waandishi 44, wasanii, wanataalimungu, waandishi wa habari juu ya mada ya simulizi. Mwandishi wa riwaya wa Amerika ananasa kwa umakini moja ya hoja ambazo waandishi wengi wa kitabu hiki wanakutana: hadithi kama “kitambaa”, kilichoundwa na “kamba zisizoweza kuharibika” ambazo huunganisha kila kitu na kila mtu, sasa na zamani, na inaruhusu sisi kujifungua hadi siku zijazo na hisia za uaminifu na matumaini.

Kipengele hiki cha maandishi (kwa ni Kilatino ili kuelekeza kitambaa ambacho maandishi yake ni ya Kiitaliano) kilikuwa kitovu cha Ujumbe wangu kwa Siku ya Upashanaji Habari Ulimwenguni 2020 ambacho kilikuwa kama cheche iliyotokeza tafakari nyingine zote zilizokusanywa hapa. Kuanzia Februari hadi Oktoba 2020, kiukweli usomaji wa Ujumbe wangu, uliochapishwa kwenye kurasa za Osservatore Romano uliibua maoni kwa umma. Baaadye niliombwa kuongeza hitimisho la mwishoni mwa mfululizo huu mzuri ambao tayari nilikuwa nimeusoma kwa furaha kubwa ulivyokuwa ukiendelea kwa miezi mingi. Kwa hivyo nilikubali kwa furaha, ikiwa tu hauchukuliwe kuwa ni mwisho kidogo kwa sababu, kama asemavyo Frodo, mhusika mkuu wa ‘Il signore degli anelli di Tolkien’, yaani ‘Bwana wa pete ya Tolkien’, “hadithi hazina mwisho” na baadaye kwa sababu kipengele kizuri sana cha kitabu hiki ni maana ya uwazi, ya mzunguko, na ya mazungumzo.

Kabla ya kurudi kwenye mada ya “yaliyomo”, kiukweli, ningependa kujikita  kwa ufupi juu ya “mbinu” ya kitabu hiki: mwanzoni kuna ujumbe unaozinduliwa; ujumbe huu unashirikishwa na kutolewa kwa tahadhari kwa baadhi ya watu wanaokubali kuulizwa maswali na kuimarisha ujumbe huo kwa mchango wao; mwandishi wa ujumbe anasoma michango hii yote na kuzindua kwa upya tafakari mpya ambayo ni tajiri zaidi kuliko ile ya awali kutokana na mchango wa wote; hatimaye, msomaji wa kitabu hiki ataingia katika mazungumzo haya na kuyaendeleza katika maisha yake ya kila siku. Hapa kuna “mahema ya kukusanyika” ambayo Tartt anazungumza, hapa kuna upatanisho ambao “unatufunga kwa nguvu” hata kwa vizazi.

Maneno na ukimya, pamoja. Yote haya yanasema mengi. Na anasema hasa kwamba katika historia kinachozingatiwa ni kusema, lakini labda kusikiliza zaidi. Kitabu hiki ni kufafanua mazungumzo ambayo hayaishii kwenye ukurasa wa mwisho na, kama mazungumzo, yana moyo wake katika kusikiliza. Hata kimya. Katika kurasa hizi za historia uwepo wa ukimya unahusishwa sana. Kwa mtazamo huo ni muhimu kwamba pia kuna insha, ninarejea katika maandishi: “Unazungumza hata ukiwa kimya” cha Massimo Grilli, aliyejitoa moja kwa moja kuzungumzia kuhusu ukimya. Takriban sehemu ya kukanusha, sehemu ya kupinga, ni muhimu kama mada kuu inayoimbwa na waimbaji wengine wa bendi. 

Na hapa ninataka kurudi kwenye vipengele vya maudhui ili kuonesha miongoni mwa uwezekano (mkusanyiko ni mzuri kwa sababu ya uhuru na aina mbalimbali za mitazamo na maoni), mada tatu ambazo zinaonekana kwangu zinazorudiwa mara kwa mara: Ya kwanza tayari nimesisitiza ya kusimulia historia kama “kufuma”; ya pili imefichwa ndani ya kumbukumbu ya ukimya, na ni mada ya “fumbo” ; ya tatu ni mada ya “huruma”. Kwanza, kama nilivyokwisha sema, kufuma labda ni kipengele ambacho waandishi wengi wanazingatia, wengine wakisisitiza jukumu la wanawake, kama vile Marcelo Figueroa, wengine wakisisitiza “kubadilika” kwa ufumaji wa historia”  zenye uwezo wa kukaribisha hali mpya na wapokeaji wapya” (J.P.Sonnet), wakati wengine kama Antonella Lumini wanazingatia uthabiti wa historia ambazo hata hivyo zipo, na kushikilia na mwelekeo, kama maji kwenye chanzo cha mto ambao baadaye unaingia baharini”.

Mada ya  fumbo, ilipungua kama hisia ya kikomo lakini pia kama “mazingaombwe” yanayoingilia wakati wa msukumo wa kishairi, na linapatikana kutoka katika maandishi wa kwanza, yale ya mbunifu Renzo Piano ambaye sisi sote wanadamu tumeunganishwa kwa ufahamu huu wa fumbo linaloruka juu yetu, linatuzidi. Hili pia linahusiana na ushairi. “Nisichojua, naweza kuimba” unataja wimbo wa mwimbaji wa Roma Francesco De Gregori aliyehojiwa katika mkusanyiko huo, na wasanii, anaongeza Judith Thurman, kwa uelewa wa kina, “lazima waandike sio sana juu ya kile wanachofanya,  kujua, lakini kuhusu wasiyoyajua walijua  mpaka wakamkomboa kutoka gizani.

Hisia ya fumbo inafungua kwa wale wanaopita maumbile, kuelekea mwelekeo wa kiroho usio na shaka, wa kidini. Donna Tartt anaona kwamba “labda, ni vizuri zaidi, historia ni turubai la matanga ambayo tunapandisha ili kunasa pumzi ya kimungu. Mawazo ya watu wengine huchukua maisha ya ajabu ndani yetu, na ndiyo maana fasihi ni sanaa ya kiroho zaidi ya yote na kwa hakika ndiyo inayobadilisha zaidi. Kama hakuna njia nyingine ya kuwasiliana, historia inaweza kubadilisha njia yetu ya kufikiri, kwa bora au mbaya [...] tamaduni za kale na za kisasa zimezingatia historia kuwa za viinimacho na hatari  kwa sababu moja: kwa sababu unaweza kusikia historia na, mwisho wake, kuwa mtu tofauti kabisa “.

Na hii inaongoza katika kipengele cha tatu, huruma, pia iko katika maandiko kadhaa yaliyokusanywa katika kitabu.  Kwa namna ya pekee mwandishi Marylinne Robinson, akikumbuka historia  na nyimbo ambazo mama yake alimsomea na kumwimbia, anaweka wazi huruma ambayo kwa maana yake pana na kwa muibu wake katika maisha ya roho, sawa na neema ya kimungu na baadaye anaongeza kwamba: “Historia inaonesha jinsi masimulizi yalivyo muhimu kwa jamii.” Kwa hivyo, fasihi inahusishwa na huruma na hii husababisha mabadiliko yanayotokea katika kila uandishi na usomaji, na hufanyika kwa njia isiyoeleweka, na kwa hivyo hatari ni kwamba historia pia inaweza kutoa nguvu hasi, ya ujanja, ya uharibifu.

Huruma, kama ninavyorudia mara nyingi katika mazungumzo yangu, ni mojawapo ya sifa tatu za mtindo wa Mungu, pamoja na ukaribu  kwa huruma. Kwa hiyo ni nguvu yenye nguvu, na haiwezi kupunguzwa tu kwa mambo ya ndani, kipengele cha karibu, kwa sababu pia ina mwelekeo wa umma, wa kijamii ili historia ijidhihirishe kama nguvu ya kumbukumbu, kwa hiyo mlezi wa siku za nyuma, lakini pia, hasa kwa hili, chachu ya mabadiliko kwa siku zijazo. Huruma hupata  picha inayowakilisha zaidi katika sura ya Msamaria Mwema iliyopo katika sura ya 10 ya Injili ya Luka. Mtu huyu ana huruma kwa mtu aliyejeruhiwa na anampatia huduma na uponyaji lakini pamoja nao pia historia nyingine ya maisha yake ambayo kwa ishara yake amemkomboa kutoka gizani. Huruma hubadilisha maisha ya wahusika wakuu wawili, na hii ni kweli kwa kila mtu na kwa kila jamii.

Mwelekeo huu wa “kisiasa” wa simulizi ikiwa tunataka, pia upo sana katika maandishi 44 ya kitabu. Ninafikiria tafakari ya Alessandro Zaccuri ambaye anamtaja Yesu kama “Masiaha msimulizi” ambaye anaonekana hana silaha lakini kwa uhalisia aliyepewa silaha yenye nguvu ya simulizi. Kama vile mwandishi wa riwaya wa Ireland, Collum McCann anavyoona katika masimulizi “moja ya njia zenye nguvu zaidi tunazopaswa kubadilisha ulimwengu wetu. […] Masimulizi ndiyo demokrasia yetu kuu. Ni jambo ambalo sote tunaweza kufikia. Tunasimulia historia  zetu kwa sababu tunahitaji kusikilizwa. Na tunasikiliza historia kwa sababu tunahitaji kuhusika. Simulizi huvuka mipaka. Huvunja dhana potofu. Na inatupatia ufikiaji wa maua kamili ya moyo wa mwanadamu”.

McCann anachodokeza ni hitimisho lililofikiwa na Daniel Mendelsohn anaposema kwamba “Neno ni daraja […] kupitia simulizi tunaweza kupunguza umbali unaotutenganisha na nadhani hii ni muhimu zaidi leo hii kuliko hapo awali”. Mendelsohn anarejea wakati ambapo maandishi haya yaliandikwa, mchango wake ni wa Aprili 2020, na anaonesha marejeo sahihi ya kifasihi: Decameron ya Boccaccio, iliyowekwa katika wakati janga la  tauni. Hata kitabu hiki chenye maandishi yake ya watu  44 kimetungwa wakati wa janga la uviko na tunahisi umuhimu, uharaka wa kurudi katika shughuli za zamani zaidi na ya kibinadamu: sanaa ya kusimulia historia ambayo ni, kujenga madaraja yanayoweza “kuunganisha walio hai na wafu, kutuongoza, katika karne na vizazi, kuelekea wakati ujao utakaojengwa, uliosukwa pamoja.

MAONI YA PAPA KATIKA KTABU KIPYA
27 May 2022, 15:13