Mtawa asiye kuhani katika Shirika anaweza kuwa Mkuu wa Shirika!
VATICAN NEWS.
Kuteuliwa kuwa mkuu wa Shirika au taasisi hata bila kuwa kuhani, katika mashirika ya kitawa au Mashirika ya Kazi za kitume zenye haki ya kipapa ndiyo inaweza kutokea kuanzia sasa na kuendelea kwa wale ambao wanafanya kuwa Sehemu ya familia ya Kitawa, kama vile wanashirika wasio mapadre au kwa kundi lile la wanashirika ambapo walio wengi wanaitwa "ndugu".
Hili limeanzishwa na Papa kwa maandishi ambayo yanaanza kutimika tangu tarehe 18 Mei 2022 kufuatana na mkutano wa tarehe 11 Februari iliyopita ambapo kwa mujibu wa taarifa, Papa Francisko alikuwa ameruhusu Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Vyama vya Kitume "kitivo cha kuidhinisha, kwa hiari yake na kibinafsi, kesi" ya uwezekano huu, "bila upendeleo katika ibara ya 134 §1” ya Sheria ya Kanoni (ambayo inafafanua ni nani kwa kawaida wanapaswa kuzingaziwa kuwa maaskofu na wakuu wa mashirika.)
Kwa Maandishi ya kipapa yaliyochapishwa tarehe 18 Mei 2022 yana vifungu 4 vinavyothibitisha viwango mbalimbali vya uidhinishaji ambavyo lazima vipokee uteuzi wa mwanashirika ambaye sio Padre ili aweza kuwa Mkuu wa kuongoza Taasisi, awe ameteuliwa kama mkuu wa eneo au mkuu kabisa , au aliyechaguliwa kuwa msimamizi. Hata hivyo, kimsingi inabaki kuwa ni Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mashirika ya Kitawa na Vyama vya Kazi za kitume ambalo kama lilivyoainishwa katika kifungu cha nne linahifadhi haki ya kutathmini kesi ya mtu binafsi na sababu zilizotolewa na Msimamizi Mkuu au Mkutano Mkuu.