Papa akutana na maprofesa wa Chuo Kikuu cha Loyola,Chicago
Na Angella Rwezaula- Vatican.
Papa Francisko amekutana na kikundi cha maprofea wa Chuo Kikuu cha Loyola huko Chicago, nchini Marekani, Ijumaa tarehe 13 Mei 2022 mjini Vatican ambapo hata hivyo alikuwa amefanya mazungumzo ya madaraja kuanzia Kaskazini hadi Kusini mnamo tarehe 24 Februari 2022 na Baba Mtakatifu na wanafunzi kutoka vyuo vikuu 120 vya Amerika Kusini na Marekani.
Pamoja na Katibu wa Tume ya Kipapa ya Amerika Kusini (PCAL), Profesa Emilce Cuda na Ujumbe mzima wa maprofesa wengine kutoka Marekani na Amerika Kusini, watakuwa na mikutano ya kazi mjini Vatican ili kukuza kimataifa mchakato wa sinodi ya chuo kikuu. Pia watatangaza uzinduzi wa kozi mpya za masomo ya mtaala, katika nyanja mbali mbali za kibinadamu na sayansi ngumu, zinazofundishwa kwa pamoja na vyuo vikuu kutoka Kaskazini, Kituo na Kusini Bara la Amerika. Lengo, ambalo linapatana na mafundisho ya papa wa sasa ni kuzalisha michakato ya uhamisho wa teknolojia na ushirikiano wa ujuzi kati sehemu zote mbili za kuhamasisha mageuzi ya ikolojia. Migogoro ya uhamaji, nishati na chakula ni kitovu cha mpango huo ambao unaungwa mkono na Papa Francisko.
Mahojiano na Profesa Peter Jones, Profesa wa Mafunzo ya Kichungaji katika Chuo Kikuu cha Loyola amesema kutoka kwa Papa kuna mpango wa kufanya wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka Amerika yote kushirikiana kwa njia sawa na mchakato unaoendelea wa sinodi. Na kwamba wamefika Roma hasa baada ya mkutano na wanafunzi wao na Papa Francisko walianza kwa haraka mchakato kwa ajili ya wanafunzi wa vyo vikuu kusaidia ushiriki na kusikilizana kwa namna ya kwamba wanaweza kupendekeza au kuzungumza katika mchakato wa Sinodi.
Na Profesa Cuda, aliyeshirikishana nayo katika kuendeleza mpango hu alimpatia taarifa Baba Mtakatifu, na yeye alikuwwa na shauku kubwa na kuamua kuzungumza na wanafunzi jambo ambalo lilitoka mnamo tarehe 24 Februari. Kwa hivyo, kiuhalisia mkutano huu ni mwendelezo wa mkutano huo na una lengo lake la kuendelea na kazi hiyo na kuhamasisha uwezekano zaidi wa wanafunzi kuunganishwa na mchakato wa sinodi ulimwenguni kote.