Papa Francisko:Injili,Ekaristi na uinjilishaji kwa vitendo ni programu ya maisha ya mkristo
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Charles de Foucauld, Marie Rivier na Padre Gabriel Longueville hawa wote watatu ni wa Jimbo la Viviers nchini Ufaransa, ambao Baba Mtakatifu Francisko amewaonesha kama mifano kwa vijana kutoka mji wa Ufaransa, ambao Jumamosi asubuhi tarehe 14 Mei 2022 katika Ukumbi wa Mikutano katika Jumba la Kitume mjini Vatican ambao wamefika kwa ajili kuudhulia maadhisho ya kutangazwa watakatifu hao Dominika 15 Mei 2022. Miongoni mwa wenyeheri ni kuhani aliyekwenda kwenye jangwa la Sahara, kati ya wenyeji wa Watuareg, na mwanzilishi wa Shirika la Uwasilishwaji wa Maria Hekaluni. Padre Longueville, aliyetangazwa mwenyeheri kama mfiadini mnamo 2019, yeye ni rafiki wa zamani wa Papa Francisko kwa wakati alipokuwa akiishi nchini Argentina.
Papa kwa maana hiyo amefafanua juu ya kujikana kwake na umakini kwa maskini zaidi wa parokia ambayo alifanya kazi kama mfano wa mapadre wa nchi yake ya asili. Papa Francisko amebainisha kwamba mfululizo huu wa watakatifu wenyehri na wa baadaye unaonesha wazi urithi wa jimbo la Viviers. Kwa kuwatazama Charles de Foucauld na Marie Rivier, Papa amesisitiza matashi mema anayotawakia vijana hao kwamba leo hii wajifunza kutoka kwa Charles de Foucauld kuwa na uzoefu huo wa Mungu ambao ulimpelekea kuinjilisha kwa uwepo. Njia ya busara ya uinjilishaji, ndiyo, lakini yenye kudai sana, kwa sababu inahitaji ushuhuda wa maisha madhubuti, yaani, kupatana kiukweli na matamanio ya kila mtu anayependwa na Mungu na si katikaa anasa ya muda mfupi au ya haraka na inayoonekana matokeo.
Papa Francisko amewatia moyo vijana hao kuweka maisha yao ya Kikristo kwenye misingi mitatu muhimu ya hali ya kiroho ya Charles de Foucauld: (Évangile, Eucharistie, Évangélisation) yaani “Injili, Ekaristi na uinjilishaji” kwa vitendo hiyo ni programu ya maisha katika shule ya Kristo. Papa amependekeza wajifunze kutafakari mara nyingi juu ya sala ya kuweza kujikabidhi kwa Mungu, iliyochukuliwa kutoka katika maandishi yake hasa wakati wa chaguzi na misalaba ya maisha. Kwa njia hiyo wataweza kuingia katika mienendo ya kiinjili ya Kanisa katika jimbo lao na kuongeza. Na ameongeza wazo fulani kwa vikundi vyote vya skauti ambavyo vimejiweka chini ya ulinzi wa Charles de Foucauld".
Marie Rivier, alikuwa ishara ya upendo wa Mungu kwa watoto wadogo. Papa amezungumzia juu ya Marie Rivier, ambaye shirika lake, limeenea ulimwenguni kote, na linaendelea kujitolea bila kuchoka kwa watoto, vijana na wale waliotengwa. Kutoka kwa mfano wa Marie Rivier, binti wa nchi yao, aliyejitolea katika elimu ya watoto, pamoja na Shirika la Masista wa Uwasilishaji wa Maria lililoanzishwa naye, Papa anawatakia wawe na shauku ya kufungua akili za watoto kwa mambo ya Mungu kwa umakini kwa ajili ya wengine na kuvutiwa na kazi ya uumbaji. Jinsi hii ni muhimu!
Papa anatumaini kwamba bado kutakuwa na wanawake wengi wa hadhi hiyo, wanyenyekevu na wajasiri katika kujulisha upendo wa Mungu kwa watoto wadogo wanaoomba tu kujifunza. Hatimaye, Papa Francisko amewawatakia vijana kuondoka jijini Roma wakiwa na upendo zaidi kwa Kanisa na kwamba maadhimisho hayo Diminika itawapa taswira ya ulimwengu mzima na sura zake nyingi, zote zikimlenga Mwokozi mmoja na matumaini kwamba watakatifu wa baadaye, Marie Rivier na Charles de Foucauld daima watakuwa chanzo cha faraja na maongozo yao ya maisha.