Papa Francisko:Katekesi kuhusu mwanamke jasiri wa Biblia Judith!
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Baba Mtakatifu katika mwendelezo wake wa Katekesi yake. Jumatano tarehe 11 Mei 2022, kwa waamini na mahujaji waliunganika katika uwanja wa Mtakatifu Petro, amezungumzia shujaa mmoja wa kibiblia Gudith. Baba Mtakatifu amesema hitimisho la kitabu ambacho kinachukua jina lake, kama ilivyosoma , kinatoa ufupisho wa sehemu ya mwisho ya maisha ya mwanamke huyo ambaye alitetea Israeli na maadui wake. Judith ni kijana na mwanamke mjane mwenye karama wa kiyahudi ambaye kwa neema ya imani yake, uzuri wake na ujanja wake alikomboa mji wa Betulia na watu wa Yuda dhidi ya shambulio la Olofene, Jenerali wa Nabukadreza adui mkubwa mwenye kiburi na aliyekuwa anamdharau Mungu. Na kwa namna yake ya ujanja wa kutenda Judithi akawa na uwezo wa kuua dikteta ambaye alikuwa dhidi ya nchi yake. Alikuwa jasiri mwanamke huyo lakini alikuwa na imani, Papa ameongeza. Baada ya tukio kubwa ambalo lilimwona akiwa mstari wa mbele Judith alirudi kuishi katika mji wake Betulia mahali ambapo aliweza kuishi uzee wake mzuri hadi miaka 105. Alikuwa amefikia wakati wake wa uzee kama inavyowafikia watu wengi, wakati mwingine baada ya maisha ya kina ya kazi na wakati mwingine baada ya matukio mengi au hata makubwa ya kujitoa. Ushujaa sio tu wa matukio makubwa ambayo yanatokea mbele ya watazamaji, kwa mfano wa ule wa Judith wa kuweza kumuua dikteta, lakini pia ushujaa mara nyingi hunapatikana katika shauku ya upendo kwa sababu ya familia ngumu na kwa sababu ya kusaidia jumuiya iliyo katika tishio.
Judith aliiishi zaidi ya miaka 100 ambayo ni baraka maalum Papa amesisitiza. Lakini sio adimu leo hii kuwa na miaka mingi ya kuishi baada ya kipindi cha kuwa na pensheni, Je ni jinsi gani ya kuitafsiri, jinsi gani ya kuweza kutoa matunda muda ambao upo? Ikiwa mimi ninastaafu leo hii, na miaka mingi ninaweza kufanya nini, jinsi gani ninaweza kufanya ili nikue kwani umri unakwenda peke yake lakini kukua kimamlaka, kitakatifu na kihekima? Matarajio ya kustaafu yanaendana kwa walio wengi na kile kinachostahili na shauku ya kupumzika na kazi nyingi na ngumu. Lakini hujitokeza hata kwamba mwisho wa kazi inawakilisha kisima cha wasi wasi na subira kwa mtetemeko kidogo wa kujiuliza maswali: je nitafanya nini sasa ambapo maisha yangu yamekuwa matupu kwa kile kilichojazwa sana wakati wote? Swali ndio hilo. Kazi yetu ya kila siku maana yake ni pamoja na uhusiano, kutosheka na kupata kuishi, uzoefu wa kuwa na nafasi, kustahili kuzingatiwa, kipindi chenye ujazo kwenda zaidi yauhaisi wa masaa ya kazi.
Kwa hakika kuna kazi, furaha na ugumu, kutunza wajukuu; leo hii babu na bibi wanalo jukumu kubwa katika familia ili kusaidia na kukuza wajukuu zao; lakini kuna utambuzi vile vile leo hii wa watoto ambao wanazaliwa kidogo na wazazi ambao mara nyingi wanaishi mbali zaidi na wazazi wao, katika hali halisi za kazi na mazingira ya kuishi ambayo hayatoi fursa. Na wakati mwingine kubaki katika kuwakibidhi wazee ili kuelimisha kwa kuruhusu kwamba ni mambo ambayo yanaahusiana sana na kuishi. Papa ametoa mfano mwingine kwamba wengine wanasema kidogo kwa utani kuwa wazee wa leo hii katika hali ya kijamii, kiuchumi, wanakuwa muhimu sana, kwa sababu wanapensheni. Kuna mahitaji mapya hata katika muktadaha wa elimu na ndugu ambao wanatuomba turatibu utamadun wa muungano kati ya kizazi.
Baba Mtakatifu amebainisha kuwa "Lakini, tujiulize: je, tunafanya jitihada hii ya kurekebisha upya? Au tunateseka tu kutokana na hali ya nyenzo na kiuchumi? Kuishi pamoja kwa muda mrefu, kiukweli, kunaongezeka. Je, sisi sote tunajaribu kuwafanya kuwa wanadamu zaidi, wenye upendo zaidi, wenye haki zaidi, katika hali mpya za jamii za kisasa? Kwa ajili ya babu na bibi, sehemu muhimu ya wito wao ni kusaidia watoto wao katika kulea wajukuu. Watoto wadogo hujifunza nguvu ya huruma na heshima kwa udhaifu. Haya ni masomo yasiyoweza kubadilishwa, ambayo kwa babu na bibi ni rahisi kutoa na kupokelewa. Wazee kwa upande wao, hujifunza kwamba huruma na udhaifu sio tu dalili za kupungua: kwa vijana, ni hatua zinazofanya mtu wa baadaye. Judithi alibaki mjane mapema sana na hakuwa na watoto, lakini akiwa mzee alikuwa na uwezo wa kuishi kipindi kikamilifu na cha utulivu, kwa utambuzi wa kuwa aliishi hadi mwisho utume wake ambao Bwana alikuwa amemkabidhi. Kwake yeye ni kipindi cha urithi mzuri wa hekima, wa huruma, wa zawadi kwa ajili ya familia na jumuiya: Urithi wa wema na sio wa mali tu. “ Wanapofikiria urithi, wakati mwingine wanafikiria mali na sio wema ambao aliufanya katika uzee na ambao alipanda, wema ule ambao ndiyo bora zaidi ya urithi ambao unaweza kuachwa”.
Kwa hakika katika uzee wake, Judith aliwezesha uhuru wake na urithi kwa mjakazi wake aliyekuwa anampenda. Hii ni ishara ya mtazamo wa umakini na ubinadamu mbele ya yule aliyekaa naye karibu. Mjakazi huyo alikuwa amemsindikiza katika kipindi chote cha matukio ya kuweza kushinda dikteta na kumuua. Ukiwa mzee Papa amesema unapoteza kidogo kuona, lakini si kupoteza mtazamo wa ndani unaopenyeza kwa kina, na kutazama kwa moyo. Hali hiyo inageuka kuwa na uwezo wa kuona mambo ambayo mwanzo yalikuwa yakipotea au hayaonekani. Na ndiyo hivyo, Bwana hakabidhi talanta kwa vijana tu na wenye nguvu, na yeye anazo za wote, kwa kiwango cha kila mtu. Maisha ya Jumuiya zetu lazima yatambue kufurahishwa na talanta na karama za wazee wengi ambao katika orodha tayari wako pensheni , lakini ambao ni utajiri wa kuthamanisha.
Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa hii inahitaji kwa upande wa wazee wenyewe, umakini bunifu na uwezekano mpya mkarimu. Uwezo wa awali wa maisha hai, unapoteza sehemu yake ya ujenzi na kugeuka kuwa rasilimali za kutoa, kufundisha , kufikiria, kujenga, kutibu na kusikiliza … Kupendeleawale wasio na fursa , ambao hawawezi kujimudu au waliotupwa katika upweke wao. Judith alimkomboa mjakazi wake akiwa amejazwa na umakini wa wote. Akiwa kijana alikuwa amepata kupongezwa na jumuiya kwa ujasiri wake. Kwa uzee wake alistahili kwasababu ya huruma ambayo ilitajirisha uhuru na matokeo. Judith wmwenye pensheni hakuishi kwa kujutia ujana wake, bali ni mzee mwenye ari na shauku ambaye anajaza zawadi kwa wakati wa mungu anaompatia. Kwa kuhitimisha Papa Francisko ametoa mwaliko wa kuchukua biblia na na kusoma kitabu cha Judith, na kwamba ni kidogo, na kinasomeka kwa urahisi. Ni kama sura kumi au zaidi. “Someni historia hii ya mwanamke jasiri ambaye anaishia hivi, kwa upole, kwa ukarimu, mwanamke hadi kiwango. Na kwa hivyo natamani wangekuwa bibi zetu. Yote kama haya: jasiri, wenye busara na kwamba wanatuachia urithi sio wa pesa, lakini urithi wa hekima, uliopandwa ndani ya mioyo ya wajukuu wao”.