Tafuta

2022.05.21 Papa amekitana na Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Ndugu wa Shule za Kikristo 2022.05.21 Papa amekitana na Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Ndugu wa Shule za Kikristo  

Papa Francisko:kufanya kazi pamoja kujenga mkataba wa kielimu

Udugu na kutunza nyumba ya pamoja ndiyo changamoto za dharura katika elimu ambayo ulimwengu leo hii unaishi ambapo imezidiwa na matokeo ya janga.Amebainisha hayo Papa Francisko alipokutana na Shirika la Ndugu wa Shule za Kikristo wakiwa katika fursa ya Mkutano Mkuu wao kwa kuongozwa na mada:“ Kujenga njia mpya kwa ajili ya kupyaisha maisha mapya.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 21 Mei 2022, amekutana na Shirika la Kilei la Ndugu wa Shule za Kikristo ambao walikuwa katika fursa ya Mkutano Mkuu wa Shirika hilo lililoundwa mnamo 1681 huko  Reims na Mtakatifu Yohane Mbatizaji  wa La Salle.   Shule ni kama mahali pa ujenzi wa kujenga barabara mpya zinazoelekea kwa ndugu, hasa walio maskini zaidi kama vile kufanya  kozi za elimu katika shule, vyuo, vyuo vikuu kwa takriban katika nchi mia moja ambako Ndugu wa Shule za Kikristo wapo ulimwenguni. Katika hotuba yake Papa Francisko amesema kazi ya elimu ni zawadi kubwa kwa yule anayeitimiza. Ni kazi ambayo inadai sana, tena ya kutoa sana.  Papa hata hivyo amelalamika  kwamba Mkataba wa elimu umevunjwa. Umevunjika kwa maana  Serikali, waelimishaji na familia sasa wametengana. Kwa maana hiyo ni “Lazima tutafute mapatano mapya ambayo ni mawasiliano na kufanya kazi pamoja: na ndiyo dharura ya kielimu”.

Changamoto mbili za elimu

Mtazamo wa Papa Francisko unamulika  dharura ya kielimu inayopatikana leo hii  katika kiwango cha kimataifa na kufanywa kuwa mbaya zaidi na matokeo ya janga la uviko. Kwa hiyo ameonesha changamoto mbili kwa takriban washiriki mia moja katika mkutano huo kwamba hao  ni udugu na kutunza nyumba ya pamoja.   Papa amewaeleza kwamba hao Shirika la Ndugu,  tayari ni sehemu ya eneo hilo la ujenzi, kwa hakika, wao wako mstari wa mbele, wakielimisha kutoka katika ulimwengu uliofungwa hadi ulimwengu ulio wazi; kutoka kwa utamaduni wa kutupa hadi utamaduni wa utunzaji; kuanzia kutafuta maslahi ya washiriki hadi kutafuta manufaa ya wote. Kama waelimishaji wanajua vyema kwamba mabadiliko haya lazima yaanzie kutoka katika dhamiri, au yatakuwa sura ya usoni tu.

Agano la elimu, katika shule ya Kristo

Kwa mujibu wa Papa Francisko, hiyo ni kazi ambayo haifanyiki peke yake, lakini katika ushirikiano wa kielimu na familia, jumuiya na makundi ya watu, hali halisi ya eneo. Zaidi ya hayo, watenda kazi wema Papa Francisko ameonya tena  kwamba  hawawezi kujisahau wenyewe: Mwalimu wa Kikristo, katika shule ya Kristo, juu ya yote ni shuhuda, na ni mwalimu kwa kiwango ambacho yeye ni shuhuda. Kwa maana hiyo amethibitisha kwamba katika hilo yeye hana la kuwafundisha ila tu kama ndugu, ametaka awakumbushe jambo hilo. Na zaidi ya yote amewaombea wapate kuwa ndugu, si kwa jina tu, bali wa kweli. Na ili shule zao ziwe za Kikristo sio kwa jina, lakini za kweli.

Kuinjilisha kwa kuelimisha, kuelimisha kwa kuinjilisha

Mwaliko wa Papa Francisko kwa Ndugu hao ni kwenda mbele kwa furaha: kuinjilisha kwa kuelimisha na kuelimisha kwa kuinjilisha. Kujenga barabara mpya, kwa kufahamu kwamba barabara mpya inakuwa ya kweli kweli, Njia, ni Yesu Kristo. Ni kwa kumfuata tu, ameongeza kusema Fransisko, maisha hubadilika na nasi tunakuwa chachu, chumvi na mwanga.

Kufanya kukuza mwanadamu

Kuelimisha katika ubunifu, kuishi pamoja, haki, amani, maisha ya ndani, uwazi kwa apitaye maumbile, kwa maana ya kustaajabisha na kutafakari mbele ya fumbo la maisha na uumbaji, hatimaye amewakumbusha Papa Francisko, Ndugu wa Shule za Kikristo, wenye nguvu ya mapokeo tajiri ya kielimu, wanaishi na kufasiri utume wao katika Kristo, wakitafsiri katika utimilifu wa ubinadamu kwa sababu, kama alivyokuwa akisema  Mtakatifu Yohane  Paulo II kwamba “Mtu na njia ya Kanisa”. Ni utume wao, Uhusiano wao katika uinjilishaji ni katika kumfanya mwanadamu akue sawa sawa na Kristo. Kwa maana hiyo, “shule zao ni za Kikristo, na sio kwa sababu ya lebo ya nje”.

21 May 2022, 17:20