Tafuta

2022.05.28 Kamati ya Kipapa ya Kisayansi za Kihistoria 2022.05.28 Kamati ya Kipapa ya Kisayansi za Kihistoria 

Papa Francisko kwa Kamati ya Kipapa ya Sayansi za kihistoria

Ni matarajio ya Papa kwamba wanahistoria watachangia kwa tafiti zao na kutoa matokeo ya mwendelezo unaojikita na masuala ya mwanadamu na kwa ujasiri kuanzisha michakato ya kukabiliana na kwa dhati katika historia za watu na kwa mataifa.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko Jumamosi tarehe 28 Mei 2022 amekutana na wajumbe wa Kamati ya Kipapa ya Sayansi za Kihistoria wakiwa katika fursa ya Mkutano wao Mkuu. Amemshukuru Mwenyekiti wao kwa maneno yake na shughuli yao ya ukarimu kwa huduma ya Vatican. Papa amesema kuwa ni mchango wa thamani hata kwa namna ambayo wanautoa, kuzungumza, na kushirikishana na wanahistoria na taasisi za kielimu ambao wanapendelea kujifunza sio tu historia ya Kanisa, lakini pia kwa kupanua historia ya mwanadamu na katika uhusiano na Ukristo wa muda mrefu kwa milenia mbili.

Mwaliko wa Kanisa kujiweka katika usikivu wa ulimwengu

Miaka mia moja mnamo iliyoyopita yaani tarehe 6 Februari 1922,  Pio XI , Papa mwana maktaba na Mwanadiplomasia, alitoa kwa Kanisa na katika jamii ya kiraia mwelekeo stahiki kwa njia ya ishara hakika ya kushangaza. Mara baada ya kuchaguliwa kwake Papa Ratti alipenda kuzindua Upapa wake kwa kuchungulia kupitia balkoni ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Katika ishara hiyo ameongeza kusema, Pio XI alikuwa akiwaalika kutazama ulimwengu na kujiweka katika usikivu na huduma kwa jamii ya wakati wetu.

Kuchangia tafiti katika masuala ya mwanadamu

Papa Francisko amesema kamati yao iliyoundwa na Mwenyeheri Pio XII, kwa ajili ya huduma ya Papa,  Vatican na makanisa mahalia kwa hakika wanazingatia kuhamasisha mafunzo ya historia, uwajibikaji wa maabara ya amani ambayo njia ni mazungumzo na kutafuta suluhishi za dhati, ili kujua kwa kina mtu na jamii. Ni matarajio ya Papa kwamba wanahistoria watachangia kwa tafiti zao na kutoa matokeo ya mwendelezo unaojikita na masuala ya mwanadamu, na kwa ujasiri kuanzisha michakoto ya kukabiliana na kwa dhati katika historia za watu na kwa mataifa.

Hali halisi ya Ulaya Mashariki

Papa Francisko amerudia kutazama hali halisi ya Ulaya mashariki ambayo haikuwezakana kukutana na baadhi yao waliozoea kuwa nao katika muktadha wa mikutano yao kwa makumi ya miaka ambapo wameona wakishirikiana na wataalamu wa elimu, wanasayansi wa Moscow, Urussi, wanahistoria wa Upatriaki wa Moscow. Lakini ana uhakika kwamba watajua namna ya kupokea fursa hyokwa ajili ya kuanza kwa upya na kusisitisha kazi yao ya pamoja na kutakuwa na mchango wa thamani kusaidia amani.

HOTUBA YA PAPA KWA KAMATI YA KIPAPA YA SAYANSI ZA KIHISTORIA
28 May 2022, 14:57