Tafuta

Papa:Mungu haogopi maombi yetu ya kupinga,kwani anaelewa&anajibu!

Katika Katekesi ya Papa Francisko kwa waamini na mahujaji,ni mwendelezo wa mada ya Uzee ambapo ametafakari sura ya Ayubu.Baada ya kupoteza kila kitu na kupinga dhidi ya Mungu,alitambua kuwa Bwana si mtesaji bali ni Baba mpole ambaye atamtendea haki.Papa amesema huu unaweza kuwa mfano maalum katika wakati huu ambapo janga na vita vinakusanya mizigo na mateso.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika kuendeleza  katekesi yake juu ya 'Uzee', Jumatato tarehe 18 Mei 2022, kwa waamini na  mahujaji kutoka sehemu mbali mbali za dunia, waliounganika katika uwanja wa Mtakatifu Petro, Vatican, ametafakari kuhusu sura nyingine ya kibiblia ya Ayubu (Ay 42,1-6.12.16).  Akianza Papa amesema: "somo lililosikika linafunga kitabu cha Ayubu, ambacho ni kipeo cha fasihi ya ulimwengu wote. Ni kukutana na Ayubu katika mchakato wa Katekesi kuhusu uzee na tunakutana naye kama shuhuda wa imani, ambayo haikubali 'ukaragosi' kwa Mungu, bali inapaza kelele kupinga kwake mbele ya mabaya, mpaka Mungu ajibu na kufunua uso wake. Na Mungu hatimaye anajibu na daima kwa namna ya kushangaza, na anafanya hivyo daima kwa upole. Ni lazima kusoma vizuri, sura hiyo ya kitabu, bila hukumu,ili kuweza kupata nguvu ya kilio cha Ayubu".

Katekesi ya Papa 18 Mei 2022
Katekesi ya Papa 18 Mei 2022

Kwa kufanya hivyo Baba Mtakatifu  Francisko amesema itawafanya kujiweka katika darasa, ili kushinda vishawishi vya udini mbele ya hasira na kukata tamaa kwa uchungu kwa kupoteza kila kitu. Amekumbusha jinsi ambavyo hitimisho la kitabu hicho wote wnakumbuka historia, kwani Ayubu alipoteza kila kitu katika maisha, alipotea utajiri, familia, watoto, hata afya akabaki na majeraha, akizungumza na marafiki  watatu, na wa nne ambaye alikuja kumsalimia. Hitimisho la kitabu ambapo Mungu anatoa neno, katika majadiliano ya Ayubu na marafiki zake ni kama njia ya kuweza kufikia wakati ambao Mungu anatoa neno lake. Ayubu anasifiwa kwa kuelewa fumbo la huruma ya Mungu iliyofichwa nyuma ya ukimya wake. Mungu anawakemea marafiki wa Ayubu ambao walidhani kujua kila kitu, kujua kuhusu Mungu na kuhusu maumivu, na baada ya kuja kumfariji Ayubu, waliishia kumhukumu kwa mbinu zao zilizowekwa hapo awali. Papa Francisko ameomba kwamba Mungu atuepushe na utauwa huu wa kinafiki na kimbelembele! Mungu atuepushe na huo udini wa kimaadili na ule udini wa kanuni unaotupa dhana fulani na kukupeleka kwenye Ufarisayo na unafiki.

Katekesi ya Papa 18 Mei 2022
Katekesi ya Papa 18 Mei 2022

Tazama jinsi ambavyo Bwana anajieleza mbele yao, Baba Mtakatifu ameongeza  kwamba Bwana anasema: “Hasira yangu inawaka juu yako [...], kwa sababu hukusema mambo ya haki kunihusu kama mtumishi wangu Ayubu”, Ndivyo anasema Bwana kwa marafiki wa Ayubu, “Mtumishi wangu Ayubu atawaombea ninyi, ili mimi, kwa kumjali, nisiadhibu kwa upumbavu wenu, kwa sababu hamkusema mambo ya haki juu yangu kama mtumishi wangu Ayubu” (Ayubu42:7-8). Tamko la Mungu linatushangaza,  kwa sababu tumesoma kurasa zinazowaka moto za upinzani wa Ayubu, ambazo zimetuacha tukiwa na huzuni. Hata hivyo, Bwana anasema "Ayubu alisema vizuri, hata alipokuwa na hasira na hata hasira dhidi ya Mungu, lakini alisema vizuri, kwa sababu alikataa kukubali kwamba Mungu ni "Mtesi". Mungu ni kitu kingine. Hii  nii nini? Alikuwa akimtafuta. Na kama thawabu, Mungu anamrudishia Ayubu maradufu ya mali zake zote, baada ya kumwomba awaombee marafiki zake hao wabaya.

Katekesi ya Papa 18 Mei 2022
Katekesi ya Papa 18 Mei 2022

Huu ndio wakati mzuri wa uongofu wa imani ambao unakuja kwa dhati mwishoni mwa malalamiko ya Ayubu, mahali anaposema: “Ninajua kuwa Mlipiza kisasi wangu yuko hai na kwamba, hatimaye, atapanda mavumbini! Baada ya ngozi yangu hii kuharibiwa, bila mwili wangu, nitamwona Mungu. Nitamwona, mimi mwenyewe, na macho yangu yatamtazama, si kama mgeni "(19,25-27). Hatua hii ni nzuri Papa amesisitiza. Vile vile Papa amekumbuka mwisho wa wimbo wa gwiji mmjoa mtunzi wa muziki  Handel kuhusu Masiha baada ya tamasha la Aleluya, sauti moja ya juu uimba kuwa:  “Ninajua kuwa Mkombozi wangu yu hai”, kwa amani”. Na kwa hivyo, baada ya jambo hilo lote la uchungu na furaha ya Ayubu, sauti ya Bwana ni kitu kingine. “Ninajua kuwa Mkombozi wangu yu hai”:hili  ni jambo zuri. Tunaweza kurudia hivyo: “Mungu wangu, najua ya kuwa Wewe si Mtesaji. Mungu wangu atakuja na kunitendea haki”. Ni imani rahisi katika ufufuko wa Mungu, imani rahisi katika Yesu Kristo, imani rahisi kwamba Bwana daima anatungoja na atakuja”.

Katekesi ya Papa 18 Mei 2022
Katekesi ya Papa 18 Mei 2022

Kimya cha Mungu, katika dakika ya kwanza ya tukio, kinamaanisha hili. Mungu hataepuka makabiliano, lakini mwanzoni anamwachia Ayubu katika chanzo cha malalamiko yake, na Mungu anasikiliza. Pengine, nyakati fulani, tunapaswa kujifunza heshima hii na huruma hii kutoka kwa Mungu. Papa ameshauri. Na Mungu hapendi ensaiklopidia hiyo ya maelezo, ya kutafakari ambayo marafiki wa Ayubu walifanya. Hiyo ni juisi ya ulimi, ambayo si sawa: ni udini huo unaoelezea kila kitu, lakini moyo unabaki baridi. Mungu hapendi hivyo. Zaidi anapenda kama kupinga kwa Ayubu au ukimya wa Ayubu. Kukiti  imani ya Ayubu, ambayo inajitokeza katika wito wake wa kuendelea kwa Mungu una haki kuu, na kutimizwa mwishoni mwa uzoefu wake karibu wa kifumbo ambao yeye anasema: “nilikujua kwa kwa uvumi, lakini sasa macho yangu yanakuona» (42,5).Ni watu wangapi, ni wangapi kati yetu baada ya hali mbaya kwa kiasi fulani, isiyoeleweka, tunajitoa na kumjua Mungu kuliko hapo awali! Na tunaweza kusema, kama Ayubu, nilikujua kidogo kwa kumbukumbu, au kwa uvumi, lakini sasa nimekuona, kwa sababu nimekutana nawe”. Kwa mujibu wa Papa Francisko amesema ushuhuda huu unaaminika hasa ikiwa uzee unabeba mzigo wenyewe katika udhaifu na kupoteza kunakoendelea. Wazee wameona mengi sana katika maisha yao! Na pia waliona kutofautiana kwa ahadi za watu, Watu wa sheria, watu wa sayansi, hata watu wa dini, ambao huchanganya mtesaji na muathirikaa, wakihusisha waathirika jukumu kamili la maumivu yao wenyewe. japokuwa wanakosea!

KATEKESI YA PAPA 18 MEI 2022
18 May 2022, 11:20