2022.05.28 Papa akutana na  Cursillos ya Kikristo Italia. 2022.05.28 Papa akutana na Cursillos ya Kikristo Italia. 

Papa Francisko:Pyaisheni uchaguzi wa viongozi,harakati nyingi zinakufa

Papa amekutana na washiriki wa Ultreya Kitaifa wa Cursillos ya Kikristo.Amehimiza umoja na ukaribu,kutangaza na kushuhudia injili ya maisha.Ametoa ushauri juu ya upyaishaji wa viongozi katika jumuiya zao.“Tuna uzoefu mwingi katika Kanisa.Kwa hivyo ni muhimu kupyaisha huduma ya mamlaka,kwa kuifanya iwe mpya:hakuna mtu aliye na mamlaka ya milele”.

Na Angella Rwezaula- Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 28 Mei 2022, amekutana na washiriki wa Harakati ya Cursillos ya Kikristo Italia wakiwa na Maakofu na mapadre waliowasindikiza kuja Roma kwa ajili ya Mkutano wao VII wa Ultreya Kitaifa. Papa amesema kwamba kwa kawaida wao wanatumia salamu ya mahujaji wa kizamani isemayop Ultreya, ikiwa na maana ya kukutana, ambapo tangu mwanzo wake umekuwa na tabia ya karama ya kuishi misingi ya kikristo.  Ni wakati mzuri wa mkutano, wa kutangaza ushuhuda na sala, kwa akili ya kushauriana kwa pamoja ili kwenda mbali na zaidi. Huu ni muungano uliondaliwa na sio baraza la utawala wa kampuni, lakini ni umoja wa kidungu ili kukutana kwa ari na shauku ya imani ambayo wote wanafanya uzoefu tangu mwanzo wa kuanza Cursillo ambapo walishiriki na ambao walitoa maisha yao.

Papa akutana na Cursillos ya Kikristo Italia
Papa akutana na Cursillos ya Kikristo Italia

Baba Mtakatifu Francisko akitazama shughuli zao za kila juma hasa zaidi ya mikutano yao katika Ultreya, ambayo inawasukuma zaidi, amewaelekeza mambo msingi kwa ajili ya kwenda kwao mbele ya upeo. Awali ya yote ni kwenda kuelekea umoja. Hii inahusu kwenda zaidi ya binafsi na zaidi ya kikundi binafsi ili kufanya jumuiya na kukua katika Kanisa ambalo daima ni mwili mmoja na kamwe visivyotengana. Kwa maana hiyo kamwe kwasijifungia binafasi badala yake wadumishe umoja  katika maeneo yao mahali walipofungamana.

Papa akutana na Cursillos ya Kikristo Italia
Papa akutana na Cursillos ya Kikristo Italia

Pili baba Mtakatifu amesema wao wameitwa kufanya jumuiya kwa harakati nzima ya Cursillo. Chamoto kubwa ni ile ya kuhifadhi roho ya upendo na umoja kwa kutambua kuwa karama ya mwanzilishi wa harakati ni ile ambayo aliwaonesha tangu kuanza na tangu kizazi cha kwanza , wao wanaitwa sawa sawa kuwa wawajibikaji. Umoja hausimiki juu ya karama ya ubinafsi, au juu ya tasaufi ya matukio ya kisasa. “Umoja unasimika mzizi katika urithi wa tasaufi inayokubalika kwa wote, kuiishi na kuishirikishwa kwa wote, pamoja na wote na kwa ajili ya wote”. Papa Francisko anatambua jinsi ambavyo siku zijazo watafanya Mkutano wa kimatifa wa Cursillos de Cristiandad, (Wacursillo Wakristo), ambao utaona ushiriki wa viongozu wote wa mabara yote.

Papa akutana na Cursillos ya Kikristo Italia
Papa akutana na Cursillos ya Kikristo Italia

Ni matashi mema ya Papa kwamba mkutano huo uweze kuiishi kama tukio la sinodi ya kusikiliza na kufanya mang’amuzi ya pamoja kati ya wahusika na kutoa nafasi kwa wote na kukaribisha maono kwa kutafuta maelewano ya kiroho ya ndani mwao.  Ushauri wa tatu, Baba Mtakatifu  amependa kuwambia ukaribu na kwamba huo ni mpana zaidi kwani unahitaji kufanya Jumuiya na Kanisa ambalo linajikita na ukaribu, na kusikiliza wachungaji na ushiriki wa mipango ya kuchungaji kwa Makanisa mahalia wanakoishi. Makundi yao na harakari zao, hayao karibu na Kanisa lakini haiyo i sehemu ya kanisa ambalo linaishi katika eneo hilo. Kwa maana hiyo wao wanaitiwa kujitambusha na kuhisi ndani kabisa na kutenda na Kanisa n asio nje ya Kanisa.

Kujua kutangaza upendo wa kikristo

Baba Mtakatifu Francisko ametoa mwelekeo msingi ambao ni utume. Hata harakati yao inajikuta mbele ya changamoto ya kuunda jumuiya ya mitume wamisionari wanaokwenda mbali kukutana, na  kushinda mantiki za kusema ‘daima imefanyika namna hii’. Wao na karama yao iliyowapelekea kujiunda na kujua kutangaza kwa namna moja rahisi na ya moja kwa moja ya uzoefu wa kikristo yaani upendo wa Mungu kwa kila mwanaume na mwanamke. Na wao wanajua jinsi ya kuwasilisha tangazo hilo ndani ya vifungo vya urafiki na ukaribu unaouanzisha, bila kulazimisha, na watu wengi unaokutana nao, hata wale walio na misimamo mikali zaidi na ambao wanaonekana kutojali au hata kuchukia imani. Papa amewatia moyo, kwa hiyo, kujiruhusu kuhuishwa na karama hiyo ambayo Roho Mtakatifu amewajalia, kupata furaha ya kueneza injili, katika nyanja zote za maisha, faraghani na hadharani.

Epuka mamlaka ya milele. Harakati nyingi zimekufa

“Ningependa kuongeza jambo moja: kuwa katika harakati pia ina maana ya kuishi huduma ya matangazo ya Kikristo na ushuhuda, na hii pia inawatazama watu wanaohusika au kuwajibika kwa kila nchi au kwa harakati nzima. Jambo baya ambalo lazima liuepukwe, kabla halijatokea, kwa sababu inaonekana kwamba halijatokea, lakini nawaambia kwanza: “kujiwekea mamlaka ya milele, kwamba daima ni yule yule. Tafadhali hapana. Kila mtu ni mzuri, lakini sio wote ni wa lazima”.

Papa akutana na Cursillos ya Kikristo Italia
Papa akutana na Cursillos ya Kikristo Italia

 “Sisi sio wa lazima. Ninamalizia na kazi ya Mratibu  kwa kuwa  sijui mnamwitwa nani awe wa kundi, wa nchi au Mkuu, ninarudi nyumbani, ninaingia kundini kama yeyote yule. Hapana, lakini nilifanya hivi, sasa ni juu ...”. Haigusi chochote, ni zamu yako kwenda nyumbani! Inaeleweka? Ni na upyaisho huu dhidi ya matamanio ya kibinafsi, ambayo shetani anafanya kuhama, ni kazi ya kuendelea kuishi. Kwa sababu harakati nyingi zimekufa kutokana na kukaa kwenye mikono ya kiongozi mmoja hasiyebadilishwa. Tuna uzoefu mwingi katika Kanisa. Kwa hivyo, kupyaisha huduma ya mamlaka, kwa kuifanya upya: hakuna mtu aliye na mamlaka ya milele.

HOTUBA YA PAPA KWA HARAKATI YA KIKRISTO ITALIA
28 May 2022, 14:38