Papa Francisko:Siasa ni mkutano,tafakari na matendo,sio uadui!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Jumatatu tarehe 16 Mei 2022 amekutana na Udugu Kisiasa wa Jumuiya ya ‘Chemin Neuf’. Hawa ni pamoja na Wanaume na wanawake, wanandoa watawa na waseja, wanaoishi katika maeneo mbali mbali kati ya lugha na tamaduni zote, Wakristo wa maungamo tofauti, Wakatoliki, Waorthodox, Waprotestanti, Wainjili wote kwa pamoja. Papa Papa Francisko katika hotuba yake amewakumbusha, jinsi ambavyo akikutana nao mwaka jana walimwomba awaombee kwa ajili ya ushiriki wa Mkutano wao uliokuwa unaongozwa na mada:“Changemakers, “Waleta mabadiliko” huko Budapest. Kwa maana hiyo walikutana na wakawa na mafunzo lakini hata kwa matendo, katika vyama mahalia. Namna walivyokuwa wameishi tukio hilo, Papa amesema ilikuwa na maana ya kweli ya kila ambacho ni siasa hasa kwa wakristo. Siasa ni mkutano, tafakari na matendo.
Papa akifafanua amesema: Siaa awali ya yote ni sanaa ya kukutana, kwa hakika katika mkutano huo wanaishi kwa kumkaribisha mwengine na kukubali tofauti yake, katika mazungumzo ya heshima. Kama Wakristo hata hivyo kuna kitu cha zaidi ambcho lazima kionekana hasa Injili inavyotaka kumpenda hata adui ( Mk 5, 44), na kwa maana haiwezekani kufurahia mazungumzo ya kijuu juu ya kawaida kama vile mchakato mara nyingi wa vizingiti kati ya vyama vya kisiasa. Kama wakristo wanaitwa kuishi mkutano kisiasa kama mkutano wa kidugu hasa kwa wale ambao hawakubaliani na mawazo ya; na maana yake kuonekana na wote ambaye tunazungumza kama ndugu wa kweli mwana aliyependwa na Mungu. Sanaa hiyo ya mkutano inaanza kwa maana hiyo ya kubadilishana mtazamo juu ya mwingine , kumkaribisha, na kuheshimu bila hali kutazama hali ya mtu. Ikiwa mabadilishano hayo ya moyo hajali, siasa hiyo ina hatari ya kubadilika kuwa mara nyingi vurugu kwa sababu ya kutaka kishinda mawazo binafsi, kwa kutafuta mafao maalum zaidi ya wema wa pamoja, dhidi ya misingi ya umoja unaoshinda migogoro ( Evangelii gaudium, 226-230).
Siasa hata ni matendo. Papa amefurahi kwamba Udugu wao haufurahii kuwa nafasi moja ya majadiliano na mabadilishano tu, lakini ambayo inawapelekea hata katika jitihada za dhati. Kama wakristo Papa amesema “tunahitaji kuaukabiliana daima mawazo yetu kwa nguvu ya uhalisia, ikiwa hatutaki kujenga juu ya mchanga ambapo mapema au baadaye inaishia kuanguka.” Papa amewaomba wasisahau kuwa uhalisia ni msingi wa mawazo ( Evangelii gaudium, 231-233). Kwa maana hiyo amewatia moyo jitihasìda kwa ajili ya wahamiaji na ikolojia. Papa ameelezwa kwamba badhi yao wanaishi katikati ya mitaa ya watu huko Paris ili kusikiliza maskini na ndiyo mtindo wa kikristo wa kufanya siasa. Mkutano, tafakari, matendo ndiyo mpango wa siasa kwa maana ya kikristo. Papa amefikiria kwamba wao wanafanya uzoefu huo, hasa kwa mikutano yao ya kila dominika jioni, ni kusali pamoja kwa Baba ambaye anatangulizwa kwa yote na kumwiga Yesu Kristo kwa kujiweka katika usikivu wa Roho Mtakatifu ambaye anatunza wema wa pamoja na kuweza kutapa nguvu za ndani ambazo ni msingi na za kutoa chachu.
“Msisahau misingi hii kwamba ukweli ni muhimu zaidi kuliko wazo: huwezi kufanya siasa na itikadi. Yote ni bora kuliko sehemu, na umoja ni bora kuliko migogoro", Papa amewasahuri. "Daima kutafuta umoja na msipotee katika migogoro”, Papa amewaonya. Papa Francisko amesisitiza kwamba haiwezekani maisha bila ari na mshangao, Mshangao ni ule unaokufanya kuhisi kuwa niko na Yesu na katika Yesu. Mshangao wa kuona ukuu wa Bwana, ukuu wa Nafsi yake, ukuu wa mpango wake, wa kuhisi ukuu wa Heri kama mpango wa maisha. Na badaye neno lingine ni kumbukumbu. Kwa njia hiyo kumbukumbu, tumaini, mshangao ni mambo matatu msingi ya kujikita nayo katika Jumuiya yao! "Yaliyopita, yajayo na ya sasa: hakuna wakati ujao bila ya sasa, na hakuna tumaini bila mshangao. Kuzeni sala kwa Injili ili kuhisi mshangao wa kukutana na Yesu Kristo. Na kwa sababu ya kufanya zoezi la kisiasa kama mtindo ulio mkuu wa upendo kama alivyokuwa akifafanua Papa Pio XI." Baba Mtakatifu anawasindikizwa kwa sala. Amewabariki na kuwaomba wasisahau kusali kwa ajili yake. Lakini baadye ameomba kusali kwa Bwana pamoja naye: “Bwana Yesu, utubariki sisi sote tunaofanya kazi karibu nawe. Bariki mawazo yetu, bariki mioyo yetu, bariki mikono yetu. Amina"