Papa Francisko:Tangu vita ya pili,vimeendelea vile vya kikanda
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Ijumaa tarehe 6 Mei 2022, amekutana na Washiriki wa Mkutano wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa Kikristo ambapo katika kuanza hotuba yake amewashukuru kwa moyo na Kardinali Kurt Koch kwa maneno yake kwa niaba ya wajumbe, washauri na wahudumu wa Baraza hilo. Wamefika hapo wakiwa wamehitimisha Mkutano wao ambao na hatimaye mwaka huu imewezakana kuufanya kwa sababu ulikuwa umehairishwa kutokana na janga la uviko. Janga hili kwa hakika limekuwa na muktadha mkubwa wa maisha ya kijamii kwa ulimwengu mzima na kufanya kurodora hata shughuli za kiekumenae kwa kuzuia kutimiza kwa miaka wawasiliano na mipango ya kawaida, amesema Papa. Na wakati huo hu lakini mgogoro wa kiafya umekuwa hata fursa kwa ajili ya kuongeza na kupyaisha uhusiano kati ya wakristo. Baba Mtakatifu amesema, matokeo ya kwanza ya kiekuemene katika janga yamekuwa kupyaisha utambuzi kuwa sisi sote ni familia moja ya kikristo, utambuzi ambao umekita mizizi ya uzoefu wa kushirikishana udhaifu sawa na uwezo wa kutegemea msaada kutoka kwa Mungu tu.
Sambaba na hilo janga lilolazimisha kuhifadhi umbali kati ya mmoja na mwingine, limefanya kutambua ni kwa jinsi gani kuna haja ya kuwa na ukaribu wa mmoja na mwingine na ambavyo tunawajibika kwa mmoja na mwingine. Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa ni muhimu kuendelea kukuza utambuzi huu na kuendeleza mipango ya wazi na kukuza hisia za kidugu. “Na juu ya hili, ningependa kusisitiza: leo haiwezekani kwa Mkristo, sio hivyo (anasema: “nafaa”), kwenda peke yake na imani yake. Ama twende pamoja, madhehebu yote ya kindugu, au hatutembei. Leo hii ufahamu wa uekumene ni kwamba haiwezekani kufikiria kuendelea na safari ya imani bila usindikizwaji wa kaka na dada wa makanisa mengine au jumuiya za kikanisa. Na hili ni jambo kubwa. Pekee haiwezekani kamwe. Hatuwezi.”
Ni rahisi kusahau ukweli huu wa kina kwa hakika, Papa ameonya. Kile ambacho kinatokea katika jumuiya za kikristo ni wazi kuona hatari za kujidhani na kujisikia wa kujitosheleza, tabia ambao kiukweli ni vizingiti vya kiekumene. “ Sisi tunaona. Katika baadhi ya Nchi kuna tabia hizi za ubinafsi zilizorudishwa, kwa kusema tu, za baadhi ya Jumuiya za Krikristo ambazo ni kurudi nyuma na kutoweza kusonga mbele. Leo hii, ama sisi sote tutembe pamoja au hatutaweza kutembea. Ni Huu ni ukweli wa dhamiri ya kweli na neema ya Mungu”. Baba Mtakatifu Francisko amerudi katika janga kwamba, kabla hata ya janga la kiafya kuisha, ulimwengu mzima umejikuta unakabiliana na janga jipya la changamoto ya vita vya sasa vinavyoendelea nchini Ukraine. Baada ya vita vya pili vya dunia kiukweli vita vya kikanda, kwa kutoa mfano amefikiria nchini Rwanda miaka 25 iliyopita, kwa kutaja moja lakini pia hata kufikiria Myanmar…. Lakini kwa kuwa ni nchi zilizo mbali, na ambazo hazionekani karibu, basi iliyo ya karibu inawafanya kutenda lolote, lakini vita vya kikanda havikukosekana, Papa amesisitiza.
kamwe haikuisha na ambavyo mara kadhaa, Papa amevifafanua kama vita vya tatu vilivyogawanyika vipande vipande kila sehemu. Licha ya hayo vita hivi, vya kikatili, na vya wazimu kama kila vita, ambavyo vinatishia ulimwengu mzima , haiwezekani kutotoa neno la dhamiri ya kila mkristo na kila Kanisa. Lazima kujiuliza: je wanafanya nini na Kanisa linaweza kufanya nini kwa ajili ya kutoa mchango wa maendeleo ya Jumuiya ulimwenguni, wenye uwezo wa kutimiza udugu kuanzia na watu na mataifa ambayo yanaishi urafiki kijamii? (Fratelli tutti 154). “Hili ni swali moja ambalo tunatakiwa kufikia pamoja”, amesema Papa. Katika karne uliyopita, utambuzi wa kashfa ya migawanyiko kati ya wakristo ilikuwa imeweka uzito wa kihisttoria kwa kuzaa ubaya ambao ulitoa sumu ulimwengu wa maombolezo na ukosefu wa haki ambao ulikuwa umeamsha jumuiya za waamini chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, kuwa na shauku ya umoja ambao Bwana aliuomba na kutoa maisha yake.
Leo hii mbele ya unyama wa vita, umoja huu unapaswa upyaishwe. Kudharau migawanyiko kati ya wakristo kwa ukawaida, au kujiachia, ina maana ya kuvumilia ule uchafuzi wa mioyo ambayo inafanya kuwepo na rotuba katika ardhi kwa ajili ya migogoro. Tangazo la Injili ya amani, injili ile ambayo haina silaha ya moyo kabla wanajeshi, bado itakuwa aaminifu zaidi ikiwa tangazo kutoka kwa Wakrito hatimaye watapatanishwa na Yesu mfalme wa Amani; Wakristo wanaoongozwa na ujumbe wake, wa upendo na wa udugu wa ulimwengu, ambao wanakwenda katika mipaka yake ya jumuiya na kwa ajili ya taifa lao binafasi. Papa Francisko amerudia kusisitiza kuwa “leo hii lazima kutembee pamoja au ni kubaki tumesimama. Sio rahisi kutembea pekee yako. Na si kwa sababu ndiyo mtindo wa kisasa, hapana, ni kwa sababu Roho Mtakatifu alituamsha kwa maana hiyo ya uekumene na ya udugu”, amefafanua.
Baba Mtakatifu Francisko amesema katika mtazamo huo, tafakari yao kwa jinsi gani ya kusherehekea kwa namna ya kiekumene, miaka 1700 tangu hufanyika Mtaguso wa kwanza wa Nikea, tukio litakaolofanyika mnamo 2025, linawakilisha mchango wa thamani. Licha ya matukio haya katika maandalizi hasa kwa kipindi kirefu cha kufanyika kwa Mtaguso wa kwanza ilikuwa ni tukio la upatanisho kwa ajili ya Kanisa ambalo kwa mtindo wa Sinodi, lilithibitisha umoja unaozunguka imani binafsi. Mtindo na maamuzi ya Mtaguso wa Nikea, lazima uangaze mchakato wa sasa wa kikumene na kufanya kukomaa kwa hatua moya ya kuelekea hatima mpya ya umoja wa Kikristo. Kwakuwa miaka 1700 tangu kufanyika Mtaguso wa kwanza wa Nikea unakwenda sambamba na Mwaka wa Jibilei, Baba Mtakatifu anawatakia kwamba maadhimisho yajayo ya jubilei yaweze kuwa na ukuu wa kiekumene.
Kwa kuwa Mtaguso wa kwanza wa kiekumene ulikuwa ni tendo la sinodi na kuonesha hata kwa ngazi ya Kanisa la Ulimwengu, sinodi ambayo ni mfumo wa maisha na uandaaji wa jumuiya za kikristo, Papa Francisko ametoa mwaliko kwamba pamoja na Sekretarieti Kuu ya Sinodi, Baraza lao limeeelekeza kwa Mabaraza ya Maaskofu, kuwaomba wao watafute mitindo ya kusikiliza wakati wa sasa wa mchakato wa kisinodi wa kanisa Katoliki, hata sauti za kaka na dada wa wadhehebu mengine ya kikirsto kuhusiana na masuala ambayo yanahusiana na imani na huduma katika ulimwengu wa sasa. Ikiwa kweli watasikiliza sauti ya Roho, haiwzekani wasisikie kile ambacho alisema na anataka kusema kwa wale wote ambao wamezaliwa katika maji na katika Roho (Yh 3,5).
Songa mbele, tembea pamoja. Ni kweli kwamba kazi ya kitheolojia ni muhimu sana na ni lazima tutafakari, lakini hatuwezi kusubiri kufanya safari ya umoja [mpaka] wanatheolojia wakubaliane. Wakati mmoja, Morthodoksi mkuu, mwanatheolojia mkuu wa Othodoksi, aliniambia kwamba alijua ni wakati gani wanatheolojia wangekubali. Lini? Siku moja baada ya hukumu ya mwisho, aliniambia. Lakini wakati huo huo? Kuenenda kama ndugu, katika maombi pamoja, katika matendo ya upendo, katika kutafuta ukweli. Kama ndugu. Na undugu huu ni wetu sote. Kwa kuhitimisha, Baba Mtakatifu amewatia moyo waendelee na jitihada zao na umuhimu kwa huduma na anawasindikiza kila siku kwa ukaribu na shukrani. Anamuomba Bwana awabariki na amewaomba wasisahau kusali kwa ajili yake.