Papa Francisko:Dharura ya kijamii kwa upungufu wa kuzaliwa kwa watoto
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Ni dharura ya kijamii ambayo Baba Mtakatifu Fransisko anatumia maneno ya moja kwa moja kuonesha wazi tatizo la kutozaliwa watoto, ambalo ni suala la haraka sana la kushughulikiwa kwa sababu kuzaliwa kwa watoto wachache, hasa katika nchi za Magharibi, kunaweka hatari wa mustakabali wake. Baba Mtakatifu amefanya hivyo katika ujumbe wa salamu uliosomwa kwa washiriki wa toleo la pili la 'Mataifa ya Jumla kuhusu kiwango cha kuzaliwa' lililoandaliwa na Mfuko kwa ajili ya uzazi na mchango wa Jukwaa la Vyama vya Kifamilia Italia ambao tolep hilo limefunguliwa, tarehe 12 mei 2022 atika Ukumbi mmoja wa njia ya Conciliazione, jijini Roma linaloongozwa na kauli mbiu: “Inawezekana kufanywa”; mada ambayo kwa upande wa Papa amependa. Papa Francisko katika ujumbe wake ameomba radhi kutokuwepo kwake na ameweka wazi juu ya pembezoni iliyopo katika Magharibi, isiyoonekana sana, kwa mara moja. Hii ni kuhusu wale ambao wana shauku ya mtoto na hawawezi kufanya hivyo. Ndoto ya familia ambayo inavunjika na kupunguza hamu ya kutulia badala yake, inakimbilia katika biashara, magari, kusafiri, wakati panapokuwa na muafaka.
Huu ni umaskini wa kutisha
Papa Francisko amesema kwamba “huu ni umaskini mpya unaonitisha. Ni umaskini wa kuzaa wa wale ambao hupuuza tamaa ya furaha katika mioyo yao, ya wale wanaojitolea kupunguza matarajio makubwa zaidi, ya wale wanaoridhika na kidogo na kuacha kutumaini makubwa. Ndiyo, ni umaskini wa kutisha, kwa sababu unaathiri wanadamu katika utajiri wao mkubwa zaidi: kuzaa watoto ili kuwatunza, kuonesha uwepo kwa kupokea upendo kutoka kwa wengine”. Kiwango cha kuzaliwa, Papa anaandika, ni tatizo na asiyekabiliana nalo hana maono: “Ni kukataa kuona mbali, kutazama mbele. Inamaanisha kugeuka, kufikiria kuwa shida ni ngumu kila wakati na hakuna kinachoweza kufanywa”. Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kwamba “Katika uso wa kujisalimisha, lazima turudie tena kwamba inawezekana kufanywa, mtu anaweza kutumaini dhidi ya matumaini yote, dhidi ya idadi ambayo inazidi kuwa mbaya mwaka hadi mwaka. Inaweza kufanywa inamaanisha kutokubali tu kwamba mambo hayawezi kubadilika”.
Mambo yanaweza kubadilika bila kuwa na woga
Papa kwa maana hiyo amebainisha: “mambo yanaweza kubadilika ikiwa bila kuwa na woga, kwenda zaidi ya masilahi ya kishirikina na vizuizi vya kiitikadi, tunajitolea pamoja. Kwa hivyo, natumai kwamba katika ngazi zote za kitaasisi, vyombo vya habari, kitamaduni, kiuchumi na kijamii, sera madhubuti zitapendelewa, kuboreshwa na kutekelezwa, zinazolenga kuzindua upya kiwango cha kuzaliwa na familia”. Umoja ni njia ya kushughulikia masuala magumu zaidi, tukikumbuka kwamba suala la kiwango cha kuzaliwa ni suala ambalo haligawanyi. Kwa hiyo Papa amehimiza makampuni ya biashara, benki, mashirika, vyama vya wafanyakazi, wanamichezo, waigizaji, waandishi, wanasiasa, wote kwa pamoja kutafakari jinsi ya kuanza tena matumaini maishani. “Takwimu, utabiri, idadi za sasa zinajulikana kwa wote: ukweli unahitajika. Ni wakati wa kutoa majibu ya kweli kwa familia na vijana: matumaini hayawezi na hayafai kufa kwa kungoja. Baba Mtakatifu anamwomba Mungu abariki ahadi yao. na yeye yuko karibu nao ana anashangilia pamoja ili kuweza kubadilisha mkondo wa majira ya baridi kali ya idadi ya watu na kwa maana hiyo amsisitiza kwamba “Inaweza kufanyika!