Papa Francisko:Watawa hawajaitwa kuweka Yesu katikati kana kwamba wao ndio wahusika wakuu!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Maelekezo ya vitendo na kiroho ndiyo ambayo Papa amewaelekeza Watawa wa “Maestre Pie Filippini “na waamini wa Jimbo la Viterbo na wa Civitavecchia-Tarquinia, alipokutana nao katika Ukumbi wa Paulo VI , jijini Vaican wakisindikizwa na maaskofu, mapadre mameya, mamlaka na watoto wa Komunyo ya Kwanza. Papa Francisko amesema Kuisha kwa kuhuduma, bila kujifungia binafsi ndani ya Sakrestia, bila kuangukia na kukata tamaa na kulia yaliyopita, bila kuangukia katika madai ya uwongo ya watu wengi watawa na kuweza kumweka Yesu katikati. Hapana, ni sisi tunaopaswa kujiondoa kwenye kitovu ambacho ni mali yake. Papa amefika kwenye ukumbi akiwa katika kiti cha magurudumu, huku akisindikizwa na makofi ya kishindo, katika tukio la sherehe ya kumbukumbu ya miaka 350 ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa Shirika hilo Mtakatifu Lucia Filippini, ambaye majimbo ya Lazio yanamuheshimu. Papa amesema ni wakati wa thamani kurudi kwenye vyanzo na kuchota nguvu mpya kwa ajili ya siku zijazo. Na kwa mtazamo huo maradufu wa mambo yaliyopita na yajayo, Baba Mtakatifu amewahimiza Watawa hawa kuwa mashahidi, wakifuata utume huo unaodai ambao tayari jina la shirika linapendekeza “waalimu Safi”.
“Mwalimu ndiye anayefundisha. Hata hivyo, methali moja husema kwamba hatufundishi kile tunachojua, bali kile tulicho nacho. Kwa wengine tunapitisha kile tulicho nacho ndani. Haitoshi kujaza kichwa na mawazo, hii sio kuelimisha; kuelimisha ni kueneza maisha. Na kuwa mwalimu ni kuishi utume. Kwa upande mwingine, ikiwa tunatoa hotuba nzuri, lakini maisha yanakwenda katika mwelekeo mwingine, tuna hatari ya kuwa waigizaji tu wanaofanya kuwa sehemu, lakini si waelimishaji”, Papa Francisko ameeleza. Mtakatifu Lucia, ambaye mara nyingi anawakilishwa na Msalaba mkononi mwake au kwa kitendo cha kuuelekezea msalaba akitazama macho yake Mungu atoaye uhai na kuhisi kuitwa kufanya maisha kuwa zawadi. Hivyo kwa wengine aliweza kueneza kile alichokiweka moyoni mwake: si mahubiri, si nadharia, bali yaliyomo ndani na maisha, yaliyomo katika maisha”. Mfano wake unaonesha kwamba hatuwezi kuridhika na kumfundisha Yesu, kwa maana Yesu kwanza kabisa anajishuhudia mwenyewe.
Mungu huwasiliana mwenyewe ikiwa tu anaishi katika maisha yetu, ikiwa anajaza mapenzi yetu, ikiwa anaunganisha mawazo yetu na kutia moyo matendo yetu. Na ni nini uthibitisho wa hili? Papa ameuliza swali. Kwa kujibu amesema “Uwazi wetu kwa wengine, kwa yeyote anayemjua Bwana hajifungii ndani ya sakrestia, lakini anaishi ili kutumikia, bila kuwa na wasiwasi juu ya wapi au nini anaombwa kufanya.Ni katika mtazamo huo, Papa Francisko ametoa mwaliko pia kutazama ugumu wa maisha ya kitawa, hasa kwa kuanzia na ukosefu wa miito. Papa amewapa ushauri ambao amesema hauwakilishi suluhisho la haraka la matatizo haya, bali ni njia kuu ya kuyatatua.
Awali ya yote Papa Francisko amesema hawa hawajaitwa kuweka Yesu katikati kana kwamba wao ndio wahusika wakuu; badala yake wao wameitwa kwanza kabisa kujiondoa wao wenyewe kutoka kwa kitovu ambacho ni chake, na ili kuweza kusihi wakfu wao kama wito wa huduma . Ni kuchukua njia mpya kwa ujasiri kulingana na wakati. Hivi ndivyo Yesu anaruhusiwa kufanya kazi ndani yao anavyotaka na kufundisha kushinda kujiuzulu na kutamani, kujifunza nyakati hizi ngumu na hivyo kwa hakika ni kuchukua njia mpya kwa ujasiri kulingana na nyakati, Papa Francisko amesisitiza. Kwa kufanya hivyo watakuwa walimu wazuri na watabaki vile vile kuwa wanafunzi walioitwa kila siku kuhudumia, kwa furaha!
Wazo la pili, Papa ambalo Papa Francisko amehutubia waamini wanafuata roho ya Mtakatifu Lucia Filippini ni siri ambayo mwanamke huyu aliiweka ya kuishi kwa kumtumaini Mungu daima, kwa sababu yeye alisema “hawezi kuacha kuwa baba yangu”. Mara nyingi katika maisha, tuna wasiwasi kwa sababu tunapaswa kuacha vitu vingi: baadhi ya dhamana, miaka ya ujana, afya kidogo, labda wapendwa ... Naam, ikiwa katika maisha kuna watu na mambo ambayo mapema au baadaye tunapaswa kuondoka kuyaacha, kuna uwepo ambao hautatuacha kamwe, uhakika wa kimsingi ambao utatusindikiza daima na kwamba hakuna chochote na hakuna mtu anayeweza kufuta yaani kile cha Mungu hawezi kuacha kuwa baba yangu”.
Papa Francisko, amesema “Mungu, hawezi kuacha kuwa baba yangu. Ni jambo zuri gani hili, eh? Je, turudie pamoja, sisi sote? Mungu hawezi kuacha kuwa baba yangu. Rudieti tena kwa nguvu zaidi: Mungu hawezi kuacha kuwa baba yangu. . Wekeni wazo hilo moyoni mwenu…. Kila kitu kinaweza kutuangusha, lakini si huruma ya Mungu, amehitimisha Baba Mtakatifu. Tukumbuke hili daima, hasa katika nyakati za giza: Mungu kamwe hatutupi, kwa sababu hawezi kuacha kuwa baba.