Papa,Kundi Mtakatifu Marta:Hitaji la kusindikiza na kufungamanisha waathirika wa utumwa
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wajumbe wa Kikundi cha Mtakatifu Marta, wanaofanya mkutano wa Kimataifa, ambao unaunganisha uongozi mbali mbali wa mashirika, serikali, kiraia na kidini ili kushirikishana taaluma, uzoefu na uboreshaji wa kazi, kwa lengo kuu la kuzuia na kupambana dhidi ya biashara ya binadamu na mitindo mbali mbali ya utumwa. Papa amewasahukuru kwa jitihada za kutafuta kuondoa mizizi ya shughuli hizi za kihalifu, ambazo zinakiuka hadhi na haki za wanaume, wanawake na watoto na kuacha madhara makubwa ya kudumu kwa kila mwathirika na juu ya jamii kwa ujumla.
Kikundi cha Mtakatifu Marta kuhamasisha uelewa na asili ya biashara haramu ya binadamu
Kwa miaka iliyofuata baada ya kuundwa kwake, “kikundi cha Mtakatifu Marta” kimejikita kwa dhati kuhamasisha kwa kiasi kukubwa uelewa na asili ya biashara ya binadamu na kuongeza nguvu za ushirikiano kwa ngazi ya kimataifa, kitaifa na kikanda ili kutafuta njia muafaka kwa lengo la kufikisha mwisho wa balaa hilo na kwa kuwafanya wahanga kupata msaada wa lazima, iwe kwa ngazi za kimwili na kiroho. Baba Mtakatifu amesema lakini licha ya jitihada hizo, kwa bahati mbaya mitindo mipya uya utumwa mamboleo inaendelea hata katika maeneo yaliyoendelea katika ulimwengu. Ni matumaini ya Papa kwamba mapambano dhidi ya bishara ya binadamu inaweza kufukiriwa kwa kiasi kikubwa hata kwa mfululizo wa hali halisi na mpana zaidi kama utumiaji na uwajibaki wa teknolojia na vyombo vya habari, na ulazima wa kupyaisha maono adili ya maisha ya kisiasa, kiuchumi na kijamii wanaojikita si tu kwa sababu ya faida lakini juu ya mtu.
Msingi wa kusaidia,kusindikiza na kufungamanisha waathirika wa biashara ya binadamu
Katika pendekezo hilo Papa Francisko amekumbusha hata hitaji msingi wa kusaidia, kusindikiza na kufungamisha waathirika wa biashara ya binadamu katika jumuiya na kuwasaidia katika mchakato mzima wa uponeshaji na kuwarudishia wao kujitegemea. Pamoja na kuwa kazi ngumu, Papa Francisko anawatia moyo wa kuendelea katika jitihada zao kuelekeza kusaidia hadhi iliyotolea na Mungu kwa kila mtu na kulinda haki msingi kwa wale ambao kwa bahati mbaya mara nyingi wamesahuliwa na hawana sauti. Kanisa daima linapongeza kila aina ya kielelezo cha upendo kidugu na utunzaji uliooneshwa na wale wote ambao wamefanywa watumwa na kunyonywa, kwasababu katika ulimwengu huu huruma ya Mungu inaonekana na kusukwa na jamii ambayo inatia bidiii na kupyaishwa. Na kwa kuhitimisha Papa Francisko amerudia kuwashukuru tena jitihada zao na kwa ushirikiano katika sekta hiyo. Anawatakia mema katika kazi yao. Na juu yao, familia zao na wale wote ambao wanawahudumia amewatakia baraka ya Bwana, ili wabariki wote. Na amewaomba wamkumbuke katika sala zao.