Papa:Kupaa kwa Yesu ni kutaka kukaa karibu na watu wake

Kabla ya kupaa Kristo aliaamsha mikono yake na kuwabariki mitume.Ni ishara ya Kikuhani.Mungu tangu kipindi cha Haruni,alikuwa amewakabidhi makuhani kazi ya kubariki watu.Injili inataka kutueleza kwamba Yesu ni kuhani Mkuu wa maisha yetu.Yesu anapaa kwa Baba ili kutuombea,kuwakilisha Jumuiya yetu.Kwa maana hiyo mbele ya macho ya Baba, wapo na watakuwapo daima Jumuiya ya Yesu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika siku ambayo Mama Kanisa  anasheherekea Kupaa kwa Bwana Mbinguni, Baba Mtakatifu Francisko ametoa tafakari yake kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kusali sala ya Malkia wa Mbingu, Dominika tarehe 29 Mei 2022. Akianza tafakari hiyo amesema: “Leo nchini Italia na Nchi nyingi zinasheherekea Kupaa kwa Bwana, yaani kurudi kwake kwa Baba. Katika Injili kwa mujibu wa Luka, anaelezea kuhusu kutokea kwa Mitume Mfufuka (Lk 24,46-53). Maisha ya Yesu duniani yanahitimisha kwa Kupaaa, ambayo tunasadiki katika sala ya Imani. “Amepaa mbinguni, amekaa kuume kwa Baba.” Je ni nini maana ya tukio hilo? Je tulitambue namna gani? Papa ameuliza na kujibu: Kwa kujibu swali hili, tujikite kutazama matendo mawili ambayo Yesu anatimiza kwanza kabla ya kupaa Mbinguni. Awali ya yote anatangaza zawadi ya Roho Mtakatifu na baadaye anawabarki mitume.

Waamini wakiwa uwanja wa Mtakatifu Petro kwa sala ya Malkia wa Mbingu
Waamini wakiwa uwanja wa Mtakatifu Petro kwa sala ya Malkia wa Mbingu

Kitu cha kwanza Yesu anawambia marafiki zake:“Mimi nitawatumia Yule ambaye Baba aliniahidi”. Anazungumzia Roho Mtakatifu, Mfariji, Yule ambaye atawasindikiza, atawaongoza, atawasaidia katika itume wao, na atawalinda katika mapambano ya kiroho. Anapaa mbinguni lakini hawaachi peke yao. Zaidi ya hayo anapopaa kuelekea kwa Baba anawahakikishia uvuvio wa Roho. Katika fursa nyingine alikuwa amesema: “ Yawafaa  mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka , huyo msaidizi hatakuja kwenu”. (rej. Yh 16,7). Hata hapo anaonesha upendo wa Yesu kwetu sisi, Papa amebainisha. Upendo wake ni uwepo ambao hautaki kuishia kuzuia uhuru wetu.

Waamini wakiwa uwanja wa Mtakatifu Petro kwa sala ya Malkia wa Mbingu
Waamini wakiwa uwanja wa Mtakatifu Petro kwa sala ya Malkia wa Mbingu

Kinyume chake, unatoa nafasi kwetu, kwa sababu ni upendo wa kweli ambao unazaa daima ukaribu ambao haukandamizi, lakini unafanya kuwa mhusika mkuu. Kwa njia hiyo Yesu anathibitisha :“ Mimi nina kwenda kwa Baba na ninyi mtajazwa na nguvu kutoka kwa aliyejuu. Nitawatumia Roho mwenyewe na kwa nguvu zake mtaendelea katika kazi yangu ulimwenguni ( Lk: 24,49). Kwa maana hiyo kupaa kwa Yesu Mbinguni, badala ya kukaa karibu na wachache kimwili, anakuwa karibu na wote kwa Roho yake. Roho Mtakatifu anafanya uwepo wa Yesu kwetu sisi, zaidi ya vizingiti vya wakati na nafasi, ili kutufanya tuwe mashuhuda wake ulimwenguni.

Waamini wakiwa uwanja wa Mtakatifu Petro kwa sala ya Malkia wa Mbingu
Waamini wakiwa uwanja wa Mtakatifu Petro kwa sala ya Malkia wa Mbingu

Mara moja baadaye  ilifuata tendo jingine, Kristo aliinua mikono yake na kuwabariki mitume (Lk 24,50). Ni ishara ya Kikuhani. Mungu tangu kipindi cha Haruni, alikuwa amewakabidhi makuhani kazi ya kubariki watu (Hes 6,26). Injili inataka kutueleza kwamba Yesu ni kuhani Mkuu wa maisha yetu. Yesu anapaa kwa Baba ili kutuombea, kuwakilisha Jumuiya yetu. Kwa maana hiyo mbele ya macho ya Baba, wapo na watakuwapo daima Jumuiya ya Yesu, Maisha yetu, matumaini yetu, na majeraha yetu. Kwa maana hiyo wakati anatimiza kuondoka kwake kuelekea Mbinguni, Kristo anatutengenezea Njia, anakwenda kutuandalia makao, na tangu sasa, anasali kwa ajili yetu, kwa sababu nasi tunaweza daima kusindikizwa na kubarikiwa na Baba.

Waamini katika Sala ya Malkia wa Mbingu 29 Mei 2022
Waamini katika Sala ya Malkia wa Mbingu 29 Mei 2022

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea ameomba kufikiria tangu leo hii, juu ya zawadi ya Roho ambayo tumeipokea kutoka kwa Yesu ili kuwa mashuhuda wa Injili. Ikiwa kweli sisi ni mashuhuda na hata kama sisi tuna uwezo wa kupenda wengine, kwa kuwaacha huru na kufanya kuwa na nafasi. Na baadaye je tunajua kuwaombea wengine, yaani kujua kuwaombea wao na kuwabariki maisha yao? Au tunawahitaji kwa sababu ya matakwa yetu? Tujifunze hili kusali kwa maombezi, kwa ajili ya matumaini na kwa ajili ya mateso ya ulimwengu na kwa ajili ya amani. Na tubariki kwa mtazamo wa kweli na kwa maneno kwa kila tunayekutana naye kila siku. Baba Mtaatifu amehitimisha kwa sala ya kwamba tusali kwa Mama mbarikiwa kuliko wanawake wote aliyejazwa na Roho Mtakatifu, na anasali daima kwa ajili yetu.

TAFAKARI YA PAPA YA KUPAA KWA BWANA
29 May 2022, 12:49