Tafuta

2022.04.05 Sport Senza Frontiere-bambini Ucraina 2022.04.05 Sport Senza Frontiere-bambini Ucraina 

Papa:ninateseka na kulia kwa mateso ya watu wa Ukraine

Wazo la Baba Mtakatifu kwa mara nyingine tena ni katika Nchi ya Ukraine mahali ambapo zinafika taarifa za kutisha za watoto waliofukuzwa na kuchukuliwa.Papa amesema:“Na wakati tunashuhudia kuporomoka kwa ubinadamu,ninajiuliza,pamoja na watu wengi wenye huzuni,ikiwa kweli tunatafuta amani.Amethibitisha hayo mara baada ya sala ya Malkia wa Mbingu Dominika Mei Mosi,2022.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Wazo la Baba Mtakatifu Francisko Dominika Mei Mosi 2022 limekwenda katika Mwezi uliowekwa wakfu kwa  Mama wa Mungu. Papa amesem:  “Ninapenda kuwaalika waamini wote na jumuiya kusali Rosari kila siku kwa mwezi Mei, kwa ajili ya amani.” Kwa haraka mawazo yake yamekwenda kwenye mji wa Mariupol, mji wa Maria nchini Ukraine ambao umeharibiwa sana na mabomu kwa ukatili. Hata kwa leo, Baba Mtakatifu amepyaisha maombi yake ili kuwezesha msaada wa kibinadamu kuokoa watu walio kwenye mtego wa kiwanda cha chuma katika mji huo. Papa amesema kwamba analia akifikiria mateso ya watu wa Ukraine na kwa namna ya pekee walio wadhaifu zaidi, wazee na watoto. Na zinafika habari mbaya za watoto ambao wamefukuzwa na kuchkhuliwa.

Papa amesema: “Na wakati tunashuhudia kuporomoka kwa ubinadamu, ninajiuliza pamoja na watu wengi wenye huzuni, ikiwa kweli tunatafuta amani; ikiwa kuna nia ya kuzuia kuongezeka kwa nguvu za kijeshi na chochezi za maneno; ikiwa kuna linalowezekana ili silaha zisitishwe. Tafadhali ninaomba msijisalimishe katika mantiki ya vurugu, kwa msururu potovu wa silaha. Chukue njia ya mazungumzo na amani! Tuombe,” Papa amesema.

Hata hivyo inasemekana kwamba kulipuliwa kwa kiwanda cha chuma huko Kharkiv kumesababisha angalau majeruhi 600, ambao wanahitaji huduma ya haraka. Kwa siku kadhaa, kumekuwa na mazungumzo juu ya mpango wa kuhamisha mtambo huo, lakini haujawahi kutekelezwa. Kiukweli, tarehe 29 Aprili vikosi vya Urussi vilizunguka tena jengo hilo, ambalo limeenea katika eneo la kilomita za mraba 11. Huko Kharkiv, jeshi la Kiukreni lilitangaza mashambulizi kadhaa ya ushindi, lakini wakati wa usiku mji wa pili wa nchi hiyo ulipigwa tena na mizinga ya Urussi, wakati vyanzo vya serikali ya Kiev vinazungumza juu ya “hasara kubwa” tangu mwanzo wa mzozo kati ya Urussi.

Hata hivyo matumaini machache yanasikika katika nyanja ya kidiplomasia na rais wa Ukraine, Bwana Volodomyr Zelenski, ambayealitaka kukutana na Rais Vladimyr Putin, kwa sababu: "mtu mmoja anaamua kila kitu nchini Urussi. Ikiwa kuna uwezekano wa mmoja tu, tunapaswa kuzungumza", alisema Zelenski, akibainisha kuwa hatari ya mazungumzo kushindwa ni ya juu, kwa sababu baada ya Bucha na Mariupol, watu wana uaminifu mkubwa na hamu ya ukombozi kutoka kwa  Warussi.

PAPA ATOA WITO TENA WA KUKOMESHA VITA NCHINI UKRAINE
01 May 2022, 14:20