Papa Francisko akizungumza na Tume ya Kipapa ya Amerika Kusini Papa Francisko akizungumza na Tume ya Kipapa ya Amerika Kusini 

Papa:Umoja wa Kanisa kwa umakini katika utofauti za karama,miito na huduma!

Katika ujumbe kwa njia ya video kwa Tume ya Kipapa ya Amerika ya Kusini kwenye kikao,Papa amezungumzia sinodi katika Kanisa ambalo si mwelekeo wa shirika.Sinodi inahitaji umoja na inatuhimiza kushinda ule ukasisi,ambao ni upotovu wa utulivu.Moyo wa hotuba yake ni njia ya sinodi ambayo amebainisha si mpya,kiukweli ni suala la kutoa msukumo mpya kwa kusikiliza na kutoa nafasi ya Roho Mtakatifu.

Na Angella Rwezaula - Vatican

Katika fursa ya kikao cha Tume ya Kipapa ya Amerika ya Kusini, Baba Mtakatifu Francisko amerejea katika ujumbe wake kwa njia ya video kuzungumzia umoja na ushiriki, funguo muhimu za  uelewa na utekelezaji wa kile ambacho tayari kilikuwa kimefanyika katika Mkutano Mkuu wa III wa Baraza la Maaskofu wa Amerika huko Puebla na vile vile dhana ya uongofu wa kichungaji ilikuwa lengo la Mkutano Mkuu wa IV wa Santo Domingo na wa Mkutano Mkuu wa V wa Aparecida. Moyo wa hotuba yake ni mchakato wa safari ya sinodi ambayo amebainisha kwamba si mpya, kwa sababu, kiukweli ni suala la kutoa msukumo mpya wa kusikiliza na kutoa nafasi kwa Roho Mtakatifu.

Kuacha nafasi ya Roho Mtakatifu

Papa Fransisko anatambua kwamba, mchakato wa safari ya sinodi ya Kanisa kwa asili imeshindwa katika Kanisa la Amerika Kusini huku ikihifadhiwa na Makanisa ya Mashariki. Alikuwa ni Mtakatifu Paulo VI aliyeirudisha katika mwendo mwishoni mwa Mtaguso kwa kuunda Sekretarieti ya Sinodi ya Maaskofu. Kwa maana hiyo Papa Francisko ametumia picha ya mtoto ambaye anaanza kutembea hatua ndogo, akiwa na woga na wakati mwingine hata wenye kudhoofisha ili kujifunza kutembea. Ni kitivo ambacho ni lazima kupata upya na kugundua kwa upande mmoja udogo wetu, kwa upande mwingine kwamba fursa ni wakati mwafaka (Kairos) wa kutumiwa vizuri kwa ajili uongofu kamili wa kibinafsi na wa kichungaji. Jambo la muhimu Papa Francisko ameonesha, ni kuacha nafasi kwa ajili ya pumzi ya Roho, bila kuwa na dhana ya kujua kila kitu kwanza ambapo kiukweli ni hatari kubwa zaidi kwa upande wa Papa. 

Mwanzo wa Taalimungu ya ukombozi

Papa Francisko amethibitisha wazi hasivyopenda mawazo ya kijuu juu na yaliyofungwa. Anafanya hivyo kwa kutaja kipindi ambacho kinarejea mwanzo wa Taalimungu ya Ukombozi wakati uchambuzi wa Marx, ambao Papa na Mkuu  wa Kijesuit waliitikia kwa ukali sana wakati huo, kwa sababu walipata itikadi ya kile ambacho kilkuwa kinaelezeka katika mchakato wa Amerika Kusini. “Na ninasema telluric, ameongeza kwa sababu hali ya kiroho ya Amerika ya Kusini imeunganishwa na dunia na haiwezi kutenganishwa nayo”. Papa Francisko amebainisha  jinsi ambavyo  anaamini kuwa “Kanisa la Amerika  Kusini na  Visiwa vya Carribien limefanikisha njia yake ambayo Roho hujenga wakati mawazo yetu hayajakamilika, yanapokamilika hayafanyi kazi”. Bila uwazi huu kwa Roho, Papa amesema “kipaji hakituelimishi kwa sababu hakiwezi kuingia moyoni”. Kwa sababu hakilazimishi bali kinataka kuingia wa utamu. Mwaliko wa Papa Francisko ni kuifanya zawadi hiyo itendeke, ambayo haitabiriki na inatushangaza kila wakati, iliyo ya bure na isiyostahiliwa". Kwa kutazama Pentekoste, Papa ametoa onyo  kwamba sio tukio la zamani, kwani Roho ("Mkubwa Asiyejulikana") ni wa kisasa."

Mashuhuda wa Pentekoste

Wakati wa 'maarifa yaliyofungwa' au kwa tamaa tunafikiria kutawala kila kitu tunaanguka kwa urahisi katika jaribu la udhibiti kamili, kwa kuchukua nafasi, kufikia umuhimu wa juu juu kwa wale wanaotaka kuwa wahusika wakuu kama katika mfululizo wa  vipindi vya TV. Badala yake tunahitaji kufungua michakato. Papa Fransisko amekiri kwamba hapo mwanzo Roho ni kama alileta tatizo fulani na katika suala hilo, amependekeza kuwazia kile kilichotokea asubuhi ya Pentekoste wakati mashuhuda walipokuja kufikiri kwamba walikuwa miongoni mwa walevi. Lakini basi, hapa ananukuu Mtakatifu  Basilio, kwamba hayo ni “ni maelewano”. Papa pia ameweka bayana mwelekeo wa Ekaristi kwa msingi wa sinodi halisi.” Bila mati hiyo, ushiriki wetu ungekuwa ule wa ubunge tu, wakati ni ishara ya umoja wa kikanisa ambao unajaribu kusonga mbele. Wabatizwa wote ni sinodi, marafiki wanaosindikizana na Bwana katika safari yake.

Upendo wa Ushemasi kwa Kanisa la Amerika Kusini

Sinodi si mwelekeo wa shirika au mpango wa ufufuo wa kibinadamu wa watu wa Mungu badala yake Papa amesisitiza kuwa ni mwelekeo wa nguvu na wa kihistoria wa umoja  wa kikanisa ulioanzishwa juu ya ushiriki wa Utatu ambao, wakati wa kufahamu hisia,  imani  ya watu wote watakatifu wa Mungu, umoja wa kitume na umoja na Mrithi wa Petro lazima kuhuisha uongofu na mageuzi ya Kanisa katika kila ngazi”. Kutokana na mambo hayo na ufafanuzi, mwaliko uliojitokeza ni kwamba Tume ya Amerika ya Kusini bara ambalo Papa kutoka Argentina analitazama kwa upendo na umakini wa kipekee  liwe la ushemasi ambalo litasadia mabaraza mbalimbali kutenda kwa harambee na kuelewa vyema ukweli wa kijamii na kikanisa katika kanda. Haipaswi kueleweka kama mipaka inayodhibitiwa. Mambo ya Amerika ya Kusini au mwelekeo wa Kihispania ya Canada na Marekani, hapana". Badala yake, lazima iendeleze utambulisho na udugu fulani ambao mataifa ya Amerika ya Kusini wanaishi.

Mwaliko wa kuishi umoja wa Kikanisa na kuishi tofauti za karama

Kwa kurudi kwa Roho Mtakatifu, ni yeye ambaye lazima awe mhusika mkuu ambapo Papa  Francisko amesema sio sisi. “Kama sehemu ya mageuzi ya Curia Romana, Papa ametumaini kuwa chombo cha CAL kitazalisha mienendo mipya na kufuta baadhi ya desturi na tabia zetu za mapadre". Kumbuka kwamba kujisikia kikuhani ni upotovu wa kimya. Umoja bila sinodi unaweza kutokeza kwa urahisi kati kwa uthabiti fulani usiohitajika. na kwa maana hiyo  Sinodi bila umoja inaweza kuwa ya kijuu juu katika Kanisa. Hatimaye, Papa ametoa mwaliko wa kuishi Umoja wa Kikanisa kwa umakini zaidi katika utofauti wa karama, miito na huduma, kwa kujitazama na upendeleo wa ubinafsi, na ili kujitoa katika kuhamasisha michakato inayowaruhusu watu wa Mungu, wanaotembea katika historia, kushiriki zaidi na zaidi, kuwa bora zaidi kwa jukumu la pamoja ambalo wote wanalo la kuwa Kanisa. Kwa sababu “sisi sote ni watu wa Mungu. Sisi sote ni wanafunzi walioitwa kujifunza na kumfuata Bwana. Sisi sote tunawajibika kwa manufaa ya wote na utakatifu wa Kanisa”.

HOTUBA YA PAPA KWA TUME YA KANISA LA AMERIKA KUSINI
26 May 2022, 18:54