Tafuta

2019.05.22 Mama Maria wa Sheshan, nchini China. 2019.05.22 Mama Maria wa Sheshan, nchini China. 

Papa yuko karibu na wachungaji na waamini wa China wanaoishi hali ngumu

Papa Francisko amekumbuka kumbu kumbu ya Bikira Maria Msaada wa Wakristo ambapo ametoa mwaliko kwa Kanisa kuungana katika Kanisa kwa ajili ya sala na wakatoliki wa China ambao wanaishi katika hali ngumu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Mara baada ya sala ya Malkia wa Mbingu Dominika tarehe 22 Mei 2022 amekumbusha jinsi ambavyo Jumanne ijayo yaani tarhe 24 Mei ni Kumbu Kumbu ya Bikira Maria Msaada wa Wakristo, kwa namna ya pekee siku kuu inayosikika sana nchini China ambao wanamheshimu kama Msimamizi wao katika Madhabahu ya Sheshan huko Shanghai na idadi kubwa ya Makanisa katika nchi na katika majumbani mwao. Katika tukio hilo, limempatia fursa Baba Mtakatifu kupyaisha kwao uhakikisho wa ukaribu wake kiroho; na amebainisha anavyo fuatilia kwa makini na ushiriki wa maisha na matukio ya waamini na wachungaji ambao mara nyingi wanaishi hali  ngumu, na kwa maana hiyo anasali kila siku kwa ajili yao.

Kuungana kwa sala ili Kanisa la China liwe huru na utulivu

Kwa kuongezea, Baba Mtakatifu Francisko amewaomba waungane wote katika sala hiyo, ili Kanisa nchini China, liwe na uhuru na utulivu, na linaweza kushi kwa muungano wa kweli na Kanisa la Ulimwengu ili kufanya mazoezi ya utume wake wa kutangaza Injili kwa wote, kwa kutoa hata mchango chanya kwa ajili ya maendeleo ya kiroho na zana za kijamii.

Juma la Laudato sì, 22-29 Mei 2022

Papa Francisko aidha amekumbuka Juma la Laudato si ili kusikiliza daima kwa makini kilio cha Dunia, ambacho kinatoa mwamko wa kutenda kwa pamoja kwa ajili ya kutunza nyumba yetu ya pamoja. Papa Francisko ameshukuru Barza la Kipapa la Maendeleo Fungamni ya Bindamu na mashirika mengi yaliyounga mkono na wote Papa amewaaalika kushiriki

22 May 2022, 14:59