Watawa wakishiriki Misa katika Kanisa Kuu la Mama Yetu wa Congo (Kinshasa). Watawa wakishiriki Misa katika Kanisa Kuu la Mama Yetu wa Congo (Kinshasa). 

Ratiba ya ziara ya Papa nchini Congo na Sudan Kusini:kati ya vijana &waathirika wa vurugu

Tunachapisha ratiba rasimi ya Ziara ya Kitume ya 37 ya Papa Francisko katika Nchi mbili za Bara la Afrika kuanzia Julai 2-7 Mei.Baba Mtakatifu anatarajia kutembelea nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC (Kinshasa na Goma) na Sudan Kusini katka mji mkuu wa Juba.

Na Angella. Rwezaula – Vatican.

Zitakuwa ni Nchi mbili, za bara la Afrika katka miji mitatu, hotuba nane, tafakari tatu, mikutano na Mamlaka ya raia na kikanisa, vijana, watu wakimbizi wa ndani, na waathirika wa vurugu. Ni ratiba nzito pamoja na vipindi tofauti ya kupumzika, ambayo vinamsubiri Baba Mtakatifu Francisko katika ziara yake ya kitume ya 37, kuanzia tarehe 2 hadi 7 Julai 2022 katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudan Kusini. Hii itakuwa ni kutimizia shauku ya Baba Mtakatifu Francisko aliyoelezea miaka miwili iliyopita ya kuwa “Mhujaja wa Uekumene wa Amani”, pamoja na Askofu Mkuu wa Canterbury, Justin Welby, na Mchungaji Jim Wallace wa Baraza Kuu la Kanisa la Scotland.

Ofisi ya Vyombo vya habari, Jumamosi tarehe 28 Mei 2022 imechapisha ratiba rasimi ya ziara ya kitume ya Papa, ambapo tarehe 2 Julai ataondoka saa 3.30 katika uwanja waNdege wa Kimataifa Fiumicino Roma kuelekea mji mkuu Kinshasa, DRC. Katika Kiwanja cha Kimataifa cha “Ndjili”, Papa Francisko atatelemka baada ya masa 6 na nusu hivi ya safari. Baada ya makaribisho rasimi, atakwenda kwenye Jumba Kuu la Kitaifa kwa ajili ya afla ya kukaribishwa, pia itafuatia ziara ya faragha kwa Rais Félix Tshisekedi katika Kumbi za Rais na baadaye kufanya Mkutano katika bustani Ikulu ya Rais na Mamlaka ya Rais na Wanadiplomasia ambapo atatoa hotuba yake ya kwanza ya safari. Siku yake ya kwanza itahitimishwa na mkutano wa kiutamaduni na wanajumuiya ya Kijesuit iliyoko nchini humo katika ubalozi wa kitume.

Misa na mkutano na Makleri wa Kinshasa

Siku ya Pili ya ziara ya Papa Francisko, Dominika tarehe 3 Julai atakuwa na mambo mawili. La kwanza ni Misa takatifu saa 2.00 katika Uwanja wa Ndege wa Ndolo huko Kinshasa, na baada ya misa itafutia sala ya Malaika wa Bwana. Jioni saa 12.00,  Papa Francisko atakutana na maaskofu, mapadre, watawa na waseminari katika Kanisa Kuu la Mama Yetu wa Congo.

Safari ya Kivu Kaskazini

Ratiba ya Papa Francisko mnamo tarehe 4 Julai, ataondoka Kinshasa kuelekea Kivu Kaskazini katika wilaya ya mwisho Mashariki mwa Nchi. Safari ya ndege kuelekea katika mji wa Goma inatazamiwa alfajiri na mapema saa 12.45  na kufika saa 4.15. Jambo la kwanza baada ya kufika huko Papa Francisko ataadhimisha misa saa 6.00 mchana  katika Kambi ya  Kibumba; Jioni saa 11.00, Papa Francisko atakutana na waathirika wa vurugu waBeni. Huu ni mji wa pili muhimu huko Kivu Kaskazini , ambao umepata janga la Ebola na majanga ya asili, lakini zaidi kuwa na matukio mengi ya mauajia  ya raia  na matatizo mengine mengi kama vile uutekaji nyara,  ujambazi, mauaji ya jumla yaliyofanywa na wanamgambo na jeshi. Papa Francisko atakaa karibu zaidi ya saa moja kuzungumza na waathirika katika Kituo cha Mapokezi cha Jimbo la Goma, na baadaye saa 12.30 jioni ataondoka kurudi uwanja wa Ndege ili kurudi Kinshasa.

Safari Sudan Kusini

Na kutoka Kinshasa, Baba Mtakatifu atawaaga siku inayofuata, Jumanne tarehe 5 Julai 2022 akiwa anaelekea Mji Mkuu Juba Sudan Kusini. Kabla ya kuondoka lakini atakutana saa 2.40 katika Uwanja wa Mashahidi na Vijana na Makatekista.  Saa 4.10 asubuhi hivi ikifuata afla ya kuagwa katika uwanja wa Ndege Ndjili”.  Kwa njia hiyo  safari yake ni pamoja na Askofu Mkuu Welby na Wallace kwenda  Juba mahali ambapo watafika muda wa saa 9 alasiri. Hatua ya kwanza ni katika Jumba la Rais kwa ziara ya faragha kwa Rais Salva Kiir Mayardi, ambaye mnamo Aprili 2018, Baba Mtakatifu alikuwa amewakaribisha katika nyumba ya Mtakatifu Marta pamoja na vongozi wakuu wa kidini na kisiasa wa Sudan Kusini kwa ajili ya mafungo ya kiroho ya kiekumene, yaliyokuwa yamelengwa kwa ajili ya kuomba zawadi ya amani katika Nchi ambayo imeteseka kwa umwagaji damu wa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Muda kidogo baadaye kutakuwa na mkutano na Makamu Rais wa Sudan Kusini katika Bustani ya Ikulu, Mamlaka na viongozi wa kidiplomasia. Katika fursa hiyo kunatazamiwa hotuba ya Papa

Mkutano wa watu wakimbizi wa ndani

Siku ya Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 6 Julai, itafunguliwa na ziara kwa watu wakimbizi wa ndani katika Kambi za ndani huko Juba , saa 2.45. Wakati huo asaa 5.30 subuhi, Papa atakutana kwa faragha na Wajesuit wa Sudan katika Ubalozi wa Vatican nchini humo. Baada ya mapumziko marefu, saa 11.00, jioni Baba Mtakatifu Francisko atakutana na maaskofu, mapadre na watawa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Teresa. Saa 12.30 itafuata sala ya kiekumene katika uwanja wa Kumbu kumbu ya John Garang”,(wa chama cha ukombozi wa watu) eneo linalokubusha kiongozi wa Sudan, na Makamu rais wa Sudan Kusini baada ya mkataba wa amani.

Misa na safari ya kurudi Roma

Katika eneo la kumbu kumbu na hata mikutano ya kisiasa, Papa Francisko atarudi tena kesho yake asubuhi tarehe 7 Julai, kuadhimisha misa inayotarajiwa kufanyika saa 2.00 asubuhi na itakayo kuwa ya ya mwisho wa safari yake. Baba Mtakatifu Francisko anatarajia kuondoka saa 4.45 hivi kuelekea uwanja wa Ndege kwa afla ya mwisho ya kuagwa . Safari ya kurudi Roma inatarajiwa kuanza saa 5.15 hivi  na kutua Uwanja wa Kimataifa wa Fiumicino Roma saa 12.05 jioni .

 

28 May 2022, 16:17