2022.06.20 Maaskofu wa Brazili wakiwa' katika hija yao ya kitume.  2022.06.20 Maaskofu wa Brazili wakiwa' katika hija yao ya kitume.  

Papa alikutana na Maaskofu kutoka Brazili wakiwa katika hija ya

Papa Francisko alikutana na maaskofu wa 17 mjini Vatican wanaowakilisha Kanda ya Kaskazini ya Baraza la maaskofu Brazili,Majimbo ya Amazonia na Roma na Kaskazini-Magharibi huko Ekari,Kusini mwa Amazonia na Rondônia,ambapo walimkabidhi kofia kichwa na ubao ulioandikwa “SOS Yanomami”,ambao umechorwa kwa maandishi 1989 na msanii wa kiasilia.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kifuniko au kofia? Hawakuweza kuwa na zawadi ya tabia nyingine zaidi kwa Papa Francisko kutoka kwa maaskofu waliokuja kutoka Amazonia kwenye ziara ya kitume Visita ad Limina jijini hasa kutoka kwa wawakilishi wa Kanda 1 ya Kaskazini la Baraza la Maaskofu Nchini Brazili (CNBB) (Majimbo ya Amazonia na Roraima) na Kaskazini Magharibi (Acre, kusini mwa Amazonia na Rondônia). Maaskofu hao 17 walipokelewa Jumatatu asubuhi tarehe 20 Juni 2022. Kwa Askofu Mkuu wa Porto Velho, huko Rondônia, Roque Paloschi, akihojiwa mara baada ya mkutano huo  na Papa na Vatican News,  amesema huo ulikuwa ni mkutano wa umoja, matumaini na ujasiri. “Kutoka katika umoja,  kwa sababu alikaribisha kila kitu tulicholeta kutoka kwetu ukweli wa makanisa yetu huko Amazonia. Kutokana na tumaini, kwa sababu alitutia moyo ili kuishi utume wetu kama wachungaji na sio warasimu, na tusipoteze mwelekeo huo. Na ujasiri, kuwa pamoja na idadi ya watu maskini zaidi na, zaidi ya yote, kwamba Kanisa linajua jinsi ya kuheshimu tamaduni, changamoto ya Umwilisho".

Hija ya Kitume ya Baraza la Maaskofu Nchini Brazili
Hija ya Kitume ya Baraza la Maaskofu Nchini Brazili

Kukabiliana na changamoto wanayokabiliana nayo leo hii kama vile uhaba wa makasisi, matatizo ya kiuchumi, suala la hali ya kukata tamaa ya kutoheshimiwa kwa wakazi wa kwanza wa ardhi yaani Watu asilia wa Msalaba Mtakatifu wanaoishi huko, ambapo Papa alitumia usemi kwamba “chukua hatari ndugu zangu msipojihatarisha tayari mnafanya makosa'. Kwa maneno mengine, amewathibitishia kwamba hawapaswi kuogopa pia kuchukua changamoto mpya, kuishi zaidi ya yote kwa uaminifu kwa maskini. [...] Pia aliwaomba wawe wachungaji, sio warasimu; wachungaji wenye harufu ya kondoo na ukaribu na watu. Kwa upade wa Askofu Lúcio Nicoletto, msimamizi wa Jimbo katoliki la Roraima, amesema  kwamba Papa Francisko aliwahimiza Maaskofu kutenda bila hofu ya kukabiliana na changamoto ambazo wakati wa sasa zipo, ambazo zinahitaji neno la kinabii kutangaza matumaini ya Injili ya maisha, lakini pia kukemea kila kitu kinachokanyaga chini ya miguu ya haki za kimsingi za watu wa kiasilia na utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja.

Hija ya Kitume ya Baraza la Maaskofu Nchini Brazili
Hija ya Kitume ya Baraza la Maaskofu Nchini Brazili

Kupitia mkutano huo wa kibinadamu na wa kindugu, Maaskofu wakihimizwa kuwa karibu kila siku na wa mwisho na bila hofu ya kuchukua hatari, Askofu Mkuu Roque alisema kwamba Papa alizungumza tena juu ya Mkutano wa Aparecida wa 2007, ulioleta pamoja Maaskofu wa Amerika ya Kusini na ya visiwa vya Carribien na jinsi alivyovutiwa na mengi yaliyosemwa kuhusu suala la ikolojia wakati huo. Mbali na Maaskofu wa Amazonia, Askofu Mkuu wa Porto Velho alitoa maoni kwamba  Waraka wa  Papa wa Laudato si' ulimsaidia kuchukua hatua hiyo ya  kuelekea umuhimu wa mada, kama vile Sinodi ya Maaskofu wa Amazonia mnamo 2019  na kutoa Wosia wa  Querida Amazonia, yaani Mpendwa Amazonia.

Hija ya Kitume ya Baraza la Maaskofu Nchini Brazili
Hija ya Kitume ya Baraza la Maaskofu Nchini Brazili

Querida Amazonia' ni kukumbatia huku kwa upole na mapenzi ambayo aliichukulia sio tu kwa suala la bioanuai ya Amazon, lakini utunzaji na hata aliweza kutumia usemi huu naye wa Bustani ya Mungu, ya nyumba ya pamoja, wasiwasi kwa vizazi vijavyo. Kwa hiyo, Papa  Francisko alionesha, kwa njia hiyo, dhamira hii na uwazi huu kwamba hawawezi kuacha kile ambacho ni dhamira yao ya kuitunza bustani hiyo waliyokabidhiwa, bali si kwa ajili yao tu, na alisisitiza mara tatu umuhimu wa wao kujifunza kila siku kutoka kwa watu wa asili, kutoka kwa watu wa kiasili, uhusiano huu wa usawa na heshima na uumbaji, kuishi imani inayofumbatwa katika uhalisia huu mahali walipo; aidha kutotaka kurejea mpango wa ukoloni, bali, kinyume chake, ni kuingia na kuzama katika tamaduni na hilo  lilikuwa zuri sana, alisistiza Askofu.

Hija ya Kitume ya Baraza la Maaskofu Nchini Brazili
Hija ya Kitume ya Baraza la Maaskofu Nchini Brazili

Mchoro wa 'SOS Yanomami' uliotolewa kwa Papa

Kwa mujibu wa Askofu Lucius, mkutano wa pamoja na Papa uliwajaza moyo baada ya changamoto nyingi katika utume unaohitaji sana na Papa alionekana kusubiri kuwatia moyo na kuwakaribisha na, kwa mara ya kwanza, bila kuvuta sikio, alitania.. Kwa niaba ya watu wa Roraima, Askofu alimpatia Papa mchoro uliotayarishwa mwaka 1989 na msanii wa ndani, Cardoso, ambaye kwa miaka mingi alichora mateso na matumaini ya watu wa Amazonia. Mchoro wa kazi aliyopewa Papa Francisco ni ishara Nisaidie yaani SOS Yanomami, mojawapo ya makabila makubwa zaidi katika Amazonia, ambayo wakati huo yalikuwa yakikemea mateso ya wenyeji wa eneo hilo kwa sababu ya kukanyagwa haki na masuala kama vile uchimbaji madini, ukataji miti hovyo, ukosefu wa utunzaji wa mazingira na ukosefu wa heshima kwa idadi ya watu.

Hija ya Kitume ya Baraza la Maaskofu Nchini Brazili
Hija ya Kitume ya Baraza la Maaskofu Nchini Brazili

Kwa kuhitimisha amesema: “Leo, baada ya miaka 33, hali hii inabakia kuwa ya hali ya kutisha,  mfumo wetu wa maisha. Papa Francisko, kwa hiyo, ametoa wito kwa kila mtu kupitia upya mtindo wao  wa kuishi, kuanzia utamaduni unaoheshimu nyumba yetu ya pamoja”.

Mahojiano na Vatican News kuhusu mkutano wa Papa na maaskofu wa Brazili wakiwa katika hija ya kitume Vatican.
21 June 2022, 16:49