2022.06.23 Washiriki wa Mkutano Mkuu  wa 95 wa shughuli za kutoa Msaada wa Makanisa ya Mashariki (ROACO) 2022.06.23 Washiriki wa Mkutano Mkuu wa 95 wa shughuli za kutoa Msaada wa Makanisa ya Mashariki (ROACO) 

Papa amekumbusha majanga ya vita duniani:salini ili njia ya amani ipate nafasi

Papa Francisko akiwahutubia wawakilishi wa ROACO,shirika la Kanisa linalotoa misaada na usaidizi kwa Wakristo wa Mashariki ya Kati wamewaalika wasiache kusali, kufunga, kusaidia na kufanya kazi ili njia za amani ipate nafasi katika msitu wa migogoro.Na mtindo wa Sinodi umewaongoza hata katika Mkutano maalum wa Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya Nchi za Mashariki ya Kati.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano Mkuu wa 95 wa ROACO wakiwa katika hitimisho la Mkutano wao ambapo amempa Salamu Kardinali Sandri, Zenari na wangine wawakilishi wa Mabaraza ya Kipapa, mashirikia Makuu na maafisi wote ambao kupitia wao ambao kila nchi wanapata uwezekano wa ukarimu wao. Kila mmoja ana jukumu na anaitwa kufanya mazungumzo na wengine kwa kushauriana, kusoma, kuuliza na kutoa mapendekezo na maelezo, kutembea pamoja. Zana za TEHAMA ambazo zinatayarishwa na afisi zao zitafanya mchakato kuwa mzuri zaidi, lakini ni muhimu ziunge mkono mkutano na majadiliano ambayo umekomaa kwa miaka mingi, na kusaidia kukuza ulinganifu wa upendo pamoja. Wakati Bendi inapofanya kazi muhimu, kabla ya kuanza ni lazima tune za vyombo zijaribiwe. Ni kwa njia hiyo utendaji utastahili na kufunua ujuzi wa wanamuziki. Baba Mtakatifu amesema katika kuanzisha ulinganifu wa upendo, waendelea kutafuta maelewano na kukimbia jaribu lolote la kujitenga na kufungwa ndani yao na katika vikundi vya watu binafsi, ili kubaki wazi kuwakaribisha wale kaka na dada ambao Roho amewapendekeza kuanzisha uzoefu wa ukaribu na huduma kwa Makanisa Katoliki ya Mashariki, katika nchi mama na pia katika maeneo ya wale wanaoitwa.

Mkutano wa ROACO
Mkutano wa ROACO

Na ili  kukubaliana, na kusikilizana, ni muhimu kwani  hurahisisha utambuzi na ambao unapelekea chaguzi za pamoja, za kweli za kikanisa. Hivi ndivyo walivyofanya, kwa mfano, na Baraza la Maaskofu Katoliki Siria, katika Kongamano lililofanyika huko Damascus mwezi Machi uliopita na ambalo vijana wengi walishiriki kikamilifu. Katika jangwa la umaskini na hali ya kukata tamaa iliyosababishwa na miaka kumi na miwili ya vita huko Siria inayopendwa na kuteswa, umeweza kugundua ukiwa Kanisa kwamba chemchemi za kufanya nyika kuchanua na kutoa maji kwa wenye kiu zitabubujika tu,  ikiwa kila mmoja anajua jinsi ya kuacha ubinafsi fulani na kusikiliza wengine ili kutambua vipaumbele vya kweli. Bila shaka, haya ni matone katika bahari ya hitaji, lakini tone la Kanisa haliwezi kukosa, wakati jumuiya ya kimataifa na mamlaka mahalia daima zinatarajiwa kuzima moto wa mwisho wa matumaini kwa watu hao wanaoteseka.

Mkutano wa ROACO
Mkutano wa ROACO

Baba Mtakatifu Francisko amewambia kwamba mtindo wa sinodi umewaongoza hata katika Mkutano maalum wa Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya Nchi za Mashariki ya Kati. Mwezi Septemba ujao itakuwa ni mwaka wa kumi wa Wosia wa Kitume wa Kanisa la Mashariki ya Kati, uliochapishwa na Mtangulizi wake Papa Mstaafu Benedikto XVI wakati wa ziara yake ya Kitume nchini Lebanon. Katika miaka kumi mambo mengi yametokea. Kwa kufikia matukio yenye huzuni ambayo yameikumba nchi ya Iraq na Siria, mabadiliko ya nchi ya Lebanon.   Kumekuwapo na hata nuru za matumaini, kama vile kutiwa saini katika  Hati ya Abu dhabi, kuhusu Udugu wa kibinadamu. Lakini itakuwa lazima kuhakikisha juu nyanza za matunda ya Sinodi kwa ajili ya Nchi za Mashariki. Lakini zaidi ya hayo inabidi kutafuta zana ya kusasisha na mtindo stahiki kwa ajili ya kuelezea ukaribu wa Makanisa ya Kanda. Ni matarajio mema zaidi ya Baba Mtakatifu kwamba kuweza wao kuanza kazi juu ya meza ya uratibu juu ya Siria na Iraq iliyoanzisha miaka kadha kwa kuweka hata Lebanon katika tafakari ya pamoja.

Mkutano wa ROACO
Mkutano wa ROACO

Baba Mtakatifu Francisko aidha amewaomba pia wazingatie na kutazama picha ya Msamaria Mwema. Walelelezea na anatambua wanavyopendelea kufanya hata katika majanga yaliyosababishwa na ambayo huko Tigray yamejeruhi kwa upya nchini Ethiopia na sehemu ya karibu na Eritrea, na  hasa kwa ajili ya nchi pendwa na inayoteseka ya Ukraine.  Hapo kumerudi tena tukio la Kaini na Abeli. Zimeibuka vurugu ambazo zinaharibu maisha, vurugu za moto, hatari ambazo “sisi kama waamini tunaalikwa kutenda kwa nguvu za sala, kwa msaada wa dhati wa upendo, kwa kila zana ya kikristo ili silaha ziweze kuacha nafasi ya mchakato wa mazungumzo”. Papa Francisko amependa kuwashukuru kwa mchango ambao unapeleka bembelezo kwa Kanisa na Papa nchini Ukraine na nchi nyingine ambazo zinawakaribisha wakimbizi. Katika imani amesema tunajua kuwa majivuno ya mwanadamu yatainamishwa, na kiburi cha watu kitashushwa na kwamba “taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.”(Is 2,4). Kwa sasa utafikiri ni kwenye kinyume kwani  mwelekeo ni tofauti, kwa sababu chakula kinapungua na milio ya vita inaongezeka.

23 June 2022, 17:54