Misa ya Jumuiya ya Congo jijini Roma 2019 Misa ya Jumuiya ya Congo jijini Roma 2019  

Papa amepokea tafsiri ya Kifaransa ya kitabu kuhusu Misale ya Waamini wa Congo

Papa Francisko ameandika utangulizi wa katika tafsiri ya Kifaransa ya kitabu kiitwacho Papa Francisko na Misale ya Kirumi kwa Majimbo ya Zaire", kilichoandikwa na Sr Rita Mboshu Kongo na kuhaririwa na Nyumba ya kuchapisha Vitabu Vatican.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika fursa ya uwakilishi wa kitabu chenye kichwa:“Le Pape François et le Missel Romain pour les Diocèses du Zaïre",  yaani: " Papa Francisko na Misale ya Waamini ya Kirumi kwa ajili ya majimbo ya Zaire", kilichochapishwa na Nyumba ya Vitabu Vatican, Papa Francisko amewatumia ujumbe washiriki, katika uwasilishaji wa kitabu hicho, uliofanyika katika Ukumbi wa Marconi, makao makuu ya Radio Vatican, Jumatatu tarehe 20 Juni 2022. Katika ujumbe huo Papa Francisko anafurahi na kukaribisha kuingia katika mawasiliano na wao kwa ajili ya tukio muhimu la Kanisa, Familia ya Mungu ambalo ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Uwakilishi wa tafsiri ya kifaransa, chini ya usimamizi wa Sr. Rita Mboshu Kongo, kinajikita katika muktadha wa maandalizi ya ziara yake katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, katika nyayo za  mtangulizi wake Mtakatifu Yohane Paulo II.  Papa amesema, inawezekanaje kutokumbuka kile alichokuwa amesema Mtakatifu Yohane Paulo II kwa Kanisa la Afrika kwamba:“ Katika Nchi yenu ya Kiafrika, imepyaishwa Pentekoste ya Yerusalemu.”  

Mababu walisikia habari njema na kuinamisha vichwa kwa ubatizo katika roho

Mababu zetu walisikia ujumbe wa habari Njema, ambayo ni lugha ya Roho. Mioyo yao ilipokea kwa mara ya kwanza neno hili na kuinamisha kichwa katika maji kwenye kisima cha ubatizo, ambapo mtu kwa njia ya Roho Myakatifu anakufa pamoja na Kristo msulibiwa na kuzaliwa kwa upya maisha katika ufufuko wake (…) Ilikuwa kweli kwa hakika Roho mwenyewe aliyesukuma watu wa imani, wamisionari wa kwanza ambao mnamo 1491 walianza kuvuka mto Zaire, huko Pinda kwa kutoa mwanzo wa kweli na wa umisionari. Iliwa tena ni Roho Mtakatifu aliyetenda kwa namna yake katika moyo wa waamini ambao ulimsukuma mfalme Nzinga-a-Nkuwu wa Congo kuwahamaisha wamisionari kufika ili kutangaza Injili” (taz. Ecclesia in Africa, n. 32). Baba Mtakatifu Francisko amebainisha katika ujumbe huo kwamba kiukweli mkristo angekuwa na thamani gani zaidi ya imani yake katika Yesu Kristo? Imani hii sio labda tunu kubwa ambayo imerithishwa kwa kizazi kilichotangulia na ambacho kinapaswa kuendelea kurithisha kwa kizazi kijacho? Kwa maana hiyo inaelewaka uhusiano mzuri wa imani, kwa sababu yaliyomo, yanaunda imani na wakati huo huo mtindo ambao imani ya watu inajifafanua kwa tamaduni yao ya ibada.

Ibada ya Congo ni tunda la mahubiri ya kimisionari

Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu Francisko anakaribisha tafsisi ya lugha ya kifaransa na kwamba Ibada ya Congo katika maadhimisho ya Ekaristi kwa hakika ni tunda la mahubiri ya kimisionari chini ya jua la Afrika na linalokaribishwa katika machweo.  Katika imani yake mara tatu ya imani, na ya utamaduni wa kitume, kwa asili ya kina ya liturujia katoliki yenyewe na hatimaye, ugwiji wa dini na urithi wa utamaduni wa Afrika na Congo ‘Missel Romain pour les Diocèses du Zaïre’ yaani Misale ya waamini kwa majimbo ya Zaire ni moja ya misale ya kiroma ya “utamadunisho” iliyozaliwa kwa njia ya mageuzi ya Liturujia ya Mtaguso wa II wa Vatican. Ni tunda la miaka mingi ya utafiti, ya matumaini katika eneo na tunda la ushirikiano kati ya Vatican na Kanisa mahalia la Congo. Inawezekana kuthibitisha ukweli wa kichwa ambacho kipo katika misale hiyo na kueleza kamili malengo ambayo yamekusudiwa. Kwa hakika inaruhusu Wakongo kusali katika lugha yao, kwa miili yao na roho yao na kutumia alama ambazo ni za kifamilia.

Makanisa mengine ambayo bado yanatafiti, yanaweza kuiga mfano huo

Mnamo tarehe 30 Aprili 1988, Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti lilirudia na kuthibitishwa Misa ya kawaida kwa lugha ya kifaransa pamoja na, kama nyongeza, utangulizi, kalenda na Misa.  Kwa maana hiyo Papa Francisko amethibitisha kwamba anapendekeza ibada ya Congo katika maadhimisho ya Ekaristi, iwe kama mtindo kwa ajili ya Makanisa mengine ambayo bado yanatafiti kuwa na kielelezo cha kiliturujia kinachofaa kwa ajili ya kupeleka ukomavu wa matunda  ya kazi ya kimisionari ya uinjilishaji wa tamaduni na utamadunisho wa Injili. Kwa kuongezea amebainisha kwamba: “Sio vema kudharau kwa uamuzi muhimu ambao unajivika katika utamaduni uliomo katika imani, kwa sababu utamaduni wa uinjilishaji, mbao pamoja na vikwazo vyake, una rasilimali zaidi, kwa urahisi mwingi wa waamini kukabiliwa na mashambulizi ya ulimwengu mamboleo. Utamaduni mmoja wa watu wa kuinjilisha una thamani ya imani, na ya mshikamano ambayo unaweza kuibua maendeleo ya jamii yenye haki zaidi na aminifu na ina hekima muhimu sana ambayo inatakiwa kujua kwa mtamzamo uliojaa shukrani (Evangelii gaudium, n. 68).

Ufanisi mwema wa kusoma kitabu na kuadhimisha maajabu ya Mungu

Papa Francisko kwa kuhitimisha ujumbe wake amewashauri kama alivyokuwa akisema Mtakatifu Yohane Paulo II mnamo tarehe 23 Aprili 1988 kwa Maaskofu wa Congo wakati wa hija yao ya kitume (in visita ad limina Apostolorum) ya kujibidhisha na wakati huo huo kwa pamoja na ibada za Sakramenti na visakramenti ambavyo walikuwa wanaandaa ili kutafakari ibada hiyo”. Papa Francisko amewatakia ufanisi mwema katika kusoma kitabu hicho ili kuelewa kwamba ni vema kuadhimisha pamoja maajabu ya Mungu wetu katika Mwanae Yesu Kristo, Bwana wetu.

Ujumbe wa Papa kuhusu kitabu kinachohusu Misale ya Waamini wa Congo kwa lugha ya kifaransa
20 June 2022, 17:57