Papa kwa Charis:Amani inaanzia ndani ya familia!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake kwa njia ya Video, kwa washiriki wa mkesha wa Pentekoste, usiku wa tarehe 4 Juni 2022 wakiomba nguvu ya Roho Mtakatifu, iwashukie katika maadhimisho ya Pentekoste. Baba Mtakatifu Francisko amesema:“Katika kitabu cha Matendo ya Mitume, inasomeka kuwa mara baada ya ufufuko, wakati wa siku zile arobaini, aliwatokea wao na kuzungumza nao kuhusu Ufalme wa Mungu. Siku moja wakati anakula pamoja nao, aliwaamuru wasiende mbali na Yerusalemu, lakini wasubiri ahadi ya Baba ambayo alikuwa amewambia: “Yohane alibatiza kwa maji; siku chache zijazo, mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu”. Na mbele akaongeza: Roho Mtakatifu atakapokuja, atashuka juu yenu, mtapokea uwezo na mtakuwa mashuhuda wangu huko Yerusalemu na Galilaya Yote na Samaria hadi miisho ya dunia”.
Uzoefu wa nguvu ya Roho Mtakatifu
Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na ujumbe wake amesema: “Usiku kama wale leo hii, wale wanawake na wale wanaume waliokuwa na woga, wamejifungia katika Chumba cha Karamu Kuu huko Yerusalemu, kwa sababu walikuwa wanajua wanavyoteswa, waliweza kufanya uzoefu wa nguvu ya uwepo wa Roho Mtakatifu, ambaye aliwawabadili maisha yao daima. Na maisha yao yaliyobadilishwa na nguvu ya Roho ilibadili historia. Usiku huu katika ulimwengu, wakristo wote tumeunganika katika sala kwa kusubiri ahadi ya Baba, ujio wa Roho Mtakatifu. Tunamsubiri kwa sababu hakuja kwa kuwa hakuwapo. Hapana. Alikuwapo tayari wakati wa uumbaji na yupo kwa wote, kwa njia ya Ubatizo tuliopokea” . Papa amesema: “Kila mwaka, katika Mkesha wa Pentekosta, tunataka kuwa na uzoefu ule ule walioishi na uhakika wa uwepo wake katikati yetu, katika maisha yenyewe na katika jumuiya zetu”.
Magonjwa na vita, njaa
Ni uhalisi wa ulimwengu leo hii ambao umegubikwa na ugonjwa, janga la uviko ambalo limeondoa mamilioni ya watu ulimwenguni kote na kwa uchungu huo, mateso na ukosefu. Na hata katika pande nyingi za dunia, njaa na watu wengi waliolazimika kuhama. Na vita pia vita kati ya ndugu, vita kati ya wakristo, kama ilivyo kesi ya wakati huu ya uvamizi huko Ukraine. Kuna mifano kama hii ya vita ulimwenguni kote, hata hali halisi huko Yemen, watu mashahidi wa Rohingya na kwa namna ya pekee miongoni mwake hali ya Lebanon … vita! Mbele ya kugubikwa ulimwenguni na hata hofu ya wakati ujao inaibuka katika usiku wa uwepo wa mwanga wa Roho Mtakatifu, ambaye anatupatia nguvu na kutupatia ujasiri na msimamo ili kufanya kazi bila kuchoka kwa ajili ya amani ambayo, peke yake anaweza kuitoa.
Amani inaanzia katika familia
Baba Mtakatifu Francisko akindelea na ujumbe wake kwa njia ya video amesema “Amani inaanzia katika familia, katika uhusiano binafsi, uhusiano kati ya Wakristo na wajumbe wa dini nyingine. Amani inaanza katika upendo kwa adui, kwa yule asiye fikiria kama mimi… Peke yetu hatuwezi. Kwa njia ya Roho Mtakatifu tunaweza”. Papa Francisko ameongeza: “Chuki utafikiri imechukua madaraka ulimwenguni sasa. Lakini kuna nguvu zaidi, ya uwezo wa chuki, ni nguvu ya upendo kwa sababu “… upendo wa mungu umemiminwa katika mioyo yetu kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye alitupatia” (Rm, 5, 5). Baba Mtakatifu Francisko amesema “Kesho kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, tutafute mtu huyo ambaye ametuhumiza, ambaye hatumpendi kwa namna tofauti, labda ni ndani ya familia zetu wenyewe, na tuombe msamaha, au tumsamehe na kumkumbatia. Ndivyo inaanza amani. Kidogo kidogo, moja kujumlisha moja.
Kueneza utamaduni wa amani
Utamaduni wa amani ambao tunapaswa kuueneza, unaanza namna hiyo. Viongozi wa serikali, watafanya kazi au kidogo kwa ajili ya amani, na watakuhumiwa kwa historia. Kila mmoja wetu anasubiriwa kueneza upendo na kushinda chuki kwa matendo yetu ya kila siku. Na watoto wetu watajifunza kuiishi na wajukuu watajifunza kutoka kwao, na hivyo tutaweza kufanya lolote ili ulimwengu upate kubadilika. Sisi sote tunaalikwa kuanza safari hiyo: Wakati Roho Mtakatifu anashuka juu yenu, anasema Bwana “Mtapokea nguvu na mtakuwa mashuhuda wangu huko Yerusaleme na Samaria hadi miisho ya dunia”. Hayo ndiyo matashi yangu kwenu, kwamba mpokee nguvu ya Roho Mtakatifu na muwe mashuhuda. Na Bwana awabariki”, amehitimisha Papa Francisko.