2022.06.20  Manuel mweusi,Mtumishi mwenye asili ya Capo Verde wa miaka ya karne ya kumina na saba ambaye historia yake inahusiana na ibada ya Bikira Maria wa  Lujan nchini Argentina. 2022.06.20 Manuel mweusi,Mtumishi mwenye asili ya Capo Verde wa miaka ya karne ya kumina na saba ambaye historia yake inahusiana na ibada ya Bikira Maria wa Lujan nchini Argentina. 

Papa Francisko:enendeni mbele kwa imani rahisi inayobadili historia

Papa Francisko amewatumia ujumbe kwa njia ya video Harakati ya Kimisionari ya Francisko katika fursa ya Kuzindua “Njia ya Kihistroai ya utamaduni wa Mweusi Manuel’ kwa Bikira Maria wa Luján.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kama sehemu ya maadhimisho kwa ajili ya heshima ya Bikira wa Luján, kumefanyika hija ya matembezi ya kihistoria na kiutamaduni iliyoangazwa na imani. Papa Francisko katika ujumbe wake kwa njia ya video kwa washiriki wa hija hiyo amewatumia Harakati ya Kimisionari ya Francisko akiwatakia matashi mema kwamba Bikira na awalinde, na Manuel Mweusi awaombee wote. Na waendelee, “kwa imani hiyo rahisi, kwa imani hiyo ambayo ni imani waliyopokea kutoka kwa wazazi wao, ni imani ya watu wetu. Imani ndiyo inabadilisha historia. Kwa maana hiyo “Bikira Maria wa Luján awalinde, na Manuel Mweusi ' awaoneshe njia”.

Ibada kwa Bikira Maria wa Lujan

Asili ya ibada kwa Bikira wa Lujan, ambayo ni picha ya Maria inayoheshimiwa zaidi huko nchini Argentina, ni tangu karne ya 17, ambapo inahusishwa na hisotria ya ‘Negro Manuel’, mtumishi wa asilia wa Capo Verde. Akiwa na umri wa miaka 25 aliuzwa na kupelekwa nchini Brazili katika huduma ya nahodha wa Ureno Andrea Juan. Katika nchi hiyo alibatizwa usiku wa Siku Kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana mnamo 1629. Miezi michache baadaye, Kapteni Juan aliondoka kwa ajili ya utume mwingine wa kupeleka  picha ya Bikira  Maria Msafi  kwenye Kanisa la Sumampa, katika mkoa wa Santiago ya Nje.

Papa Francisko amesisitiza mara nyingi Bikira Maria wa Lujan

Hata hivyo, anapotua Buenos Aires, akiwa na tume nyinginezo, alikabidhi kazi ya kukamilisha uwasilishaji kwa kutumia ardhi kwa mtumishi wake anayemwamini. Siku ya pili ya maandamano, ng'ombe waliokuwa wafungwa kwenye gari na sura ya Bikira walisimama ghafla na hawakutaka kuendelea na maandamano. Negro Manuel hakuwa na shaka yoyote: Mama yetu alichagua kuiacha hapo, Luján. Wakati wa Upapa wake, Papa Francisko mara nyingi amewashauri kuacha wasindikizwe katika safari ya maisha na Bikira wa Luján Msimamizi wa Argentina. Katika Katekesi ya tarehe 12 Mei 2021, hasa, Papa anakumbuka tukio la familia moja. Baba aliambiwa kwamba binti yake ni mgonjwa sana kutokana na maambukizi.

Muujiza wa kupona

Kwa upande wa madaktari walisema hataweza kuishi kwa usiku. Mwanamume huyo, akilia, aliwaacha mkewe na binti yake hospitalini. Akapanda treni na kufika kwenye Madhabahu ya Luján ambako alikesha usiku kucha katika sala. Kutokana na kwamba alifika wakati Kanisa Kuu lilikuwa limefungwa alishikilia gate la lango kuu na alisali usiku kucha na mapema asubuhi aliingia kwenye Kanisa Kuu na akamwelekea Mama. Tukio hilo haliwezi kufutika: “Niliona! Niliishi hivyo”, alisema wakati huo  Papa. Pambano la baba huyo katika maombi yalitangulia tabasamu lile la mke wake ambaye alimwambia, mara baada ya kurudi nyumbani, kwamba binti yake ameponywa kwa njia isiyoelezeka. “Mama yetu alimsikiliza”.  Sala kwa upande wa Papa alikumbuka wakati huo “kuwa hufanya miujiza”.

21 June 2022, 17:07