Papa Francisko:Shika njia ya safari kwa upendo mwaminifu wa familia
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Katika muktadha wa Mkutano X wa Familia duniani, huu ni wakati wa kushukuru. Kwa shukurani ambayo leo hii tunapeleka mbele ya Mungu, kama sadaka kubwa ambayo Roho Mtakatifu alipanda ndani yenu. Ndivyo Baba Mtakatitu Francisko ameanza tafakari yake kwenye misa kwa ajili ya Mkutano wa Familia Duniani iliyofanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vaticani kwa kuongozwa na Kardinali Kevin Farreli Rasi wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, Jumamosi jioni tarehe 25 Juni 2022, ambao ulianza tarehe 22 Juni kwa kuwaona zaidi wa washiriki elfu mbili wawakilishi wa majimbo mbali mbali kutoka mabara yote ulimwenguni. Na baada ya masomo yote, Baba Mtakatifu aliyeshiriki alitoa mahubiri hayo. Baba Mtakatifu Francisko akiendelea amebainisha juu ya baadhi yao walishirikisha vipindi vya tafakari ‘ jijini Vatican na zaidi walihuisha hata majimbo mbali mbali.
Papa Francisko amefikiria jinsi utajiri wa uzoefu, mapendekezo, ndoto na pia kutokosekana hata wasiwasi na ukosefu wa uhakika. Na hivyo muda huo ni kuwakilisha kwa Bwana na kumwomba Yeye aweze kuwasaidia kwa nguvu yake na upendo wake. Baba Mtakatifu amesema kwamba wao walikuwa ni mababa, mama, watoto, bibi na babu, na wajomba kwa namna nyingine ni watu wazima watoto, vijana, wazee na kila mmoja kwa uzoefu tofauti wa familia lakini wenye matumaini sawa yanayofanywa pamoja katika sala na Mungu abariki na kulinda familia zao na familia nzima ya ulimwengu. Baba Mtakatifu Francisko akidadavua somo la pili lililosomwa la Mtakatifu Paulo aliyezungumzia juu ya uhuru, amesema, uhuru ni moja ya mali msingi inayopendwa na kutafutwa na mtu wa kisasam wa mamboleo. Wote wanatamani kuwa huru, bila kuwa na masharti, kizingiti na hivyo kutaka kujiondoa na lolote la kufungwa na utamaduni, kijamii na kiuchumi. Lakini pamoja na hayo ni watu wangapi wanakosa uhuru mkubwa zaidi ule wa ndani.
Mtume anakumbusha kwa wakristo kwamba hiyo ni zawadi kubwa kwa maana anasema “ Kristo alitukomboa uhuru (Gal 5,1). Uhuru tulipewa. Sisi sote tunajua ni masharti gani tuliyo nayo, ya ndani na nje na hasa tabia ya ubinafsi, ya kujiweka katikati na kufanya tunavyotaka. Lakini utumwa huo tulikombolewa na Kristo. Wenzi wote wanaoundwa na familia, kwa neema ya Kristo waliofanya uchaguzi huo wa ujasiri wasitumie uhuru wao binafsi, lakini kwa kupenda watu ambao Mungu aliwaweka mbele yao. Badala ya kuishi kama kisiwa, wao wanapaswa kuwa katika huduma ya mmoja na mwingine. Na ndiyo maana ya kuiishi uhuru katika familia, kwani sio sayari au satelaiti inayosafiri katika njia yake. Familia ni mahali pa kukutana, pa kushirikishana, kutoka nje yao binafsi ili kukutana na kukaa karibu. Ni mahali pa kwanza pa kujifunza kupenda.
Baba Mtakatifu Francisko amesema kwamba wakati wao inaaminika kusema hilo, wanajua vema kuwa kwa vitendo daima sio hivyo, kwa sababu nyingi na hali nyingi. Kwa maana hiyo wakati wanathibitisha uzuri wa familia, wao wahisi kuliko hapo awali kwamba wanapaswa kuilinda. Wasiache ichafuliwe na sumu ya ubinafsi, utamaduni wa kutojali na upotevu,na hivyo kupoteza vinasababa (DNA) vyake ambavyo ni ukarimu na roho ya huduma. Uhusiano kati ya Nabii Elia na Elisha, unawakilisha katika somo la kwanza kufikiria uhusiano kati ya kizazi, hatua ya ushuhuda, kati ya wazazi na watoto. Uhusiano huo katika ulimwengu wa sasa sio rahisi na mara nyingi ni sababu ya wasi wasi. Wazazi wanaogopa kwamba watoto hawatakuwa na uwezo wa kijielekeza katika ugumu na katika mkanganyiko wa jamii zetu, mahali ambamo inaonekana machafuko na hatari, na kwamba hatimaye wanapoteza njia yao. Hofu hii huwafanya wazazi wengine kuwa na wasiwasi, wengine hulinda kupita kiasi, na wakati mwingine hata huishia kuzuia hamu ya kuleta maisha mapya ulimwenguni.
Papa kwa maana hiyo amesisitiza kwamba itakuwa vizuri kutafakari kwa kina kati ya Elia na Elisha. Elia katika wakati wa mgogoro na hofu ya wakati ujao alipokea kutoka kwa Mungu amri ya kumpaka mafuta Elisha kama mfuasi wake. Mungu alimfanya Elia kutambua kuwa ulimwengu hauishi na yeye na akamuamru arithishe mwingine utume wake. Hiyo ndio maana ya andiko hilo kwamba Elia alimvika mabegani Elisha vazi lake na kwa wakati huo ,mfuasi akachukua nafasi ya Mwalimu wake ili kuendelea na huduma ya kinabii huko Israeli. Mungu anaonesha hivyo kuwa na imani kwa kijana Elisha. Jinsi gani ilivyo muhimu kwa wazazi kutafakari kwa namna ya kutenda kwa Mungu! Mungu anawapenda vijana, lakini si kwamba wanaondolewa hatari, kila aina ya changamoto na kila teso. Yeye hana wasiwasi na kulinda kupita kiasi; kinyume chake anayo imani kwao na anawaita kila mmoja kadiri ya kipimo cha maisha yao na wa utume. Kwa kutoa mfano Papa ameomba kufikiria mtoto Samueli, kijana Daudi, kijana Yeremiah; na hasa kwa kufikiria Bikira Maria. Kwa maana hiyo Neno la Mungu linaonesha njia; si kuwahifadhi watoto na kila usumbufu na mateso, bali kujaribu kuwapitishia shauku ya maisha, kuwasha ndani yao hamu ya kupata wito wao na kukumbatia utume mkuu ambao Mungu amewawazia.
Kwa hakika katika ugunduzi huo, ndio ulimfanya Elisha awe jasiri, shupavu na kumfanya akomae. Kuondokana na wazazi na kuuawa kwa wanyama ndio ishara ambayo Elisha alielewa kwamba sasa ni yeye wakati huo kupokea wito wa Mungu na kuupeleka mbele kwa kile ambacho alikuwa ameona anafanya mwalimu wake. Na alifanya kwa ujasiri hadi mwisho wa maisha yake. Baba Mtakatifu amewaomba wazazi wawasaidie watoto wao kugunda na kupokea wito wao, wataowaona wao wanachukuliwa katika utume huo na watakuwa na nguvu ya kukabiliana na kushinda matatizo ya maisha. Papa Francisko amependa pia kuelekeza kwa mwalimu, namna nzuri ya kusaidia mwingine ili afuate wito wake. Hii ni kukumbatia kwa upendo binafsi na mwaminifu. Ndicho wafusi waliona Yesu akifanya na katika Injili iliyosomwa imeonesha wakati mkuu ambapo Yesu alichukua uamuzi stahiki wa kujiweka katika safari kuelekea Yerusalemu (Lk 9,51) kwa kutambua vema kwamba kutakuwa na kuhukumiwa na kuuawa.
Yesu akiwa katika nia ya Yerusalemu, alipata kukataliwa na wakazi wa Samaria, kukataliwa huko ambako kulisababisha kukasirika kwa Yakobo na Yohane, lakini Yesu alikubali kwa sababu ni sehemu ya wito wake. Tangu mwanzo alikuwa amekataliwa Nazareth, na sasa Samaria na mwisho atakataliwa huko Yerusalemu. Yesu anakubali yote kwa sababu alikuja kuchukua dhambi zetu. Na wakati huo huo hakuna kitu kilicho kizuri zaidi kwa watoto ambao wanaona wazazi wao wakiishi ndoa yao na familia yao kama utume, kwa uaminifu, uvumilivu, licha ya matatizo, wakati wa huzuni na majaribu. Kilichomtokea Yesu huko Samaria, ndicho kinajitokeza kwa kila wito wa mkristo, hata kwa familia. Kuna vipindi ambamo ni lazima kujichukulia mwenyewe upinzani, kufungwa, kutoelewana kutokana na moyo wa mwanadamu na kwa neema ya Kristo, kuwageuza kuwa wakaribishaji wa wengine, katika upendo wa bure.
Mara baada ya tukio hilo, ambalo linaeleza kwa maana nyingine wito wa Yesu, Injili inawakilisha mialiko mitatu. Baba Mtakatifu amesema mwaliko wa kwanza ni ule ambao Yesu anasema: kutotafuta makao thabiti, mahali pa usalama wakati wa kufuata Mwalimu. Yeye kiukweli hajui mahali pa kulaza kichwa chake ) Lk 9,58). Ni kufuata Yesu na kujiweka katika mwendo na kubaki katika mwendo wa safari ya Yeye kwa njia ya matukio ya maisha. Hiyo ni kweli kwa wanadoa, Papa amesisitiza kwani “ wao kwa kupokea wito wa ndoa na wa familia waliacha kiota chao na wakaanza mchakato wa safari ambayo wasingeweza kutambua kwanza kwa hatua zake zote, na ambapo unawadumisha katika mwendo wa kuendelea, kwa hali mpya daima, kwa matukio yasiyotarajiwa na mishangao. Ndivyo ilivyo safari ya Bwana. Ni mwendo, usio tarajiwa na ambao unafikia kugundua kwa mshangao. Baba Mtakatifu amewahimiza wakumbuke kuwa pumziko la kila mfuasi wa Yesu ndilo hilo la kufanya kila siku mapenzi ya Mungu, kwa lolote liwe!
Wito wa mfuasi ambao anaalikwa ni kutorudi nyuma ili kuzika wafu ( Lk 9, 59-60). Hii haina maana ya kwenda kinyume na amri ya nne, ambayo inabaki daima kufaa kabisa; badala yake ni mwaliko wa kutii, awali ya yote amri: kumpenda Mungu zaidi ya kila kitu. Na ndiyo wito wa tatu kwa mfuasi anayealikwa kufuata Kristo kabisa kwa moyo wote bila kugeuka nyuma na wala kwenda kuwaaga famila zake ( Lk 9,61-62). Baba Mtakatifu Francisko ameeleza familia zote kwamba wao wanaalikwa wasiwe na vipaumbele vingine na wala kurudi nyuma, kwa maana ya kulilia maisha ya kwanza, uhuru wa kwanza, na madanganyo yake: maisha hubadilika wakati hayakaribii mapya ya mwito wa Mungu, na yakijutia yaliyopita. Lakini Yesu anapita, hata katika maisha ya ndoa na ya familia, anaomba kutazama mbele na daima anawatangulia katika mchakato wa safari, anawatangulia katika upendo na katika huduma. Anayemfuata hawezi kukatishwa tamaa.
Masomo ya liturujia kwa maana hiyoyanapendekeza wema, yanazungumza wito ambao ndiyo hasa wa kauli mbiu iliyoongoza Mkutano wa X wa Familia Duniani isemayo “ Upendo wa Familia: wito na njia ya Utakatifu. Kwa nguvu ya Neno la Maisha, Papa anawatia moyo wa kuchukua safari kwa uaminifu wa upendo wa familia, kuushirikisha na wajumbe wote wa familia kwa furaha ya wito huo, unaotoka, wenye uwezo wa kugusa walio dhaifu na waliojeruhiwa ambao wanakutana nao njiani, wadhaifu katika mwili na wadhaifu katika roho. Upendo kiukweli hata wa familia unatakasa na kuongezeka nguvu wakati wa kuutoa. Kanisa lipo nao na zaidi Kanisa pamoja nao, kwani kiukweli lilizaliwa na Familia, ile ya Nazaret na kimsingi, limetengenezwa na familia. Bwana awasaidie kila siku kubaki katika umoja, katika amani, furaha kwa kuwaonesha wote kuwa Mungu ni upendo na muungano wa maisha.