Tafuta

2022.06.25 Papa Washriki wa Mkutano Mkuu wa Wana wa Mpaji na Familia ya Karama ya Mtakatifu Orione 2022.06.25 Papa Washriki wa Mkutano Mkuu wa Wana wa Mpaji na Familia ya Karama ya Mtakatifu Orione  

Papa Francisko:Jitupeni katika moto wa nyakati mpya kwa mafao ya watu

“Na tufanye ishara ya msalaba na kujitupa kwa uaminifu katika moto wa nyakati mpya kwa ajili ya wema wa watu.”Ni Maneno ya Mtakatiu Orione mwanzilishi wa Shirika la Wana wa Mapaji ambao wamekutana na Papa katika fursa ya kuadhimisha miaka 150 ya kuzaliwa kwake.Amewaomba moto usibaki tu katika nyumba yao,jumuiya zao na si hata katika kazi zao,bali waweze kujitupa ndani ya moto wa nyakati mpya kwa manufaa ya watu.

Na Angella Rwezaula- Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Familia yak arama ya Shirika la Mtakatifu Luigi Orione wakiwa katika maadhimisho ya miaka 150 tangu kuzaliwa kwa mwanzilishi huyo. Amemshukuru Mkuu wa Shirika ambaye amechaguliwa kwa mara nyingine tena kuliongoza  shirika la Mungu Mpaji na washiriki wote wa Familia ya karama ya Orione. Ni kishina kimoja chenye matawi mengi, kilichoundwa na watawa wa kike na kiume, walio wekwa wakfu na Walei wote wakiwa wanamwilishwa na karama moja ya Mtakatifu Luigi Orione ambaye mwaka huu amefikisha miaka 150 ya kuzaliwa mnamo tarehe 23 Juni 1872 huko Alexandria. Ninashukuru Bwana pamoja nanyi ambaye kutokana na mbegu hiyo kama Injili inavyosema alifanya kukuza mmea mkubwa, ambao unawapa makaribisho, malazi na kiburudisho kwa watu wengi, hasa wale wenye uhitaji zaidi na wasio na furaha. Na wakati mnashukuru na kusherehekea, nguvu ya karama ikiwa hai, muhisi kujitoa kunakohitaji kuwa wafuasi na wanafamilia wa ushuhuda mkuu wa upendo wa Kristo; kujitoa kufanya sasa, kwa maisha yenu na hatua yenu, moto wa upendo huu katika ulimwengu wa leo, unaoangaziwa na ubinafsi na utumiaji, ufanisi na mwonekano.

Papa amekutana na Familia nzima ya karama ya Mtakatifu Luigi Orione
Papa amekutana na Familia nzima ya karama ya Mtakatifu Luigi Orione

Papa Francisko ametumia maneno hayo na kusema kuwa  ndivyo alivyoandika Padre Orione mwanzoni mwa karne ya ishirini na kwamba: “Tunaishi katika karne ambayo imejaa baridi na kifo katika maisha ya roho; yote yakiwa yamejifungia nafsi yake, haioni lolote zaidi ya anasa, ubatili na matamanio na maisha ya dunia hii, na si zaidi”. Na alikuwa anajiuliza Je  ni nani atakayehuisha kizazi hiki kilichokufa kwa uzima wa Mungu, ikiwa si pumzi ya upendo wa Yesu Kristo? [...] Kwa maana  hiyo hatuna budi kumwomba Mungu sio cheche moja ya upendo, [...] bali tanuru ya upendo ili itutie moto na kufanya upya ulimwengu wa baridi, kwa msaada na neema ambayo Bwana atatupatia. Baba Mtakatifu Francisko amesema wao kama wanashirika wa Mungu Mpaji, kama mada ya Mkutano wao Mkuu uliohitimishwa hivi karibuni  walikuwa wamechagua usemi wa mfano wa bidii ya kitume ya Padre  Orione kwamba “Na tufanye ishara ya msalaba na kujitupa kwa uaminifu katika moto wa nyakati mpya kwa ajili ya wema wa watu.” (Maandiko 75, 242).  Kwa njia hiyo  Papa amewaomba kwamba moto usibaki tu katika nyumba yao na katika jumuiya zao, na si hata katika kazi zao tu, bali waweze kujitupa wenyewe ndani ya moto wa nyakati mpya kwa manufaa ya watu.

Papa amekutana na Familia nzima ya karama ya Mtakatifu Luigi Orione
Papa amekutana na Familia nzima ya karama ya Mtakatifu Luigi Orione

Baba Mtakatifu amesema Yesu alisema kuwa: "nimekuja kutupa moto duniani na ninataka uwe umewaka (Lk 12,49) Bkwa maana hiyo moto wa Kristo ni moto mzuri sio wa kuharibu kama alivyokuwa akitaka James na Yohane wakati walipomwambia “ Bwana unataka tusema kwamba moto ushuke toka mbinguni na kuchoma kila kitu (Lk 9, 54). Lakini Yesu aliwakaribiwa ndugu hao wawili. Mtot wake ni wa upendo, moto ambao unawasha mioyo ya watu, moto ambao unatoa nuru, unapasha na kuuisha. Kwa kiasi ambacho wanawaska upendo wa Kristo katika wao, uwepo wap na matendo yao yanakuwa muhimu kwa Mungu na kwa watu kama alivyoandika Mtakatifu Orione kwamba: “sababu ya Kristo na ya Kanisa haipaswi kuhudumiwa upendo mkubwa wa maisha bila matendo, upendo unafungua maisha ya imani na kupasha mioyo ya upendo kuelekea Mungu. Matendo ya moyo na upendo wa Kikristo ndiyo unawaaka na ndiyo wa waamini".

Baba Mtakatifu Francisko amesema kiukweli katika mkutano wao Mkuu wameweka kiini cha upyaisho wa uhusiano na Mungu, na moyo wa utambulisho wao. Moyo unaongezeka kwa kupokea kutoka kwa Mungu na maisha ya sala, tafakari ya Neno, na neema ya Sakramenti. Padre Orione alikuwa mwanaume wa matendo, na wa kutafakari. Kwa njia hiyo alikuwa anashauri kuwa “Hebu tujitupe chini ya miguu ya Tabernakulo” na pia: “Tujitupe chini ya msalaba”, kwa sababu “kumpenda Mungu na kuwapenda ndugu zetu ni miali miwili ya moto mmoja mtakatifu”. Baba Mtakatifu Francisko amesema leo wanafunzi wa kimisionari, hutumwa na Kanisa, si kuanza kufanya kitu, kwana shughuli yake ni utambulisho wa kitume unaoendelea kurutubishwa katika maisha ya kidugu ya jumuiya ya kitawa au ya familia. “Walipo wawili au watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo  kati yao” (Mt 18:20). Ni muhimu kutunza ubora wa maisha ya jumuiya, mahusiano, na sala ya kawaida: hii tayari ni utume, kwa sababu ni ushuhuda.

Papa amekutana na Familia nzima ya karama ya Mtakatifu Luigi Orione
Papa amekutana na Familia nzima ya karama ya Mtakatifu Luigi Orione

Papa  Francisko amesema “Ikiwa kuna ubaridi kati yetu, au, mbaya zaidi, hukumu na masengenyo, ni utume gani tunataka kufanya? Tafadhali, tusifanye masengenyo. Masenyenyo ni mdudu, anayeharibu, mdudu anayeua maisha ya jumuiya, ya utaratibu wa shirika la kitawa. Hakuna kufanya masengenyo. Papa amebainisha jinsi ambavyo sio rahisi juu ya  kushinda masengenyo hayo  sio rahisi na mtu ananiuliza: "Lakini jinsi gani inaweza kufanyika? Papa kwa kujibu amesema “ Kuna dawa nzuri sana, nzuri sana: kuuma ulimi wako. Itakutendea mema! Ushuhuda wa upendo wa jumuiya ya kitawa na katika familia ni uthibitisho wa kutangaza kiinjili ni jaribu la moto. Jumuiya nzuri ya nguvu na mahali ambapo panaishi maelewano ya mioyo na amani haiwezekani isiwe pendwa, yenye shauku na inayojenga wote”, alikuwa anasema Padre Orione na kwamba inageuka kuwa ya kuvutia hata miito mipya. Baba Mtakatifu Francisko aidha amependa kurudi katika wosia wa “kujitupa katika moto wa nyakati mpya” . Hii inahitaji kutazama dunia ua leo kwa mtazamo wa mitume, yaani na mang’amuzi lakini kwa shauku, bila kuogopa, bila hukumu, kwa ujasiri: kuutazama kama anavyotazama Mungu , kwa kusikia maumizi yetu, furaha na matumaini ya ubinadamu. Neno linalobaki kuongoza ni lile ambalo Mungu alimwambia Musa “ Nimeona mateso ya watu wangu(…) Nimetalekama kwa ajili ya kuwakomboa ( Es 3,7-8). Lazima kutazama shida za ulikwengu wetu kama sababu ya utume wetu na sio kama kizingiti. 

Papa amekutana na Familia nzima ya karama ya Mtakatifu Luigi Orione
Papa amekutana na Familia nzima ya karama ya Mtakatifu Luigi Orione

Baba Mtakatifu Francisko amekumbusha kuwa mwanzilishi wao alikuwa anasema: “haitoshi kujililia kuhusu huzuni wa nyakati na  watu na haitoshi kusema “ Bwana, bwana! Hakuna kulilia nyakati zilizopita. Hakika sio kuwa na roho ya huzuni na wala roho iliyofungwa. Ni lazima kwenda mbele kwa utulivu na juhudi isiyotingishika”. Kwa maana hiyo nyakati zetu zinatutaka kufungua mipaka mipya, na kugundua mitindo mipya ya utume. Ni kumtazama Bikira Maria aliyekuwa wa kwanza kuanzisha, na wa upole ambaye pamoja na uharaka nyumbani alijiweka katika njia kwenda kumsaidia binamu yake Elizabeth. Na hapo katika huduma Maria alithibitishiwa mpango mzima wa Mungu mpaji. Papa amesema jinsi ambavyo anapenda kusali kwake kwa kusema kama  “ Mama Yesu wa haraka”usipoteze wakati, nenda na ufanye”. Kwa kuhitimisha amewashukuru tena kufika kwa na hasa kwa kile ambacho wao ni na wanafanya. Amebariki kwa moyo wote wao na Jumuiya nzima.

25 June 2022, 14:57