Papa Francisko:Kanisa katika dijitali,liambatane na mafunzo!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Papa Francisko ameandika utangulizi katika kitabu chenye kichwa “Kanisa katika Dijitali, cha mtunzo Fabio Bolzetta ambaye ni mwandishi wa habari na mwendesha vipindi katika Televisheni (TV2000) ya Baraza la Maaskofu Italia. Katika utangulizi huo, Papa amebainisha jinsi ambavyo mara nyingi amerudia kusema kuwa kutoka katika mgogoro inawezekana kutoka wakiwa unafanana kabla , kutoka bora au mbaya zaidi. Katika kipinid kigumu kinachokatishwa na binadamu, kwa sababu ya janga la uviko , limeonesha wazo kuwa sio tu kwamba tutatoka kwenye shida hii ikiwa tutatoka pamoja, lakini imetufanya kuelewa jinsi zana za kiteknolojia na mitandao ya kijamii inaweza kuwa muhimu. Tumeona wakati wa karantini, wakati haikuwezekana tena kukutana, kusherehekea Ekaristi pamoja, kukaa karibu na wapendwa wetu wagonjwa, kuungana katika maombi pamoja na jamaa au rafiki ambaye ametuacha. Ni kana kwamba kila kitu tulichochukua nacho kwa urahisi kimechukuliwa kutoka kwetu, tukikabiliana kimsingi na udhaifu wetu.
Mapadre walitumia teknolojia na mitandao ya kijamii wakati wa janga
Papa Francisko pia amezungumzia juhudi nyingi zilizotumika kuweka mahusiano ya kibinadamu na jamii hai, ikiwa ni pamoja na mapadre waliotumia teknolojia na mitandao ya kijamii kuwaweka watu wa Mungu kuwasiliana na neno lake na kutoa uwezekano wa kuhudhuria Misa mtandaoni. Kiukweli, Papa alisema, mitandao ya kijamii ilitumiwa “kuwasiliana, kuripoti mahitaji, kutuzuia tusijisikie peke yetu, kuamsha mipango ya kiupendo, kuendelea kuonana kwa njia ya mtandao huku tunapongojea kukutana tena uso kwa uso.” Wakati huo pia, Baba Mtakatifu amebainisha kwamba pia kulikuwa na kuna makosa juu ya makosa, lakini jambo muhimu ni kwamba wakatiwa majaribio haya yanaweka ujumbe wa kuwasilishwa katikati, badala ya kimbelembele cha mwasilishaji na lazima tutambue kwamba walikuwa na manufaa.
Wataalam wanasema kuwa mabadiliko ya matumizi haya yatachukua muda mrefu
Baba Mtakatifu anmebainisha kwamba zaidi zaidi, kulingana na wataalam, baadhi ya mabadiliko ambayo yamefanyika kwa sababu ya matumizi ya mara kwa mara ya teknolojia kwa njia ya mikutano ya kawaida yanaweza kubaki kwa muda mrefu baada ya dharura ya janga kumalizika, Papa alisema. Baba Mtakatifu amesisitiza kazi ya Chama cha Wasimamizi wa Mtandao wa Kikatoliki wa Italia (WECA) ambacho kwa muda wa miaka miwili iliyopita, kimekutana na kuwasaidia mapadre wa rika zote wanaojizatiti, hata kwa njia ya teknolojia mpya, kuweka jumuiya zilizokabidhiwa kwao umoja na hivyo kuhamaisha ukuaji wa matumizi ya zana za kidijitali katika uchungaji. Kwa hivyo, kitabu hiki kinatoa mafunzo mengi juu ya Kanisa na mawasiliano ya kidijitali, yaliyoundwa hasa kwa mapadre ambao ukarimu na kujitolea kwao wakati wa dharura ya janga la uviko lazima sasa yaambatane na mafunzo yanayofaa.
Kiukweli kuna mengi ya kujifunza jinsi ya kusikiliza na kuwafunza vijana wazawa wa kidijitali
Kwa kweli kuna mengi ya kufanywa, kukua pamoja katika ufahamu wa umuhimu lakini pia hatari zinazohusika katika kutumia zana hizi. Hii ni kwa sababu kiukweli kuna mengi ya kufanywa ili kujifunza jinsi ya kusikiliza; na kuwashirikisha na kuwafunza vijana, wazawa wa kidijitali ambao wanaweza kufufua tovuti za parokia.” Ingawa mikutano ya mtandaoni haifanyi na kamwe haiwezi kuchukua nafasi ya uzuri wa kukutana ana kwa ana, Papa Francisko ameonesha kwamba ulimwengu wa kidijitali pia unakaliwa na Wakristo ambao “wanaweza kuwa wahusika wakuu wa aina mpya za mawasiliano ya kijamii na zaidi ya kibinadamu, wenye uwezo zaidi kusikiliza na kushiriki kweli.” Hii ni kwa sababu mtandao unaweza pia kuwa nafasi ya kukutana na kusikiliza, ingawa nyakati nyingine sauti zinazopaza sauti kubwa zaidi na uchafuzi wa habari za uwongo huonekana kuwa nyingi. Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza katika utangulizi huo kwamba “Wavuti hautatufanya tujisikie peke yetu ikiwa kweli tunaweza 'kutumia mtandao,' na ikiwa nafasi ya mtandaoni haibadilishi bali inasaidia mtandao wa mahusiano yetu ya kijamii ya mwili na damu,” Papa alisema.