Papa Francisko:Kanisa ni msafara wa ndugu kuelekea umoja
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Papa Francisko Ijumaa tarehe 3 Juni 2022 amekutana na mapadre vijana na wamonaki wa Makanisa ya Kiorthodox ya Mashariki na tamaduni zao. Ameanza na salamu ya Mtakatifu Paulo kwa Wakorinto: “Neema ya Bwana Yesu Kristo, na upendo wa Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote!” ( 2 Wakorintho 13:13). Papa amesema alivyopendelea kuwakaribisha na kuonesha furaha yake ya kutembelewa kwa kutumia salamu hiyo. Maneno ya Mtume mara nyingi hufungua, katika ibada ya Kirumi, ile Sintaksia ya Ekaristi ambayo, anatumaini, wataweza kuadhimisha pamoja siku ambayo Bwana anapenda.
Ziara hiyo imekuja katika kesha la Pentekoste, kwa mujibu wa Kalenda ni Dominika Ijayo. Kwa maana hiyo amependa kuwapa ushauri mfupi kwa mambo manne ambayo yanahusiana na umoja kamili ambao wanachuchumalia. Awali ya yote umoja ni zawadi, moto ambao unakuja kutoka juu. “Tunapaswa kusali bila kuchoka, kufanya kazi, kuzungumza, kujiandalia ili neema hii maalum iweze kukaribishwa. Hata kama ufikiaji wa umoja hautegemei na matunda ya duniani bali ya mbinguni, awali ya yote, ni matokeo ya jitihada, ya juhudi zetu na makubaliano yetu, lakini ya utendaji wa Roho Mtakatifu, ambaye tunapaswa kufungua mioyo yetu kwa uaminifu ili atuongoze kwenye njia za ushirika kamili. Umoja ni neema, zawadi”.
Pili mafundisho ya Penekoste, ambao ni mumoja ni maelewano. Shirikisho lao limeundwa na Makanisa ya kiutamaduni na muungano wa imani na sakramenti, inaonesha vizuri uhalisia huo. Umoja siyo sare na sio tunda la ahasi au udhaifu wa msimamo wa kidiplomasia. Umoja ni maelewano katika tofauti za Karama zilizotoka kwa Roho. Kwa sababu Roho Mtakatifu anapenda kutoa umoja kama Petenkoste, mahali ambapo lugha nyingi hazikupunguzwa kuwa moja lakini zilifanana katika wingi wao. Maelewano ni njia moja ya Roho kwa sababu kama asemavyo Mtakatifu Basili Mkuu kuwa ni maelewano.
Tatu, mafundisho ya Siku ya Pentekoste ambayo ni umoja pia ni safari. Sio mradi wa kuandika, yaani mpango wa kusoma mezani; haufanyiki ukiwa umekaa, lakini katika mwendo mpya ambao ni roho, kuanza na Pentekoste inayouishwa kwa mitume. Inafanyika wakati wa mwendo kwa kufanya kukua katika kushirikisha, hatua kwa hatua katika umoja unawezekana kupokea furaha na ugumu wa safari, mshangao ambao kila mmoja anapitia. Kama vile Mtakatifu Paulo anavyowaandikia Wagalatia kuwa “tunalazimika kuenenda kulingana na Roho (taz. Gal 5:16:25)”. Au, kama Mtakatifu Ireneo asemavyo, ambaye hivi karibuni alimtangaza kuwa Mwalimu wa Umoja kwamba Kanisa ni melodia moja , usemi ambao unaweza kutafsiriwa kama msafara wa Ndugu. Kwa maana hiyo baba Mtakatifu Francisko amesema “Hapa, katika msafara huu, umoja unakua na kukomaa, ambao kulingana na mtindo wa Mungu, hauji kama muujiza wa ghafla na wa kushangaza, lakini katika ushirikiano wa subira na uvumilivu wa safari iliyofanywa pamoja”.
Hatimaye Baba Mtakatifu Francisko akifafanua mantiki ya nne, amesema umoja siyo kitu rahisi peke yake, bali kimefungamana na matunda ya kutangaza. Umoja ni kwa ajili ya utume. Kama Yesu alivyosali kwamba “ili wote wawe kitu kimoja, na ili ulimwengu uamini (Yh 17,21)”. Wakati wa Pentekoste, inazaliwa Kanisa la Kimisionari. Leo hii kwa mara nyingine tena, ulimwengu unasubiri kwa utambuzi pia, kwa kujua Injili ya Upndo, uhisi na amani ambayo sisi sote tunaalikwa kushuhuda kwa mmoja na mwingine na sio dhidi ya mmoja na mwingine au kwa walio mbali na wengine.
Papa Francisko kwa suala hili, anashukuru kwa ushuhuda wa kawaida unaotolewa na Makanisa yao na anadhani kwa namna ya pekee wale na walio wengi ambao wametia muhuri imani yao katika Kristo kwa damu yao. “Asante kwa mbegu zote za upendo na matumaini zilizotawanyika, kwa jina la Msalaba Uliotukuka, katika kanda mbalimbali bado ishara ambazo kwa bahati mbaya, zimegubikwa na vurugu na migogoro ambayo mara nyingi husahaulika.” Papa Francisko ameongeza kusema “ Msalaba wa Kristo uwe dira inayotuongoza katika njia ya kuelekea umoja kamili. Kwa sababu ni juu ya mti huo Kristo, amani yetu, alitupatanisha, akiwakusanya wote katika taifa moja (rej. Efe 2:14)”. Na maana hiyo Baba Mtakatifu ameweka kwenye mikono ya msalaba kwa mawazo, Altare ya umoja, maneno ambayo alitaka kushirikishana nao karibu kama ishara nne za ushirika kamili, ambazo ni: zawadi, maelewano, safari, utume. Amewashukuru tena na kuwahakikisha sala zake na pia kuwaomba nao wamkumbuke katika sala zao na Bwana awabariki na Mama wa Mungu awalinde.