Tafuta

2022.06.04 Papa Francisko akutana na Wjumbe wa Shirikisho linaloshirikisha Mamlaka za Afya za Mitaa, Italia. 2022.06.04 Papa Francisko akutana na Wjumbe wa Shirikisho linaloshirikisha Mamlaka za Afya za Mitaa, Italia. 

Papa Francisko:Kukata rasilimali kwa afya ni chukizo kwa wanadamu

Papa Francisko amependekeza dawa tatu kwa viongozi wa Shirikisho la "Federsanità ili kuhamasisha ushirikiano wa afya ya kijamii na ustawi wa jamii ambazo ni ukaribu,uadilifu na wema wa wote. Magonjwa yanaweza kushika mwili,kuingiza mawazo,kutoa nguvu lakini hayawezi kuondoa kamwe thamani ya maisha ya mwanadamu ambayo yanapaswa yalindwe daima kuanzia kutungwa kwake hadi mwisho wa maisha.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 4 Juni 2022 amekutana mjini Vatican na wajumbe wa Shirikisho linaloshirikisha Mamlaka za Afya za Mitaa, Italia (Confederazione Federsanità). Amemshukuru Rais wake kwa maneno ya hotuba yake. Katika hotuba hiyo Papa emesema amemtaja Mtakatifu Guseppe Moscati kama Msamaria mwema aliyetambua kujikita na mtindo wa utunzaji fungamani, katika eneo alilokuwa akifanya kazi katika fya. Hata Shirikisho lao, linaloshirikisha Mamlaka za Afya za Mahalia, Hospitali  pamoja na Taasisi za kulaza na kutunza zenye tabia ya Kisayansi pamoja na  wawakilishi wa vyama vya  Manispaa  Italia, zina uhusiano wa nguvu katika maeneo na mwendelezo wa kubadilishana kati  ya wilaya, Mkoa na Taifa. Kwa juhudi yao wanachangia kutunza uhusiano kati ya miji na pembezoni, kati ya mdogo na mkubwa kwa kusuka uhusiano na kuhamasisha michakato fungamani kijamii ya kiafya na jamii ya maisha.

Pendekezo la ukaribu na kushinda vishawishi vya kujitosheleza

Kutokana na utambulisho wao  shirikisho hilo  Papa Francisko amependa kupendekeza dawa tatu  ambayo inaweza kuwasadia kutembea katika nyayo zao walizozianzisha.  Awali ya yote, amesema ukaribu ni dawa ya kushinda kujitosheleza. Kwa kumwona mgonjwa ni kama mimi mwenyewe anayekata mnyororo wa ubinafsi, kwa kuwa kisimamio ambacho wakati mwingine tunajaribiwa kupanda na kuzuia kumjua ndugu, kuanzia na lugha yake, mahali anapotokea kijiogafia, hali yake kijamii au hali ya kiafya. Ikiwa katika mtu ambaye tunakutana naye kwenye njia za Hospitali, katika vituo vya kutunza, katika zahanati tunatambua awali ya yote kumwona kaka na dada, hapo inabadilisha kila kitu. Ni kuchukulia mzima kwa  kuacha  masuala ya ukiritimba na kuwa na mkutano,  kusindikiza na kushirikisha. Papa Francisko amesema,  Mungu wetu ni wa karibu, ambaye alichagua kuwa katika mwili wetu, sio Mungu wa mbali hasiyefikiwa, anatembea na sisi, katika njia zenye kiu ya ulimwengu huu, kama alivyofanya na mitume wa Emau (Lk 24,13-32), ambaye anaacha kusikiliza mahangaiko, mateso, huzuni, na kilio cha uchungu wa kila mmoja. Kwetu  sisi anataka tufanye hivyo hivyo.  Na hivyo ni muhimu unapokutana na  mgonjwa  na mateso. Kuwa karibu ina maana  ya kuondoa umbali  na kufanya kila njia kwamba, pasiwepo na mgojwa wa daraja la ‘A’ na la ‘B’ na kuweka mkakati wa mzunguko na rasimali ili kila mmoja asitengwa na utunzwaji wa afya kijamii. Papa Francisko ameongeza: “Kwa hiyo kile Rais alichokumbuka kuhusu afya ya umma: nchi inapopoteza utajiri huu ambao ni afya ya umma, huanza kuleta tofauti kati ya watu; wale wanaoweza kupata, wanaoweza kupata huduma za afya, kwa fedha, na wale ambao hawana huduma za afya. Kwa sababu hii, hapa nchini Italia, afya ya umma ni hazina yao: msiipoteze, tafadhali, msiipoteze!

Pendekezo la dawa ya pili ufungamanishwaji

Papa Francisko amependekeza dawa ya pili ambayo ni  uadilifu wa ufungamanishwaji ambao unastahili katika  msuko wa dunia hii. Ikiwa kila kitu kimeunganishwa, lazima kufikiria mantiki ya afya katika mtazamo wa ufungamanishwaji ambao unakumbatia kila hali ya mwanadamu, amesisitiza Papa. Bila kupunguza thamani ya ujuzi maalum, kutibu mgonjwa ina maana ya kuzingatia si tu asili ya ugonjwa (patholojia) fulani, lakini hali yake ya kisaikolojia, kijamii, kiutamaduni na kiroho. Yesu anapomponya mtu, pamoja na kutokomeza uovu wa kimwili kutoka kwa mwili wake, anarudisha heshima yake, kumrudisha katika jamii, kumpa maisha mapya. Bila shaka, ni Yeye pekee anayeweza kufanya hilo, lakini mtazamo, mbinu kwa mtu ni kielelezo kwetu. Maono kamili ya utunzaji husaidia kutofautisha "utamaduni wa kutupa", ambao haujumuishi wale ambao, kwa sababu tofauti, hawafikii viwango fulani. Katika jamii ambayo inahatarisha kuona wagonjwa kama mzigo, gharama, ni muhimu kuweka katikati kile kisicho na bei, kisichoweza kununuliwa au kuuzwa, ambacho ni hadhi na utu wa mtu. Magonjwa yanaweze kushika mwili, kuingiza mawazo, kutoa nguvu lakini hayaweze kuondoa kamwe thamani ya maisha ya mwanadamu ambayo yanapaswa yalindwe daima kuanzia kutungwa kwake hadi mwisho wa maisha.. Na ndiyo papa Francisko amewatakia kwamba utafiiti na taaluma mbali mbali za kiafya ziweze daima kuwa na upeo huo.

Pendekezo la tatu ni dawa ya kufanya kazi kwa ajili ya wema wa pamoja

Muktadha wa tatu  ambao Papa amependekeza ni wema wa pamoja ambao kama dawa ya kuachilia matakwa binafsi. Hata katika nyanja ya kiafya, kuna vishawishi vilivyopo vya kuona zaidi wenye kuleta faida kiuchumi au kisiasa kwa kila kikundi kuhsiana na sehemu kubwa ya watu. Na hiyo ni sawa hata juu ya mipango ya kimataifa. Papa Francisko amesema haki msingi wa kutetea afya, katika Mkataba wa Wahudumu wa Kiafya: “inahusu thamani ya haki, ambayo kulingana nayo hakuna tofauti kati ya watu na mataifa, kwa kuzingatia hali ya lengo la maisha na maendeleo ya sawa, katika kutafuta manufaa ya wote, ambayo wakati huo huo ni wema wa kila mmoja” ( 141). Janga la uviko, limetufundishwa kuwa kujiokoa inavyowezekana, na ambayo inatafsiriwa hata kuwa wote dhidi ya wote, kupanua mkasi wa ukosefu wa usawa na kuongezeka kwa migogoro. Inahitajika kufanya kazi kwa sababu wote waweze kupata matibabu, na kwa sababu mfumo wa kiafya uweze kusaidia na kuhamasisha, na pia kwa sababu uendelee kuwa wa bure. “Kukata rasilimali kwa afya ni chukizo kwa wanadamu”.  Ukaribu, ufungamanishwaji na wema wa pamoja, ndio mambo matatu ambayo Papa Francisko amewatakia matashi mema  na kama dawa ambayo anawatia moyo wa kuendelea kufanya huduma kwa wagonjwa, na wa ubinadamu wote. Mtakatifu Yosefu Moscati, awalinde katika kazi yao kila siku na kuwapa hekima ya kutunza na kulinda.

04 June 2022, 14:27