Papa Francisko:kushuhudia Yesu hata katika udhaifu wa uzee

Katika Katekesi ya Papa kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro,amejikita na mada ya udhaifu wa uzeee unaosababisha utegemezi kwa wengine."Wazee hawapaswi kuwaonea wivu vijana wanaochukua nafasi zao,hata wafuasi wasiotenda kwa lazima,wa kutafakari kihisia na kusikiliza kwa bidii neno la Bwana,kama lile la Maria,dada yake Lazaro,watakuwa sehemu bora zaidi ya maisha yao na maisha yetu sisi wazee”.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, akiendelea na mchakato wa katekesi yake kuhusu  Uzee , amejikita juu ya mazungumzo kati ya Yesu Mfufuko na Petro katika hitimisho la Injili ya Yohane 21,15-23, Jumatano tarehe 22 Juni 2022. Baba Mtakatifu amesema kuwa ni mazungumza yanayo yanayogusa ambamo yanaweka wazi, upendo wote wa Yesu kwa wafuasi wake na hata juu ya uhusiano wa ubinadamu wake na wao na kwa namna ya pekee na Petro. Kuwa na uhusiano mzuri lakini si wepesi, moja kwa moja, nguvu, bure, na wazi. Uhusiano kwa watu na katika ukweli. Kwa hiyo, Injili ya Yohana, ya kiroho sana, ya juu sana, inafunga katika ombi kuu na toleo la upendo kati ya Yesu na Petro, ambalo linaunganishwa, kwa kawaida kabisa, na majadiliano kati yao. Mwinjili anatuonya: anashuhudia ukweli wa mambo (rej. Yn 21:24).

Papa akiwa na watoto wa Ukraine wakati wa kusalimu waamini waliokuwa katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Papa akiwa na watoto wa Ukraine wakati wa kusalimu waamini waliokuwa katika uwanja wa Mtakatifu Petro

Na ni ndani yao kwamba ukweli lazima utafutwe. Papa ameomba kujiuliza iwapo tunao uwezo wa kulinda sauti kuuu kati ya Yesu na wafuasi wake kwa  mujibu wa mtindo ulio wazi wa moja kwa moja na wa kweli na hali kibinadamu? Jinis gani uhusiano wetu na Yesu ulivyo? Na kama ulivyo ule wa mitume na Yeye. Papa ameomba kujiuliza kama, sisi hatujaribiwi mara nyingi sana kujifungia ushuhuda wa Injili katika ufunuo wa sukari, ambao tunaongeza heshima yetu kwa tukio hilo? Mtazamo huu, unaoonekana kuwa wa heshima, kwa hakika unatuweka mbali na Yesu wa kweli, na hata unakuwa tukio la safari ya imani ya kidunia isiyoeleweka sana, inayojielekezea sana, ya kiulimwengu sana, ambayo si njia ya Yesu. Yesu ndiye Neno wa Mungu aliyemuumba mwanadamu, na anatenda kama mwanadamu, anazungumza nasi kama mwanadamu, Mungu-mtu. Kwa huruma hii, na urafiki huu, na ukaribu huu. Yesu sio kama picha hiyo ya sukari ya picha ndogo, hapana: Yesu yuko mikononi mwetu, yuko karibu nasi.

Katekesi ya Papa 22 Juni 2022
Katekesi ya Papa 22 Juni 2022

Katika mazungumzo ya Yesu pamoja na Petro, tunapata mafungu mawili yanayohusiana kwa usahihi na uzee na kipindi cha  wakati, yaani muda wa  kutoa ushuhuda, na wakati wa maisha. Hatua ya kwanza ni onyo la Yesu kwa Petro, kwamba ulipokuwa kijana ulikuwa unajitosheleza, utakapokuwa mzee hutaweza tena kujitawala mwenyewe na maisha yako. Papa kwa kusema ukweli ametoa mfano wa hali  halisi yake ambaye kwa sasa anatembea na kiti cha magurudumu. "Lakini ndio hivyo, maisha ni kama haya na uzee unapata magonjwa haya yote na lazima kuyakubali yanapokuja. Wazee hanawana nguvu kama vijana. Lakini na ushuhuda wake, Yesu anasema kwamba utasindikizana na udhaifu huu. Lazima uwe shuhuda wa Yesu hata katika udhaifu, katika magonjwa na kifo", papa amebainisha.

Katekesi ya Papa 22 Juni 2022
Katekesi ya Papa 22 Juni 2022

Kuna kifungu kizuri kutoka kwa Mtakatifu Ignatius wa Loyola ambaye anayesema: “Kama vile katika maisha, hata katika kifo lazima tushuhudie kama wanafunzi wa Yesu". Mwisho wa maisha lazima uwe mwisho wa maisha ya wanafunzi: ya wanafunzi wa Yesu, ambao  Bwana daima anazungumza nasi kulingana na umri wetu. Mwinjili anaongeza maelezo yake, akieleza kwamba Yesu alirejea ushuhuda uliokithiri, ule wa kufia imani. Lakini tunaweza kuelewa vizuri maana ya onyo hili kwa ujumla zaidi na wafuasi wake watalazimika kujifunza kujiruhusu kufundishwa na kutengenezwa na udhaifu wao, kutokuwa na uwezo wao, utegemezi wao kwa wengine, hata katika kuvaa na katika kutembea.

Katekesi ya Papa 22 Juni 2022
Katekesi ya Papa 22 Juni 2022

Lakini ninyi “nifuateni” Baba ameongeza “ Kumfuasa Yesu daima kunaendelea, na afya njema, na afya mbaya, kujitegemea, si kwa kujitosheleza kimwili, lakini kumfuata Yesu ni muhimu kwa sababu inawezakana  kumfuata Yesu daima, kwa miguu, kukimbia, polepole, kwa kiti cha magurudumu, lakini daimani kumfuata. Hekima ya kufuata lazima itafute njia ya kubaki katika ungamo lake la imani na hivyo Petro akajibu: “Bwana, wewe wajua ya kuwa nakupenda” (rej.15.16.17), hata katika hali zenye mipaka za udhaifu na uzee. Baba Mtakatifu Francisko amedhihirisha jinsi ambavyo anapenda kuzungumza na wazee akiwa anatazamana nao machoni kwa sababu wana macho makali, macho hayo ambayo yanazungumza na wewe zaidi ya maneno na ushuhuda wa maisha. Na hii ni nzuri, hivyo tunapaswa kuitunza hadi mwisho. "Mfuate Yesu hivyo, mkiwa mmejaa maisha", amebainisha Papa.

Katekesi ya Papa 22 Juni 2022
Katekesi ya Papa 22 Juni 2022

Maisha ya wazee ni kuaga, polepole, lakini kuaga kwa furaha. Papa kwa kutoa mfano mwenyine amesema: Niliishi maisha yangu, nilihifadhi imani yangu”. Hii ni nzuri wakati mzee anaweza kusema hivyo kwamba aliishi maisha, na hiyo  ni familia yake. Aliishi maisha yake, alikuwa mwenye dhambi lakini pia alifanya mema”. Na hii amani inayokuja, hiyo ni ndiyo kwaheri ya wazee”. “Hata wafuasi wasiotenda kwa lazima, wa kutafakari kihisia na kusikiliza kwa bidii neno la Bwana, kama lile la Maria, dada yake Lazaro, watakuwa sehemu bora zaidi ya maisha yao, ya maisha yetu sisi wazee”. Kwamba sehemu hii haitaondolewa kamwe kutoka kwetu (rej. Lk 10:42). Tuwaangalie wazee, tuwasaidie ili waweze kuishi na kueleza hekima yao ya maisha, watupatie walichonacho cha uzuri na wema. Hebu tuwaangalie, tuwasikilize. Na sisi wazee, tunavyo waangalia vijana na daima tunatabasamu, kwa vijana: watafuata njia, watafanya kile tulichopanda, hata kile ambacho hatujapanda kwa sababu hatukuwa na ujasiri au fursa, wataendelea nacho. Lakini daima kuwepo uhusiano huo. Mzee hawezi kuwa na furaha bila kuwatazama vijana na vijana hawawezi kuendelea na maisha bila kuwaangalia wazee.

KATEKESI YA PAPA 22 JUNI 2022
22 June 2022, 16:19