Tafuta

2022.06.10 Papa amekutana na Bi Ursula von der Leyen, Rais wa Tume ya Ulaya. 2022.06.10 Papa amekutana na Bi Ursula von der Leyen, Rais wa Tume ya Ulaya. 

Papa Francisko na Bi Von der Leyen kuungana kumaliza vita nchini Ukraine

Katika mazungumzo mjini Vatican,Ijumaa Juni 10 kati ya Papa na Rais wa Tume ya Ulaya,wamejikita katika umakini kuhusu mantiki ya kibinadamu iliyosababishwa na migogoro.

Vatican News.

Papa Francisko Ijumaa tarehe 9 Juni 2022 amekutana katika Jumba la Kitume, Vatican na Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Bi Ursula von der Leyen, ambaye mara baada ya mkutano huo pia akakutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, akisindikizana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Nchi na Mashirikia ya Kimataifa.

Papa Francisko na Rais wa Tume ya Ulaya na wasindikizaji wenzake
Papa Francisko na Rais wa Tume ya Ulaya na wasindikizaji wenzake

Katika mazungumzo yao na Katibu wa Vatican, wamesisitiza juu ya mahusiano mema yaliyopo kwa sehemu mbili na juu ya jitihada za pamoja kwa ajili ya kufanya kuisha mwisho wa vita nchini Ukraine, kwa namna ya pekee umakini wa mantiki za kibinadamu na matokeo mabaya ya vyakula ambayo yamekuwa sababu pia ya migogoro.

Papa Francisko na Rais wa Tume ya Ulaya
Papa Francisko na Rais wa Tume ya Ulaya

Wakiendelea na mazungumzo hayo  aidha, wamezungumzia hitimisho la Mkutano Kuhusu Wakati ujoa wa Ulaya na Matokeo yake kwa nyakati zijazo muungano wa Umoja wa Ulaya.

Katibu wa Vatican na Rais wa Tume ya Ulaya
Katibu wa Vatican na Rais wa Tume ya Ulaya

Na kwa mujibu wa Msemaji wa Vyombo vya habari Dk. Matteo  Bruni amewambia wandishi wa habari akizungumza kuhusu Mkutano kati ya Papa na Bi Ursula von der Leyen amesema kwamba: “ Hata na Papa wamezungumzia vita vya Ukraine, hali ya tabianchi na usanifu endelevu".

Zawadi

Katika ubadilishanaji wa zawadi za kiutamaduni, Papa alitoa picha ya shaba inayoonesha mikono miwili inayoshikilia msingi wa nguzo ya Mtakatifu Petro, pamoja na mwanamke mwenye mtoto na meli ya wahamiaji na maandishi: "Hebu tujaze mikono ya wahamiaji katika mikono mingine". Pia kama zawadi nyingine ni vya  Ujumbe wa Amani wa mwaka huu, Hati juu ya Udugu wa Amani na  kitabu cha Statio Orbis cha tarehe 27 Machi 2020, kilichohaririwa na LEV na juzuu la Ghorofa ya Kipapa. Na kwa upande wa Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya alitoa kitabu kuhusu shule ya Bauhaus na picha ya mpango unaolenga mipango endelevu ya miji.

Papa wakati wa kupena zawadi na Rai wa Tume ya Umoja wa Ulaya
Papa wakati wa kupena zawadi na Rai wa Tume ya Umoja wa Ulaya

Tweet ya Von der Leyen

Katika ujumbe wake mfupi kwa Twitter Bi Urusula aliandika: "Nimefurahi sana kukutana na Baba Mtakatifu Francisko tena huko Roma. Tuko pamoja na wale wanaoteseka kutokana na maangamizi huko Ukraine. Vita hivi lazima vikome, na kurudisha amani Ulaya". Hata hivyo ikumbukwe kwamba Bi Von der Leyen alikuwa amekutana na Papa mnamo tarehe 22 Mei 2021, na wakawa wamezungumzia juu ya athari kubwa za janga la uviko, suala la wahamiaji na shida ya hali ya tabianchi.

10 June 2022, 16:22