Papa hataadhimisha Misa ya na Maandamano ya Corpus Domini
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Ka mujibu wa taarifa kuttoka makao makuu ya vyombo vya habari, wamesema: “Kutokana na hali halisi ya kiafya kwa Papa Francisko kuhusu goti na kwa umuhimu sana wa liturujia ya sherehe za Ekaristi katika fursa ya Siku kuu ya Mwili na Damu ya Yesu Kristo hataweza kufanya hivyo”. Hii ni kutokana na kwamba maumivu ya goti ambayo yamekuwa yakiathiri hata ratiba ya Papa kwa siku nyingi, kwa hivi karibuni kuahirishwa kwa safari ya kitume barani Afrika iliyokuwa imepangwa kufanyika wiki ya kwanza ya Julai, kunarejea tena hata kubadilishwa kwa liturujia za sherehe za Kipapa. Sherehe ya Mwili na Damu Yesu Kristo pamoja na maandamano ambayo ni mojawapo ya siku ya dhati kabisa, kiini cha maombi ambayo chimbuko lake ni katika karne ya kumi na tatu haitaweza kuadhinishwa na Papa.
Siku Kuu ya Mwili na Damu ya Yesu 16 Juni 2022
Hayo yote yameelezwa Jumatatu tarehe 13 Juni 2022 kwa Ofisi ya Habari ya Vatican kwa waandishi wa habari na kufahamisha kwamba: “kutokana na mapungufu yaliyopo ya kiafya ya Papa hasa kwa goti na kufuatia na mahitaji maalum ya kiliturujia ya adhimisho hilo, Misa Takatifu na Maandamano hayataadhimishwa kwa Baraka ya Ekaristi wakati wa Sikukuu ya Mwili na Damu ya Yesu Corpus Domini” .
Maadhimisho wakati wa Janga la Uviko katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro
Hata hivyo, sio tu nia ya kutaka kulinda matokeo ambayo matibabu ya yanaendelea kuleta lakini pia hata sherehe yenyewe inayohitajika sana na ambayo ni muhimu, ambayo itafanyika Alhamisi tarehe 16 Juni. Tayari katika miaka miwili iliyopita, kutokana na tishio la janga la Uviko-19, Misa ya Maadhimisho inayothibitishwa uhalisi wa Yesu katika Ekaristi ilikuwa imeadhimishwa katika kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na waashiriki waamini wachahche na sio katika eneo la kiutamaduni kwenye Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane huko Laterano Roma na maandamano ya kwenda Mtakatifu Maria Mkuu, au hata katika maeneo ya mijini kama ilivyotokea mnamo 2018, huko Ostia,na mnamo 2019, huko Casal Bertone.