Tafuta

Papa:Katika nyakati zetu kwa nini uzee kwa njia nyingi unadharauliwa?

Nikodemo anaelewa vibaya kuzaliwa huku,na anatilia shaka uzee kama uthibitisho wa kutowezekana kwake:mwanadamu anazeeka,ndoto ya ujana wa milele hutoweka kabisa.Imani inayopokea tangazo la kiinjili la Ufalme wa Mungu ambamo sisi tunaelekea,ina matokeo ya ajabu ya kwanza,kama asemavyo Yesu.Inaturuhusu “kuona” ufalme wa Mungu.Ni katika tafakari ya Katekesi ya Papa kuhusu uzee.

Na Angella Rwezaula- Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika mwendelezo wa Katekesi yake kuhusu “Uzee”, Jumatano tarehe 8 Juni 2022 ameongozwa na kifungu cha Injili ya Yohane 3,4 kinachoeleza juu ya Nikodemu aliyeuliza swali  Yesu kuhsu  kuzaliwa kwa upya wakati akiwa mzee, kwa waamini na wanahija waliounganika katika uwanja wa Mtakatifu Petro, Jijini Vatica. Papa akianza amesema “Kati ya sura  za wazee ambazo zinaonekana katika Injili kuna Nikodemu mmoja wa wakuu wa Wayahudi ambaye kwa kutaka kujua alikwenda  usku kwake Yesu akiwa amejificha. (Yh 3,1-21). Katika mazungumzo na Yesu na Nikodemu, inajionesha  moyo wazi wa Yesu na utume wake wa ukombozi, anaposema kuwa: “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” (Yh 3,16).

Katekesi ya Papa 8 Juni 2022
Katekesi ya Papa 8 Juni 2022

Yesu alimwambia Nikodemu kuwa ili kumwona Mungu lazima azaliwe mara ya pili kutoka juu. Hii haina maana ya kuanza mwanzo wa kuzaliwa, kurudia mahali ambapo tulikuja ulimwenguni, kwa kuamini kuwa kwa kurudi tumboni, ni kufungua uwezekano wetu wa kuwa na maisha bora.  Kurudia huku kusingekuwa na maana. Badala yake kungeweza kuondoa maana ya kuishi, kufuta na kama vile uzoefu huo kushindwa, thamani iliyoharibika, utupu wa kupoteza.  Ni kinyume na hiyo. Maisha haya ni yenye thamani mbele ya Mungu: yanatutambulisha kama viumbe waliopendwa na Yeye kwa huruma. Kuzaliwa kutoka juu, kunakotuwezesha kungia katika ufalme wa Mungu ni kizazi katika Roho, hatua  kati ya maji kuelekea dunia iliyohaidiwa na uumbaji uliopatanishwa na upendo wa Mungu. Mi kuzaliwa upya kutoka juu, kwa neema ya Mungu.Sio kuzaliwa kimwili kwa mara nyingine tena.

Katekesi ya Papa 8 Juni 2022
Katekesi ya Papa 8 Juni 2022

Nikodemo anaelewa vibaya kuzaliwa huku, na anatilia shaka uzee kama uthibitisho wa kutowezekana kwake: mwanadamu anazeeka, ndoto ya ujana wa milele hutoweka kabisa. Papa ameuliza kuwa anawezaje kuwazia hatima ambayo ina namna ya kuzaliwa? Nikodemu anafikiri hivyo na hapati njia ya kuelewa maneno ya Yesu maana ya  kuzaliwa upya maana yake nini? Kupinga kwa Nikodemu ni fundisho kwetu. Taweza kiukweli kuupindua, katika mwanga wa Neno la Mungu, katika ugunduzi wa utume hasa wa uzee. Kiukweli kuwa mzee sio kizingiti tu cha kuzaliwa kutoka juu ambako anazungumza Yesu, lakini unageuka kuwa fura ya kuunganisha, kuufungua na ukosefu wa matumaini yaliyoisha.

Katekesi ya Papa 8 Juni 2022
Katekesi ya Papa 8 Juni 2022

Katika nyakati zetu na utamadunu wetu, ambao uanonesha tabia ya wasi wasi wa kufikiria kuzaliwa kwa mtoto kama masuala rahisi ya uzalishaji na uzazi wa kibayolojia wa binadamu, kisha kukuza hadithi ya ujana wa milele kwa kulazimisha, kukata tamaa ya mwili usioharibika. Kwa nini uzee kwa njia nyingi unadharauliwa? Kwa sababu unaleta ushahidi usio na shaka wa kufukuzwa kwa hadithi hiyo ambayo ingependa kutufanya turudi kwenye tumbo la mama, ili daima kurudia kuwa vijana katika mwili. Mbinu hiyo inajiwezesha kuvutiwa na hadithi hii kwa njia zote: wakati wa kusubiri kushindwa kifo, tunaweza kuweka mwili hai na dawa na vipodozi, ambayo hupunguza kasi, kujificha, kuondoa uzee. Kwa kweli, ustawi ni jambo moja, kulisha hadithi ni tofauti kabisa. Hata hivyo, haiwezi kukataliwa kwamba mkanganyiko kati ya vipengele hivi viwili unaleta mkanganyiko fulani wa kiakili. Mengi yanafanywa ili kumrejesha kijana huyo kila wakati: hila nyingi, upasuaji mwingi ili kuonekana kijana, Papa amebainisha. Kwa kuongeza Papa amesema: “ Nakumbuka maneno ya mwigizaji wa Kiitaliano mwenye busara, Magnani, walipomwambia kwamba wanapaswa kuondoa makunyanzi yake, na akasema: “Hapana, msiyaguse! yalichukua miaka mingi kuyapata: msiyaguse!

Katekesi ya Papa 8 Juni 2022
Katekesi ya Papa 8 Juni 2022

Papa Francisko ameongeza kusema “Ndiyo hayo: makunyanzi ni ishara ya uzoefu, ishara ya maisha, ishara ya ukomavu, ishara ya kuwa na safari. Msiyaguse ili yawe kijana, lakini kijana  usoni: kinachokuvutia ni utu wote, kinachokuvutia ni moyo, na moyo unabaki na ujana wa divai nzuri, ambayo inakua bora zaidi”.  Aidha amefafanua papa kuwa “Uzima  katika mwili wa kufa ni uzuri ambao haujakamilika: kama kazi fulani za sanaa ambazo zina uzuri wa kipekee kwa kutokamilika kwao. Kwa sababu maisha hapa chini ni ‘jando’, sio utimilifu: tunakuja ulimwenguni kama hivyo, kama watu halisi, kama watu wanaoendelea kukua kiumri, lakini ni wa kweli milele. Lakini maisha katika mwili wa kufa ni nafasi ndogo sana na wakati wa kuweka sawa na kutimiza sehemu ya thamani zaidi ya uwepo wetu katika wakati wa ulimwengu.

Katekesi ya Papa 8 Juni 2022
Katekesi ya Papa 8 Juni 2022

Imani ambayo inayopokea tangazo la kiinjili la Ufalme wa Mungu ambamo sisi tunaelekea, ina matokeo ya ajabu ya kwanza,  kama asemavyo Yesu. Inaturuhusu “kuona” ufalme wa Mungu.Tunakuwa na uwezo wa kuona kwa hakika ishara nyingi za kukadiria za tumaini letu la utimilifu wa kile, katika maisha yetu, kinabeba ishara ya hatima kwa ajili ya umilele wa Mungu. Ishara ni zile za upendo wa kiinjili, unaoangazwa kwa njia nyingi na Yesu. Na kama tunaweza kuziona tunaweza pia kuingia” katika ufalme, kwa njia ya Roho kupitia maji ya kuzaliwa upya. Uzee ni hali, iliyotolewa kwa wengi wetu, ambayo muujiza wa kuzaliwa huku kutoka juu unaweza kuunganishwa kwa karibu na kufanywa kuaminika kwa jamii ya wanadamu: haiwasiliani na yale ya zamani ya  kuzaliwa kwa muda, lakini upendo kwa marudio ya mwisho. Kwa mtazamo huu, uzee una uzuri wa kipekee: tunatembea kuelekea Milele.

08 June 2022, 15:57