Tafuta

2022.06.17 Papa na Uwakilisho wa Kibudha wa Sangha ya Chetuphon 2022.06.17 Papa na Uwakilisho wa Kibudha wa Sangha ya Chetuphon 

Papa kwa Wabudha:Kuna ulazima wa mazungumzo kuliko awali katika dunia iliyo na migogoro!

Papa Francisko amekutana na uwakilishi wa Wabudha kutoka Thailand waliojumuisha wamonaki wa kibudha 33 wa Shule ya Theravada na Mahayana na wabudha 60 walei na wawakilishi wa Kanisa katoliki Thailand,katika fursa ya miaka 50 ya mkutano wa kihistoria wa XVII kati ya Mkuu wa kibudha nchini Thailand na Papa Paulo VI mnamo Juni 5,1972.Papa amesema uwepo wa ukuaji wa mazungumzo na ushirikiano kati ya tamaduni mbili za kidini yanayohitajika katika ulimwengu wa leo.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Ijumaa tarehe 17 Juni 2022 amekutana na uwakilishi wa Wabudha kutoka Thailand ambao ulikuwa unajumuisha wamonaki wa kibudha 33 wa Shule ya Theravada na Mahayana na  wabudha 60 walei na wawakilishi wa Kanisa katoliki nchini Thailand. Dhumuni la ziara yao ni kufanya kumbu kumbu ya miaka 50 ya Mkutano XVII wa kihistoria wa mheshimiwa sana Somdej Phra Wannarat, na Upatriaki mkuu wa Kibudha huko Thailand na Papa Mtakatifu Paulo VI mnamo tarehe 5 Juni 1972. Baba Mtakatifu Francsiko ameelezea hisia zake za shukurani kwa Patriaki Mkuu Somdej Phra Sri Ariyavongsagatanana IX na Kiongozi mkuu wa Sangha Supremo ya Thailand kwa kumtuma Somdej Phra MahaTheerajarn na uwakilishi wa Thailand jijini Vatican kwa kupyaisha uhusiano wao wa urafiki na kushirikiana kwa pamoja.

Papa Francisko na Uwakilisho wa Kibudha wa Baraza la Sangha ya Chetuphon
Papa Francisko na Uwakilisho wa Kibudha wa Baraza la Sangha ya Chetuphon

Katika fursa hiyo, Baba Mtakatifu amependa kupyaisha hisia za Papa Paulo VI alikutana na Uwakilishi wa Thailand miaka 50 iliyopita kwamba “Tuna tafakari ya kina kwa ajili ya hazina za kiroho, kimaadili na kijamii na kiutamaduni ambazo mmepewa kupitia tamaduni za thamani. Tunatambua maadili ambayo ninyi ni wasimamizi wake na tunashirikishana shauku ya kuhifadhiwa na kuhamasishwa. Tunatazamia kuwa na mazungumzo ya kirafiki zaidi na ushirikiano wa karibu kati ya tamaduni mnazowakilisha na Kanisa Katoliki(Mafundisho, 1972, X, 604-605). Katika mchakato wa miaka 50 Papa Francisko amebainisha kuona ukuaji hatua kwa hatua na endelevu wa mazungumzo ya kirafiki na ushirikiano wa bega kwa bega kati ya tamaduni zote mbili za kidini. Papa mekumbuka ziara uwakilishi wao uliofanyika mnamo tarehe 16 Mei 2018 na tamaduni za kizamani za maandiko ya kibudha kwa lugha ya kipali, ambayo imehifadhiwa katika Maktaba ya Vatican. Na bado anayo kumbu kumbu hai ya ziara yake katika nchi yao pendwa mnamo tarehe 20-23 Novemba 2019, na mshangao mkubwa wa makaribisho na ukarimu alioupokea. Papa amepongeza pia urafiki wao na mazungumzo ya kidugu na wajumbe wa Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya kidini na Jumuiya katoliki nchini Thailand.

Papa Francisko na Uwakilisho wa Kibudha wa Baraza la Sangha ya Chetuphon
Papa Francisko na Uwakilisho wa Kibudha wa Baraza la Sangha ya Chetuphon

Katika wakati huu ambao familia ya binadamu na sayari inajikuta kukabiliana na hatari nyingi, mazungumzo ya kirafiki na ushirikano wa bega kwa bega ndio vitu bado ni muhimu zadi. Kwa bahati mbaya kila sehemu ya ulimwengu inasikika ubanadamu uliojeruhiwa na dunia iliyogawanyika. Budha na Yesu walielewa ulazima wa kushinda ubinafsi ambao unaibua migororo na vurugu. Tasaufi ya Dhammapada inakusanya mafundisho hayo ya Budha: “kuepuka ubaya, kukuza wema na kutakasa akili binafsi ndiyo mafundisho ya Budha” (Dph 183). Na Yesu aliwambia wafuasi wake:“Ninawapa amri kuu mpya; pendaneni (Yh 13,34). "Ndiyo kazi yetu leo hii ya kuongoza sehemu zetu mbili za waamini wetu kwa maana  iliyo hai kabisa ya ukweli ambao sisi sote ni kaka na dada. Na hii inapelekea  ulazima wa kufanya kazi pamoja kwa ajili ya kukuza huduma na ukarimu kwa ajili ya binadamu wote hasa wale maskini na waliobaguliwa".

Papa Francisko na Uwakilisho wa Kibudha wa Baraza la Sangha ya Chetuphon
Papa Francisko na Uwakilisho wa Kibudha wa Baraza la Sangha ya Chetuphon

Katika roho hiyo "ninawatia moyo juhudi zetu kutafakari kwa kina na kupanua mazungumzo na mshikamano na Kanisa Katoliki". Papa Francisko amewashukuru kwa upya  kwa ishara hiyo ya kutembelea Vatican ili kufanya kumbu kumbu isiyofutika kati ya Watangulizi wao. Kwa kuwatakia heri ya ziara yao jijini Roma Papa amewatakia matashi mema ya mkutano ambao walikuwa waufanye mchana huo ukiongozwa na mada: “Urafiki kati ya Wabudha na wakristo kwa ajili ya utamaduni wa kukutana"  uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Kipapa Urbaniana. Amehitimishwa kwa kuwabariki nchi yao pendwa na wakazi wake wote.

HOTUBA YA PAPA KWA WAWAKILISHI WA WABUDHA KUTOKA THAILAND
17 June 2022, 16:19